Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Salaam ndugu zangu,
Naomba mtu asichangie kama hajasoma.
Mnaokumbuka, toka awali nilisema nitakuwa nikitoa ushauri tu kwa CHADEMA na sina nia ya kugombea nafasi yeyote.Hata hivyo mara zote nikishauri kitu tu nimekuwa nikishambuliwa kwamba nimetumwa.Sasa leo nawaletea Plan "A" na plan "B" na nijukumu la kila mtu kufikiri na kuchagua mwenyewe.
Kwenye taasisi ya kisiasa ni lazma kwanza ijengwe na nadharia za kifalsafa juu ya muelekeo wa kifikra wa ndani (internal philosophical paspective) halafu ndio ichague falsafa za nje (sera, mikakati dhidi ya vyama vingine n.k).
Jaribu kupitia Mitizamo ya aina ya siasa za Ndani ambayo CHADEMA inaweza kuchagua na kujijenga katika mtizamo mmoja ikijua wazi ni nini kinachotarajiwa mbeleni.
PLAN "A "
===================================================
PLAN "B" INAFUATA HAPO CHINI
Naomba mtu asichangie kama hajasoma.
Mnaokumbuka, toka awali nilisema nitakuwa nikitoa ushauri tu kwa CHADEMA na sina nia ya kugombea nafasi yeyote.Hata hivyo mara zote nikishauri kitu tu nimekuwa nikishambuliwa kwamba nimetumwa.Sasa leo nawaletea Plan "A" na plan "B" na nijukumu la kila mtu kufikiri na kuchagua mwenyewe.
Kwenye taasisi ya kisiasa ni lazma kwanza ijengwe na nadharia za kifalsafa juu ya muelekeo wa kifikra wa ndani (internal philosophical paspective) halafu ndio ichague falsafa za nje (sera, mikakati dhidi ya vyama vingine n.k).
Jaribu kupitia Mitizamo ya aina ya siasa za Ndani ambayo CHADEMA inaweza kuchagua na kujijenga katika mtizamo mmoja ikijua wazi ni nini kinachotarajiwa mbeleni.
PLAN "A "
MTIZAMO WA VIONGOZI WA JUU WA CHAMA | ||
MTIZAMO | FAIDA | CHANGAMOTO |
Kuhodhi fikra na kujenga utiifu wa woga kwa viongozi wa chini na wafuasi kwa kuwashughulikia wenye fikra tofauti | Kujenga chama chenye utiifu wa hali ya juu kwa viongozi wa kuu,utiifu unaowafanya wasihoji wala kuchunguza jambo na hivyo kuleta utulivu wa kifikra kwa Viongozi. | Wanachama/viongozi wa kati na chini , kuwa na dhamira mbili zinazopingana. (a)dhamira ya nje inayolenga kuonesha utiifu wa hali ya juu kwa kuyakubali yote yanayosemwa na wakubwa 100% (b) dhamira ya ndani inayosukumwa na mawazo na imani binafsi ya muhusika. -Kwa ujumla kuishi katika mazingira ya unafiki. |
AINA YA VIONGOZI WA NGAZI YA KATI | ||
MTIZAMO | FAIDA | CHANGAMOTO |
Wenye elimu ya kati au ndogo, wasio sukumwa na fikra huru, wasio wabunifu, wasioweza/penda kutafiti mambo na wanaofanya kile wanachoelekezwa tu. | Hawatahoji mapato wala matumizi,hawataanzisha ajenda, wala hawatalalamikia jambo hadharani.Hii itasaidia kuwapunguzia viongozi wakuu msongo wa mambo na kujikita katika kukabiliana na wapinzani wa nje tu. -Itaepusha hali ya kudhaniana kwamba wahusika wametumwa na CCM n.k | -Itachochea ukiritimba wa fikra ndani ya taasisi kutoka miongoni mwa watu wachache -kudumaa kwa fikra miongoni mwa wadau na watendaji -kudumaa kwa ukuaji wa taasisi kwa ndani. -wadau kukaa na duku duku moyoni -Kuibuka kwa migogoro mizito mizito |
AINA YA WASHAURI WA CHAMA | ||
-Wasiwe wataalam/wasomi waliobobea kwenye fani husika -wasioheshimu ukweli "Facts" na wanaosema kile ambacho kinaweza kufurahisha viongozi tu | -Watakuwa wakiwafariji viongozi hasa wakati wa misuko suko inayotokana na upinzani wa nje -Watakuwa wakiwatia moyo viongozi na hivyo kupata ari zaidi. | -Daima hawatasema ukweli -daima hawatatumia taaluma na uzoefu wao -Watawalewesha sifa viongozi wa chama -Wataua Chama. |
MBINU ZA UENEZI WA CHAMA | ||
Utumiaji wa Propaganda safi na chafu kama mbinu kuu ya uenezi | Watapatikana waungaji mkono na washabiki wengi hasa vijana wa kiume. | -chama kitapoteza uungwaji mkono kutoka kwa wasomi walio wengi. -Chama kitapoteza uungwaji mkono kutoka kwa watu wanaofikiri na kuchambua mambo. -chama kitapoteza uungwaji mkono kutoka kwa watu wanaopenda siasa za kistaarabu. -watakaokiunga mkono chama, wanaweza kubadili fikra masaa24, kabla ya uchaguzi kwa kuwa hawana msingi imara wa kusimamia zaidi ya emotions. |
UHUSIANO KATI YA CHAMA NA TAASISI NYINGINE | ||
Kujenga uadui na uhasama na taasisi nyengine nje ya chama chenyewe. | Taasisi nyengine zitakiogopa chama na hivyo ni vigumu kuingilia shughuli za chama | -Taasisi nyingine zitaogopa kushirikiana na chama kwa kuhofia kutuhumiwa -Hazitatoa ushirikiano mwema wakati wa uchaguzi (kwa roho safi) -Chama kikishika dola kitashindwa kuiongoza serikali. |
UFUAJI WA VIJANA NDANI YA CHAMA | ||
Kuandaa vijana watiifu na wanaowashabikia viongozi wao kwa 100% | Viongozi wa chama watapata hamasa kubwa kufanya kazi wakiwa wana matumaini makubwa | Kutakuwa na kundi kubwa la viongozi/vijana ndani ya chama wasio na uelewa wowote katika uongozi; vijana wasio na fikra pembuzi. |
AINA YA AJIRA YA WATUMISHI NDANI YA CHAMA | ||
Ajira za muda mfupi na kujitolea | Fedha kidogo tu itatumika | -Ni rahisi watumishi hao kubadilika badilika kutokana na kutokuwa na uhakika wa maisha yao. -ni rahisi watu hao kurubuniwa na kufanya kazi binafsi. |
RASILIMALI NA UCHUMI/UTUMIAJI WA FEDHA. | ||
Kuwekeza katika operesheni fupi fupi zinazokatika.Mf.Kulipia mkutano hotelini, kukodi vifaa n.k | -Haina haja ya kutumia akili nyingi katika utekelezaji. -inafaa sana kama wahusika hawana uhakika juu ya kesho yao | Kutumia fedha nyingi bila mipango endelevu na kusababisha uwepesiwa taasisi "org fragility" |
===================================================
PLAN "B" INAFUATA HAPO CHINI