CHADEMA Kuchagua Siasa: Plan "A" Vs Plan "B". (Hakikisha unapitia kwa makini.)

Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,915
Likes
2,483
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,915 2,483 280
Salaam ndugu zangu,

Naomba mtu asichangie kama hajasoma.
Mnaokumbuka, toka awali nilisema nitakuwa nikitoa ushauri tu kwa CHADEMA na sina nia ya kugombea nafasi yeyote.Hata hivyo mara zote nikishauri kitu tu nimekuwa nikishambuliwa kwamba nimetumwa.Sasa leo nawaletea Plan "A" na plan "B" na nijukumu la kila mtu kufikiri na kuchagua mwenyewe.

Kwenye taasisi ya kisiasa ni lazma kwanza ijengwe na nadharia za kifalsafa juu ya muelekeo wa kifikra wa ndani (internal philosophical paspective) halafu ndio ichague falsafa za nje (sera, mikakati dhidi ya vyama vingine n.k).

Jaribu kupitia Mitizamo ya aina ya siasa za Ndani ambayo CHADEMA inaweza kuchagua na kujijenga katika mtizamo mmoja ikijua wazi ni nini kinachotarajiwa mbeleni.

PLAN "A "
[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD="colspan: 3"]
MTIZAMO WA VIONGOZI WA JUU WA CHAMA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]MTIZAMO

[/TD]
[TD="width: 213"]FAIDA
[/TD]
[TD="width: 213"]CHANGAMOTO

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]Kuhodhi fikra na kujenga utiifu wa woga kwa viongozi wa chini na wafuasi kwa kuwashughulikia wenye fikra tofauti

[/TD]
[TD="width: 213"]Kujenga chama chenye utiifu wa hali ya juu kwa viongozi wa kuu,utiifu unaowafanya wasihoji wala kuchunguza jambo na hivyo kuleta utulivu wa kifikra kwa Viongozi.[/TD]
[TD="width: 213"]Wanachama/viongozi wa kati na chini , kuwa na dhamira mbili zinazopingana.
(a)dhamira ya nje inayolenga kuonesha utiifu wa hali ya juu kwa kuyakubali yote yanayosemwa na wakubwa 100%
(b) dhamira ya ndani inayosukumwa na mawazo na imani binafsi ya muhusika.
-Kwa ujumla kuishi katika mazingira ya unafiki.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
AINA YA VIONGOZI WA NGAZI YA KATI
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]MTIZAMO

[/TD]
[TD="width: 213"]FAIDA [/TD]
[TD="width: 213"]CHANGAMOTO[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]Wenye elimu ya kati au ndogo, wasio sukumwa na fikra huru, wasio wabunifu, wasioweza/penda kutafiti mambo na wanaofanya kile wanachoelekezwa tu.[/TD]
[TD="width: 213"]Hawatahoji mapato wala matumizi,hawataanzisha ajenda, wala hawatalalamikia jambo hadharani.Hii itasaidia kuwapunguzia viongozi wakuu msongo wa mambo na kujikita katika kukabiliana na wapinzani wa nje tu.

-Itaepusha hali ya kudhaniana kwamba wahusika wametumwa na CCM n.k[/TD]
[TD="width: 213"]-Itachochea ukiritimba wa fikra ndani ya taasisi kutoka miongoni mwa watu wachache
-kudumaa kwa fikra miongoni mwa wadau na watendaji
-kudumaa kwa ukuaji wa taasisi kwa ndani.
-wadau kukaa na duku duku moyoni
-Kuibuka kwa migogoro mizito mizito[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
AINA YA WASHAURI WA CHAMA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]-Wasiwe wataalam/wasomi waliobobea kwenye fani husika -wasioheshimu ukweli "Facts" na wanaosema kile ambacho kinaweza kufurahisha viongozi tu[/TD]
[TD="width: 213"]-Watakuwa wakiwafariji viongozi hasa wakati wa misuko suko inayotokana na upinzani wa nje

-Watakuwa wakiwatia moyo viongozi na hivyo kupata ari zaidi.[/TD]
[TD="width: 213"]-Daima hawatasema ukweli
-daima hawatatumia taaluma na uzoefu wao
-Watawalewesha sifa viongozi wa chama
-Wataua Chama.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
MBINU ZA UENEZI WA CHAMA

