CHADEMA Kufungua kesi Mahakamani kupinga Jeshi la Polisi ‘kumteka’ Twaha Mwaipaya

BAVICHA Taifa

Senior Member
Jul 25, 2013
117
661
Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) limesikitishwa kuendelea kushikiliwa kwa Mratibu wa Uhamasishaji Bavicha Taifa Ndugu Twaha Mwaipaya na Jeshi la Polisi. Twaha Mwaipaya alikamatwa Juni 30, 2022 na Jeshi la Polisi Morogoro mjini, ambao kesho yake ya Julai Mosi, 2022 walidai kuwa amesafirishwa kwenda Dodoma. Julai Mosi, 2022 na Julai 02, 2022 viongozi wa chama waliopo Dodoma walizunguka vituo vyote vya polisi bila mafanikio. Leo ni si siku ya tatu tangu kukamatwa kwa Ndugu Twaha Mwaipaya.

Jana Julai 02, 2022 saa sita mchana Jeshi la Polisi likiwa na Twaha Mwaipaya walifika nyumbani kwake Kisewe Mbagala, Dar es salaam kufanya upekuzi. Baada ya upekuzi huo hawakuondoka na chochote, ila hawakuwa tayari kueleza wanamshikilia katika kituo gani.

Aidha, leo Julai 03, 2022 viongozi wa Bavicha Taifa wamezunguka vituo vyote vikubwa vya Polisi Dar es salaam na kuambiwa kuwa ndugu Twaha hayupo, isipokuwa kituo cha Polisi Mburahati. Viongozi hao walipofika Kituo cha Polisi Mburahati walijibiwa kuwa Ndugu Twaha Mwaipaya ametolewa asubuhi ya leo kituoni hapo kupelekwa Dodoma. Pia kuna taarifa kuwa Ndugu Twaha bado anashikiliwa katika kituo hicho cha Mburahati.

Jeshi la Polisi kuendelea kumshikilia Ndugu Twaha Mwaipaya kwa siku tatu bila kupewa dhamana au kupelekwa mahakamani ni kinyume cha sheria. Hivyo, Jeshi la Polisi limuachie huru au limpatie dhamana. Bavicha tunalitaka Jeshi la Polisi lijitokeze kueleza yuko mkoa gani na kituo gani cha polisi pamoja na kutoa nafasi kwa uongozi wa Chama, familia yake na mawakili kuweza kumuona kujua hali yake na kulinda haki zake.

Baraza limewasilisha taarifa hiyo kwa Chama na tayari Chama kimeelekeza mawakili kuanza maandalizi ya kuchukua hatua dhidi ya Jeshi la Polisi na Serikali kuwezesha Twaha Mwaipaya kuachiliwa huru au kupata dhamana na haki zake zingine kwa mujibu wa Katiba ya nchi na sheria zinazohusika.

Imetolewa leo Julai 03, 2022

Apolinary Boniface
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano - Bavicha
 
Naona Asali Haijawafikia BAVICHA ,Maana M/kiti ni kama haoni yanayoendelea kwenye Chama chake CHADEMA kwa sasa .
, 🙄😁😬 Sugar sukari kwenye saccos imeadimika sana. Lakini ndio wapate adabu na wajifunze kuwa chawa wa mwenyekiti mlamba asali kuna gharama.
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Nawashangaa polisi wanaacha kumkamata Mdude wanawakamata akina Mwaipaya wepesi kama nini.
 
Wasimtoe kwanza ili wamle mle ikibidi atoke na ujauzito kabisa ili akatulie nyumbani ,asikae kusumbua watu kwa makongamano uchwara
 
Vijana wanatafuta umaarufu kwa njia mbovu kabisa. Hata mwenyekiti wao Mbowe alishawaambia waheshimu sheria na polisi bado wanafanya siasa za 30 years ago. Hovyo kabisa.
Mtu akitenda kosa utaratibu uko wazi. Mbona hashtakiwi?
 
Sexless uko sahihi kabisa,lingekuwa ni jeshi la polisi lisingefanya huu ujinga .Lakini kwa kuwa ni jeshi la CCM ,ndiyo maana haya yanatokea.
 
Mbowe jitokeze kesho kukemea au kuvunja maridhiano. Huu upuuzi haukubaliki. Ukikaa kimya tutaamini umenunuliwa
 
Wasimtoe kwanza ili wamle mle ikibidi atoke na ujauzito kabisa ili akatulie nyumbani ,asikae kusumbua watu kwa makongamano uchwara
Vipi kile kiwanja cha Milioni Nne ulichokuwa unatafuta ununue ulishapata au bado unaishi Chumba cha Kupanga kilichojengwa na Mwanaume mwenzio??
 
Acheni kuwatetea vijana wakorofi kama Twaha Mwaipaya. Huyu muacheni akakabiliane na mashtaka yake

Alipoleta taharuki kwa watu kwamba Umeme umepanda bei na na kusambaza picture za kizushi kua Ng'ombe zimepigwa risasi na Police hamkuona kwamba ni kosa, Mbona hamkusema au lile mliona sawa kwenu,
Nyinyi huu upinzani wenu umekua wa kipuuzi Sana kwa kweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom