Chadema kuchukua kata jimbo la Januari Makamba

Kwani Januari makamba anagombea udiwani?

Hata mkapa na Wasira HAWAKUGOMBEA arumeru kwa Nassari lakini aliyelaumiwa si SIOI bali ni Mkapa kwa kushindwa ku-deliver kuwafanya wapiga kura wapigie ccm, same for makamba iwapo ccm itakataliwa kwa kumpa kura mgombea wa cdm ilihali ni jimbo chini ya ccm, failures indicators ni matokeo ya mbunge dhaifu.Nadhani umeelewa sasa
 
Mkuu nilioona thread yako imebdi nimuombe jamaa mmoja ambaye alishiriki kumsaidia kijana J.Makamba kuzunguka kupata watu wa kumsapoti kupitishwa na chama.Ameniambia kuwa ulivyosema ni sahihi kabisa na yeye alikuwa huko Bumbuli jana ameona Cdadema wakifanya kazi yao lakini pia mwitikio wa watu ni mkubwa sana ikizingatiwa mambo ya kisiasa kwa eneo hilo ni kama ulikuwa chini sana japo wanamabadiliko ni wengi.
Kikubwa kabla ya kwenda kufanya uchaguzi ni vema mkajenga network ya uhakika na mawakala wasio na njaa na ambao they truly committed kupata mabadiliko.Wapeni elimu ya kuwajenga kiraia,kidemokrasia na kimabadiilko,wakumbusheni mateso wanayoyapata yanatokana na matumizi mabaya ya kura zao.
Jamaa hapa pia amenieleza kuwa maji ni tatizo japo vyanzo vipo huko huko bumbuli kama Mlalo- Bumbuli.Mkuu tunawatakia mpanmbano mema na mshikamane kweli kweli ili kuweza kuchukua kata hiyo.

Ukitazama jinsi kikundi cha uhamasishaji cha wakina-Mama wanavyojitoa kuhamasisha wananchi kuunga mkoa chama kwa kweli ni faraja kubwa sana kwa wana-CDM.

Chama kimejipanga vilivyo kukabiliana na hujuma yoyote ile...network ya uhakika ikiwepo mawakala, wahamasishaji nyumba kwa nyumba n.k. ipo vizuri sana, kata hii inahitajika zaidi ya maelezo..
 
Binafsi nawatakia kila kheri, kwani huo ni mustakabali wenu nyinyi wana Tamota, msikubali milungula mkauza kura zetu mtajiletea matatizo wenyewe. Cha msingi mnachotakiwa kufahamu ni kuwa viongozi ni sehemu ya jamii, tunawachagua kuwakilisha si kutuwekea fedha mifukoni mkiona watu wanawapeni fedha basi hawafai kwani si suruhu la matatizo ya vijana wetu mashuleni, akina mama wajawazito, huduma za kijamii pamoja na mengineyo mengi .
 
CCM si wajanja vile kama tunavyofikiria, silaha yao ni nguvu ya pesa na ubabe, hata ukiwaamsha hawawezi kuzuia upepo wa mabadiliko.

Uchaguzi wa diwani kata ile ni muhimu kuliko hata ubunge kwani ushindi kwa CDM pale utatoa multilpier effect kubwa sana. kama mtaweza kuweka ulinzi wa kura basi mtafanikiwa, lazima kulinda kura kwa nguvu zote kwa kufuata sheria na taratibu, hapo mtawaona ccm wataanza kuyeyuka kama barafu.Makamba hakuwahi kujipima kama anakubalika bumbuli au la kura za maoni ndani ya chama chake alinunua, uchaguzi wenyewe pia alimhonga mgombea wa opposition so hana base nzuri pale kisiasa ilas kimitandaoni yes ana base.kazi anayo
 
Ukitazama jinsi kikundi cha uhamasishaji cha wakina-Mama wanavyojitoa kuhamasisha wananchi kuunga mkoa chama kwa kweli ni faraja kubwa sana kwa wana-CDM.

