Chadema kuchukua jukumu la kuwalipa mawakala wake posho ya kujikimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kuchukua jukumu la kuwalipa mawakala wake posho ya kujikimu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lu-ma-ga, Oct 8, 2010.

 1. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Taarifa zilizotolewa jana na mkurugenzi wa Nec kuwa vituo vya kupigia kura viko 51732 nchi nzima.
  Changamoto kwa chadema ni kuwa;Ni vema ikafanya utaratibu wa kuwalipa mawakala wake japo kwa kiwango cha shs.20,000 kwa siku YA UPIGAJI KURA ili kuwapa uhakika wa kifuta jasho ktk zoezi la usimamizi na pia kupunguza vishawishi.

  Kwa mfano kama chadema wakiamua kuweka wakala katika vituo nagalau 85% ya vituo vyote ina maana wataweka mawakala 43,972 nchi nzima.Mawakala hawa wakilipwa shs.20,000 gharama itakuwa: vituo 43,972* shs.20,000= shs 879,440,000

  Kwa kufanya hivyo tutapunguza ushawishi wa kupenyezwa kwa pesa haramu na pia kwa kuwa tutakuwa tumeweka mawakala loyal kwa chama tuna uhakika wa kulinda kura zetu.Tukumbuke kulinda kura ni gharama na gharama ndiyo hizo

  Mnasemaje? Basi wanaJF tuanzia hapa kujadili.KARIBUNI..........
   
 2. d

  dotto JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ..... changia CHADEMA..... changia ushindi. Mawakala wa Chadema kuwezi na uzalendo. Pesa za mafisadi kataeni.
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Naona inabidi mawakala wawekwe vituo vyooote!! Na kiwango kiwe Ths 50,000 * 51,7320. This is affordable.
   
 4. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hili la kuweka mawakala ni la Munhimu kabisa....kwani Chadema wasipo fanya hivyo ni "Sawa na Mwanafunzi ambaye amefanya mtihai wake vizuri lakini hakukusanya karatasi yake ya majibu then aanze kulalamika kua kwa nini hakufaulu". Hili la kuwalipa mawakala linawezekana ikianzia kwetu. Jamani tuchangie Chadema. Njia zote za kuchangia tunazijua.
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  CHADEMA wasithubutu kuegema kigezo cha watu wako tayari kwa mageuzi hii haitoshi ni vema chama kianze sasa kuweka mikakati ya kupata fedha.Tayari tumeanza kuchangia mimi tayari.Kama watawweka wakala vutuo vyote , gharama itakuwa: 51732*shs 20,000=shs.1,034,640,000.Hizi pesa walipwe kabla ya kwenda kituoni.
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,076
  Trophy Points: 280
  Wazo ni jema kama Chadema wako serious na huu uchaguzi waweke mawakala nchi nzima kwenye vituo vyote na kuwalipa kiwango hicho cha Tshs 20, 000/= kwa hiyo siku moja na jumla yake itakuwa ni Tshs 1, 040, 000, 000/=. Jumla ya vituo ni zaidi ya 52, 000. Bila ya hilo tusije tukalaumiana kuwa CCM wamechakachua. Demokrasia makini yahitaji kujito mhanga vinginevyo tutabaki kuota ndoto ya ingelikuwaje.

  Vile vile kuhakiki mawakala wasije pakashume wa CCM wakajipenyeza humo.
   
 7. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tunaomba harambee ya Chadema ifanyika wiki ijayo katika miji yote mikubwa Tanzania. Kuwe na siku maalumu ya Changia Chadema ishinde, inaweza kuambatana na siku ya Nyerere (14.10.2010).
   
 8. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Hilo linawezekana kama wapenda maendeleo Laki 3 kila mmoja atatuma sms10@350 tutapata zaidi ya 1.05bilion zinazohitajika kuwalipa mawakala 5200 kila mmoja 20000. shime wanachadema 3500 tu kwa kila mpenda TZ MPYA YENYE NEEMA.
   
