Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa wa CHADEMA Tanzania wameadhimia kwa kauli moja kuwa Chama kifanye maadhimisho makubwa ya kusajiliwa kwake. Viongozi hao waliokuwa Wilayani Karagwe Mkoani Kagera kwa ajili ya semina ya kuwajengea uwezo pamoja na Operesheni M4C katika Wilaya ya Karagwe na Bukoba walitoa maazimio hayo wakati wa majumuisho ya semina yao.
CHADEMA iliasajiliwa rasmi tarehe 19 July 1993 hivyo kutakuwa na mwezi au wiki ya CHADEMA ambapo Chama kitafanya shughuli mbalimbali za kijamii na za kujitolea ikiwa ni pamoja na mashindano ya kitaaluma kwa wanafunzi wa Sekondari na vyuo mbalimbali, usajili wa wanachama wa wapya, Makongamano n.k. Kilele cha sherehe hizo kitakuwa ni tarehe 19 July 2013.