Chama kimejipanga vilivyo kukabiliana na hujuma yoyote ile...network ya uhakika ikiwepo mawakala, wahamasishaji nyumba kwa nyumba n.k. ipo vizuri sana, kata hii inahitajika zaidi ya maelezo..
Mkuu Mbelwa nimefarijika sana na maelezo yako na hii inaonesha kuwa CDM kuingia kwenye damu za waTZ.Wakati tunaona mambo yanakwenda vizuri,tusipumzike kabisa maana inaweza kutokea watu kuona kazi imekwisha kumbe kazi bado sana mpaka matokeo yatakapo tangazwa.
Napenda kuendelea kuwatieni moyo wanamabadiliko popote walipo kuwa kazi ya kuchukua dola si kazi nyepesi kama tutaamini kuwa kuna watu ndo watatakiwa kuifanya na kutukabidhi mikononi hayo mabadiliko tuyatakayo basi tutakuwatunapotea na kujidanganya wenyewe,lazima wote tusimame imara kuhakikisha tunayapigania mabadiliko pasipo mapumziko,tupumzike pale tu ushindi uko mikononi na kuanzia hapo ni kuanza kuimplement tuliyoahidi.
Naamini kuwa kamanda upo mstari wa mbele ktk ujenzi huu makini wa chama na mazingira ya ushindi wa kuja kuchukua jimbo kabisa na baadae nchi mwaka 2015.Kazi njema kamanda na makamanda wengine mliopo huko Tanga-Lushoto-Bumbuli-Tamota.
 
Nimefika mara kadhaa wilayani Lushoto baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 hasa katika hivyo vyuo ulivyovitaja vya IJA na SEKUCo, kwa uhakika hamasa ya mageuzi ni kubwa sana, nilikuwa najiuliza kama hali ndio ile ilikuwaje tukashindwa kuyachukua majimbo ya Lushoto na Mlalo?

Naamini kwamba muamko wa wananchi wa wilaya ya Lushoto wa kutaka mageuzi ni mkubwa sana na hivyo ni wajibu wa viongozi wenyewe wa vyama hasa Chadema wilaya ya Lushoto na mkoa wa Tanga kwa ujumla kujipanga vizuri zaidi ili kuhakikisha kwamba wananchi wa mkoa wa Tanga wanapata matumaini mapya ya maendeleo yao.
 
Well said, 6 days to go. The biggest challenge inhere ni njaa za mawakala na hujuma ya magamba.!
 
good aluta continue naamini hata lile jimbo la mlalo 2015 CDM tutalitetea ili kufufua fikra za kimaendeleo ya wananchi zilizofifia na kufa kabisa kuanzia mwaka 1961:msela:
 
Well said, 6 days to go. The biggest challenge inhere ni njaa za mawakala na hujuma ya magamba.!

Tumejipanga vilivyo, mawakala watafanyiwa training kabambe chini ya uangalizi imara wa chama na tumejipanga kwa hujuma zozote za CCM.
 
... he deserve to be called Media Boy kwasababu hakubaliliki kwa namna ambavyo watu wengi wanaweza kufikiri zaidi ya kujenga jimbo kwenye magazeti na mitandao ya kijamii. Ukweli ni kwamba ni mwepesi mno silaha kubwa anayotumia ni nguvu ya fedha basi

Tuwe tunapongeza panapostahili na kutoa heko ili tusiwavunje moyo watu wetu. Kukosa kufanya hivyo ni kutengeneza maana na msamiati mpya kwa matendo mema kuonekana ndiyo mabaya, utajiri kuonekana ni laana, na umaskini ndiyo heri. Siasa si chuki na upinzani siyo kupinga kila kitu. January Makamba (JM) ukimuita Media Boy, Naibu Katibu Mkuu-CDM-ZZK utampa jina gani? Hata kama ...bado JM kuvaa uhusia kamili wa Wizara yake ni LAZIMA awe mtu wa kutokelezea na kutumia vema Media hasa hizi za kileo. Anayemshangaa JM kuwa front katika kutumia Media hasa Social-Media basi asishangae pale serikali inapochagua Mkurugenzi wa ICT asiyejua kutumia walau typewriter!

Kwa mtazamo wangu JM anafanya mambo yanayogusa Wananchi na yanayohitajika pahala husika. Hebu angalia mradi kama wa Ujenzi wa Kiwanda cha Kusindika Matunda; hiki ni kilio kwa mikoa yote inayozalisha matunda kwa wingi. Matunda mengi yanaozea vijijini-hakuna majokofu wala viwanda, soko linakuwa la msimu na bei inakuwa ndogo kipindi cha msimu, msimu wa mavuno ukiisha bei inakuwa nzuri lakini matunda hayapo! Sasa mtu anayekuhamasisha na kuwaongoza mkajenga Kiwanda unaweza kumuita Media Boy? Wangapi wamepata kukalia kiti hiki na kuondoka bila kuacha chochote cha maana?

Yawezekana ni kweli hapendwi si Bumbuli tu, bali Tanzania nzima. Lakini hilo haliondoi ukweli kwamba JM kwenye suala la Maendeleo ya Bumbuli anafanya mambo ya msingi sana. Maradhi yanayotutafuna Watanzania wengi ni kufanya machaguo marahisi mfano kukosoa, kulaumu, kukejeri, ila tukiulizwa pendekezo la mbadala wa tunachokosoa wengi tunajiumauma--HATUNA!
 