 9. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Ni vizuri chadema basi watoe maagizo kwa wagombea ubunge na udiwani kuhamasisha wapiga kura kutuma sms badala ya kukusanya cash.Majimbo yapo 187 ambako chadema wameweka wagombea WATUMe SMS za kutosha.
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wazao zuri sana...

  labda nikuhabarishe tu kwamba 20,000 kama ndio kiwango wanachofikiria chadema basi watalia sana baada ya uchaguzi... kiwango hicho hata kwenye primaries za CCM tu kilisaidia watu kuuza haki za wana ccm wenzao

  Just wait and see, siku hiyo mawakala watalipwa kuanzia 50,000 had laki tano kutegemea na jimbo ili tu auze kura

  watch this space
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  WATU na MAZINGIRA.
  Mimi ningependekeza sana swala la kuwalipa mawakala wa usimamizi wa kura toka vyama kuwa ni swala la Kitaifa yaani mawakala wote wanalipwa posho sawa toka mfuko wa serikali kuliko mamlaka ya vyama, kwani hali yetu bado kabisa haijaturuhusu kuacha mamlaka hayo kwa vyama vyenyewe..

  Lakini maadam tumefika ukingoni na hakuna uuwezekano huo basi kweli inabidi Chadema wabebe mzigo huu mkubwa pasipo dharau hata kidogo. Kila sehemu waliyokwenda ilibidi wakamilishe uchaguzi wa wasimamizi na kuwahakikishia posho hata kama wamejitolea...

  Dr.Slaa na kampeni zake zote hazitakuwa na umuhimu wowote ikiwa kipengele hiki kimeachwa pasipo kujiandaa vizuri na mapema.
   
 12. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Nafikiri kwenye red una maanisha kuweni na si kuwezi.
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sometimes kujitolea kwa ajili ya maslai ya umma ni suala ambalo tuwe twalifikilia
   
 14. M

  Mundu JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Watanzania wanaotaka mabadiliko hawanunuliki kirahisi. na kumbukeni kuwa pesa si kila kitu. Kama mtu anataka kununuliwa, atanunuliwa tu hata umpe kiasi gani.

  Mbona CCM hawajajunua mawakala wa Chadema kule Karatu? Kinachotakiwa hapa ni UZALENDO tu na kupenda mabadiliko. Pesa ya kujikimu kwa mawakala ni sawa! lakini hatuna kipimo cha pesa zinazomtosha mtu ili asinunuliwe.
   
 15. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kuna majimbo ambayo ni strategic kabisa, mi naona sehemu za namna hiyo kuwekwe lindo la ziada...Kuna majimbo kama Ubungo, ambako unaweza usihitaji hata hiyo 20,000, lakini cha muhimu ni uwepo wa watu ambao ni determined, na wako enthuastic kutetea maslahi ya chama!.
  Wakuu wetu wanahitaji kukaa chini na kuchambua umuhimu wa majimbo, na wagombea, na hatimaye kuamua aina ya msaada(fedha au manpower) ya kuweka mahala husika!
   
 16. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Mundu umelonga sahihi,kwa sasa tunaaamini uzalendo kwa sasa uko juu kwa watanzania wengi hasa baada ya kugundua kuwa kumbe nchi hujengwa na wenye nchi. Lakini tunajaribu pia kuweka kiwango japo kidogo kuwafanya kwa siku hiyo wawe liquid financially, Unajua hapa tunajaribu kuzingatia ubinadamu kwa mtu aliyekubebea mzigo wako akafikisha salama ni utamaduni kukarimiana au asante.Kutokana na unyeti wa swala ndiyo maana inabidi wapewa kabla ya kazi
   
 17. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Mimi pia napendekeza wapewe performance bonus baada ya uchaguzi. Na hiyo performance nzuri ya kulinda matokeo ni Chadema kushinda hasa kwenye majimbo na kata ambazo wana uhakika nazo. Kwa ngazi ya Urais Dr. Slaa kushinda au kushindwa kwa margin ndogo sana!

  Tuchangie Chadema ili wafanikishe hili la kuwalipa mawakala allowance ya siku na bonus!
   
 18. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Ni wazo zuri sana, naliunga mkono

  napendekeza siku ya nyerere day chadema wafanye harambee kubwa kabisa tanzania nzima

  @ 500 tutapata hella nyingi sana fikiria watu angalau 3 milioni wakijitokeza..

  Tuiunge mkono chadema kwa mabadiliko ya nchi yetu tanzania
   
Loading...