CHADEMA kufanya Maadhimisho Makubwa ya miaka 20 ya kusajiliwa kwake

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa wa CHADEMA nchini wameazimia kufanyika kwa maadhimisho makubwa ya kuanzishwa kwa Chama chao. Wenyeviti hao waliokuwa kwenye semina ya kujengewa uwezo na kufanya Operesheni M4C Wilayani Karagwe Mkoani Kagera wameazimia hayo katika kikao chao cha kufunga na kufanya majumuisho ya semina yao.

Maadhimisho yatakuwa na shughuli mbalimbali ikiwamo mashindano ya wanafunzi kitaaluma, kurejesta wanachama wapya na shughuli nyingine mbalimbali. Kilele cha sherehe hizo kitakuwa tarehe 19 July 2012
 
Kilele tarehe 19 July 2012? Mnaadhimisha nini sasa! Nchi bado iko mikononi mwa hawa manyang'au. Bunge bado wanalo. Mabaraza ya madiwani mengi kabisa bado wanayo wao. Serikali nyingi za mitaa na vijiji ziko mikononi mwao.

Ninyi wenyewe CHADEMA ofisi za mikoa, wilaya, majimbo, kata hata matawi ziko hoi. Ni majina ya viongozi yanasikika hapa na pale.

Kama ni kujinadi na kujitangaza tu sawa.
 
Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa wa CHADEMA nchini wameazimia kufanyika kwa maadhimisho makubwa ya kuanzishwa kwa Chama chao. Wenyeviti hao waliokuwa kwenye semina ya kujengewa uwezo na kufanya Operesheni M4C Wilayani Karagwe Mkoani Kagera wameazimia hayo katika kikao chao cha kufunga na kufanya majumuisho ya semina yao.

Maadhimisho yatakuwa na shughuli mbalimbali ikiwamo mashindano ya wanafunzi kitaaluma, kurejesta wanachama wapya na shughuli nyingine mbalimbali. Kilele cha sherehe hizo kitakuwa tarehe 19 July 2012

[/
QUOTE] Ongeza umakini mleta uzi tarehe hiyo kwenye nyekundu kimantiki si sahihi
 
Mnafanya maadhimisho gani sasa...utasikia Chadema watumia milioni 200 kwenye maadhimisho yao Dr Slaa na Mbowe wafunika.
 
Hivi wana CCM mbona mna upeo mdogo sana? Au ndio mliokaririshwa DARUSO hizo pumba zenu? Mambo ya CHADEMA nyie mnaanza kutoa povu koz mnajua haya maadhimisho yatambatana sumu za makamanda.
 
Back
Top Bottom