CHADEMA kuendelea kutumia ibada kumuombea Mbowe, kudai Katiba Mpya

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,220
5,943

Chadema kuendelea kutumia ibada kumuombea Mbowe, kudai Katiba Mpya​


By Mgongo Kaitira


Mwanza. Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeendelea na mbinu yao mpya ya kudai Katiba Mpya kwa kwa njia ya amani kwa kutumia ibada zinazoendeshwa katika makanisa mbalimbali jijini Mwanza.

Chama hicho pia kinatumia ibada hizo kumuombea mwenyekiti wao taifa, Freeman Mbowe anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi kwa kula njama na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi.

Hiyo ni baada ya viongozi na wanachama wa chama hicho mkoa wa Mwanza kuhudhuria ibada na kufanya maombi katika Kanisa Katoliki Epiphania ya Bugando lililoko katikati ya jiji hilo.

Akizungumza na Mwananchi Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zakaria Obadi amesema mbinu hiyo imeonyesha ufanisi huku mwitikio kwa wanachama wa chama hicho kuhudhuria ibada hizo ukiongezeka.

"Leo idadi ya wanachama wa Chadema waliohudhuria maombi ya kumuombea Mwenyekiti wetu, Freeman Mbowe na kudai Katiba Mpya imeongezeka kuna waliovalia sare za chama na ambao hawakuvaa sare za chama," amesema Obadi.

Ameongeza kwamba chama hicho kitaendelea kudai Katiba Mpya katika maeneo yenye mikusanyiko na kwenye nyumba za ibada bila hofu huku wakiamini kwamba Mungu atafanya muujiza wake ili kufanikisha jambo hilo.

"Tunamuombea na Rais Samia Suluhu Hassan ili Mungu amshushie hekima ili aweze kuona ulazima wa kuwa na Katiba Mpya na tunaamini tutaipata," amesisitiza Obadi.

Obadi ameongeza; "Nitoe wito kwa wanachama wa Chadema Kanda ya Victoria kuondoa hofu, waje wajiunge nasi kumuombea mwenyekiti wetu na kudai Katiba Mpya kwa njia ya amani,"

Zaidi ya wanachama 50 waliokuwa wamevaa sare za Chadema na skafu wameonekana katika misa hiyo iliyohitimishwa saa 3:30 asubuhi ya leo.


Chanzo:
Mwananchi
 
Kwahiyo lifanyavyo lile genge la maharamia kwako poa sio.
wana mamlaka nayo yanatoka kwa Mungu- Yesu Mungu HAKUBISHANA na mamlaka pamoja na kuwa na uwezo huo- Sasa nyie nani?
 
wana mamlaka nayo yanatoka kwa Mungu- Yesu Mungu HAKUBISHANA na mamlaka pamoja na kuwa na uwezo huo- Sasa nyie nani?
Kwahiyo hiyo ndio imani yako,au unasema lililo kwenye imani usiyo iamini.
 
Ulitaka waende mlingotini kuloga? Washukuru Kwa kukimbilia kwenye nyumba za ibada kumwabudu Mungu na kuwaombea watesi wao kwa Mungu ili wabadilike na kuwa watu wema badala ya kukimbilia waganga kuwaloga!
 

Mara zote nimesema kuwa msingi wa kikatiba wa kutenganisha dini na dola uheshimiwe.

Nikaongeza kuwa dua bungeni, maombi mwanzoni mwa kazi za kiserikali, na kutumia misahafu kuapa serikalini ni kuvunja katiba.

Sasa naongeza la nne: kutumia dini kuombea matukio ya kisiasa na wanasiasa kinyume cha sheria ya vyama vya siasa.

All religions are double agents of good and evil depending on who is in their control.

Waziri simbachawene anapaswa kuchukua hatua leo kwa kufanya yafuatayo:

1 . Kumkumbusha bosi wake kuwa ni vigumu kulalamikia kibanzi Ktk Jicho la jirani wakati lako lina boriti

2 . Kumkumbusha spika vivyo hivyo

3 . Na kupiga marufuku makanisa kutumiwa kama majukwaa ya Chokochoko za kisiasa.
 

Ccm imeamua kujiweka kwenye vyombo vya dola, cdm imeamua kumkimbilia Mungu. Wakanye ccm waambie wanachofanya wanatengeneza tatizo. Wakubali tu kuwa ccm sio Chama cha kizazi hiki, muda wa wao wa kukaa madarakani kwa ridhaa ya wananchi umepita.
 
KKKT na RC ndio watatoa amri kwa SAMIA aandike katiba mpya?

Watoe mara mbili, dini zote zinajuwa kuwa serikali hii iko madarakani kwa wizi wa kura. Ni vile tu tuna utamaduni wa kutoongea ukweli unaoiudhi serikali hadharani.

Kwa sasa katiba mpya ikaandikwa penda msipende. Mko madarakani kwa wizi wa kura halafu mnazuia kupatikana katiba itakayoweka viongozi madarakani kwa ridhaa ya umma?
 
Nina
Mbona Mataga mwenzenu Gwajima anawahunilia nyumbu wake ndani ya kanisa lililoletwa na wazungu kuwaambia wasichanjwe chanjo ya wazungu na husemi isipokuwa umewaona Chadema tu?
 
Acheni unafiki- hamkubali Mungu kwenye corona- kwenye katiba mpya na kesi ya UGAIDI ndo mnamkumbuka?

Hatuna mungu Mjinga wa vile, huyo mungu wa kuonyeshwa na kiongozi muovu hatumtambui. Tunamjua Mungu wa kweli, na namna ya kumuendea. Yule mungu wenu wa propaganda bakini naye nyie ambao bongo zenu zilizokuwa offline.
 
Back
Top Bottom