Attachments

  • jm.jpg
    jm.jpg
    70.3 KB · Views: 34
  • JMA.jpg
    JMA.jpg
    114.2 KB · Views: 35
Tumejipanga vilivyo, mawakala watafanyiwa training kabambe chini ya uangalizi imara wa chama na tumejipanga kwa hujuma zozote za CCM.
Imetulia sana, maana panga pangua mtaji wa ccm uliobaki si wapiga kura bali ni wizi, hujuma na ufisadi wa chaguzi
 
Jimbo la kigoma kaskazini linaongozwa na zitto kabwe chadema miaka 15 leo lakini madiwani walio wengi ni wa ccm na halmashauri iko chini ya ccm.huo ni mfano mmoja katika mingi kwa hiyo hiyo kata moja huko mumbuli ikienda cdm sio kipimo halisi
 
Imetulia sana, maana panga pangua mtaji wa ccm uliobaki si wapiga kura bali ni wizi, hujuma na ufisadi wa chaguzi

fundisho kuu ilikuwa ni umeya wa jiji la mwanza.endeleeni kuamini katika hayo wenzenu wanarudisha maeneo yao ya utawala
 
Tuwe tunapongeza panapostahili na kutoa heko ili tusiwavunje moyo watu wetu. Kukosa kufanya hivyo ni kutengeneza maana na msamiati mpya kwa matendo mema kuonekana ndiyo mabaya, utajiri kuonekana ni laana, na umaskini ndiyo heri. Siasa si chuki na upinzani siyo kupinga kila kitu. January Makamba (JM) ukimuita Media Boy, Naibu Katibu Mkuu-CDM-ZZK utampa jina gani? Hata kama ...bado JM kuvaa uhusia kamili wa Wizara yake ni LAZIMA awe mtu wa kutokelezea na kutumia vema Media hasa hizi za kileo. Anayemshangaa JM kuwa front katika kutumia Media hasa Social-Media basi asishangae pale serikali inapochagua Mkurugenzi wa ICT asiyejua kutumia walau typewriter!

Kwa mtazamo wangu JM anafanya mambo yanayogusa Wananchi na yanayohitajika pahala husika. Hebu angalia mradi kama wa Ujenzi wa Kiwanda cha Kusindika Matunda; hiki ni kilio kwa mikoa yote inayozalisha matunda kwa wingi. Matunda mengi yanaozea vijijini-hakuna majokofu wala viwanda, soko linakuwa la msimu na bei inakuwa ndogo kipindi cha msimu, msimu wa mavuno ukiisha bei inakuwa nzuri lakini matunda hayapo! Sasa mtu anayekuhamasisha na kuwaongoza mkajenga Kiwanda unaweza kumuita Media Boy? Wangapi wamepata kukalia kiti hiki na kuondoka bila kuacha chochote cha maana?

Yawezekana ni kweli hapendwi si Bumbuli tu, bali Tanzania nzima. Lakini hilo haliondoi ukweli kwamba JM kwenye suala la Maendeleo ya Bumbuli anafanya mambo ya msingi sana. Maradhi yanayotutafuna Watanzania wengi ni kufanya machaguo marahisi mfano kukosoa, kulaumu, kukejeri, ila tukiulizwa pendekezo la mbadala wa tunachokosoa wengi tunajiumauma--HATUNA!

  1. Makamba hakuwahi kujipima kama anakubalika Bumbuli
  2. Kura za maoni ndani ya chama chake alipita kwa mizengwe
  3. Pia alitumia uwezo wa fedha kuhujumu mgombea wa CDM n.k.

Makamba hana msingi(base) nzuri kisiasa zaidi ya kubebwa na jina la Baba yake, unaweza kupiga picha majengo ya Bakhressa na ukasema yako bumbuli, njia nzuri ya kutambua ukweli ni kutafuta ukweli.

Simshangai Makamba kutumia Media bali namshangaa kwa kuwaaminisha watu kuishi kwa hisia bila kutafuta uhalisia. Nenda kata ya Tamota halafu angalia miundombinu ya barabara, huduma za maji n.k. halafu linganisha na sentensi zake kwenye social media. Makamba hakuchaguliwa kwa ridhaa ya wananchi wa Bumbuli bali na kikundi cha wana-CCM.
 
Tumejipanga vilivyo, mawakala watafanyiwa training kabambe chini ya uangalizi imara wa chama na tumejipanga kwa hujuma zozote za CCM.
Kila la heri manake hao mumiani wa CCm hawachelewi kuiba na kuhonga watu ,please wishing you all the best
 
Back
Top Bottom