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]Utumiaji wa Propaganda safi na chafu kama mbinu kuu ya uenezi[/TD]
[TD="width: 213"]Watapatikana waungaji mkono na washabiki wengi hasa vijana wa kiume.[/TD]
[TD="width: 213"]-chama kitapoteza uungwaji mkono kutoka kwa wasomi walio wengi.
-Chama kitapoteza uungwaji mkono kutoka kwa watu wanaofikiri na kuchambua mambo.
-chama kitapoteza uungwaji mkono kutoka kwa watu wanaopenda siasa za kistaarabu.
-watakaokiunga mkono chama, wanaweza kubadili fikra masaa24, kabla ya uchaguzi kwa kuwa hawana msingi imara wa kusimamia zaidi ya emotions.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
UHUSIANO KATI YA CHAMA NA TAASISI NYINGINE
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]Kujenga uadui na uhasama na taasisi nyengine nje ya chama chenyewe.[/TD]
[TD="width: 213"]Taasisi nyengine zitakiogopa chama na hivyo ni vigumu kuingilia shughuli za chama
[/TD]
[TD="width: 213"]-Taasisi nyingine zitaogopa kushirikiana na chama kwa kuhofia kutuhumiwa
-Hazitatoa ushirikiano mwema wakati wa uchaguzi (kwa roho safi)
-Chama kikishika dola kitashindwa kuiongoza serikali.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
UFUAJI WA VIJANA NDANI YA CHAMA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]Kuandaa vijana watiifu na wanaowashabikia viongozi wao kwa 100%[/TD]
[TD="width: 213"]Viongozi wa chama watapata hamasa kubwa kufanya kazi wakiwa wana matumaini makubwa
[/TD]
[TD="width: 213"]Kutakuwa na kundi kubwa la viongozi/vijana ndani ya chama wasio na uelewa wowote katika uongozi; vijana wasio na fikra pembuzi.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
AINA YA AJIRA YA WATUMISHI NDANI YA CHAMA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]Ajira za muda mfupi na kujitolea
[/TD]
[TD="width: 213"]Fedha kidogo tu itatumika
[/TD]
[TD="width: 213"]-Ni rahisi watumishi hao kubadilika badilika kutokana na kutokuwa na uhakika wa maisha yao.
-ni rahisi watu hao kurubuniwa na kufanya kazi binafsi.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
RASILIMALI NA UCHUMI/UTUMIAJI WA FEDHA.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]Kuwekeza katika operesheni fupi fupi zinazokatika.Mf.Kulipia mkutano hotelini, kukodi vifaa n.k[/TD]
[TD="width: 213"]-Haina haja ya kutumia akili nyingi katika utekelezaji.

-inafaa sana kama wahusika hawana uhakika juu ya kesho yao[/TD]
[TD="width: 213"]Kutumia fedha nyingi bila mipango endelevu na kusababisha uwepesiwa taasisi "org fragility"[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

===================================================
PLAN "B" INAFUATA HAPO CHINI
 
Crashwise

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Messages
22,181
Likes
897
Points
280
Crashwise

Crashwise

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2007
22,181 897 280
Ngoja kwanza nimsikilize Mbowe hapa Mwanza nitakuja kukusoma....
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,915
Likes
2,483
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,915 2,483 280

PLAN "B"

[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
MTIZAMO WA VIONGOZI WA JUU WA CHAMA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]
MTIZAMO​
[/TD]
[TD="width: 213"]
FAIDA​
[/TD]
[TD="width: 213"]
CHANGAMOTO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]
Kuruhusu uhuru wa hali ya juu wa mawazo lakini kuheshimu kanuni vile vile

[/TD]
[TD="width: 213"]
Kujenga chama chenye domokrasia ya kweli kweli na yenye nguvu
[/TD]
[TD="width: 213"]
Kuibuka kwa minyukano ya kifikra ya ndani kwa ndani (ambayo inaweza kusababisha wenye hoja dhaifu kuchukia)
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
AINA YA VIONGOZI WA NGAZI YA KATI
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]
MTIZAMO

[/TD]
[TD="width: 213"]
FAIDA
[/TD]
[TD="width: 213"]
CHANGAMOTO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]
Wenye elimu kubwa ,wabunifu na wanaohoji na kufikiri kisomi hasa.

[/TD]
[TD="width: 213"]
Watahoji,kukosoa na kushauri kila inapobidi na watafanya hivyo kwa kutumia hekima "Professional ethics"
[/TD]
[TD="width: 213"]
Wakati mwingine Wanaweza kuonekana ni watovu wa nidhamu, wametumwa kupinga,ni wachokonozi, ni wanoko n.k

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
AINA YA WASHAURI WA CHAMA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]
Wenye weledi wa kutosha, fikra pevu,watafiti na wanaosema kweli daima

[/TD]
[TD="width: 213"]
Watakuwa wanaongea na kushauri vitu halisia "Facts" ,KITU AMBACHO NI CHA MUHIMU SANA KATIKA KARNE HII YA 21.
[/TD]
[TD="width: 213"]
Wanaweza kuonekana kwamba ni kikwazo hasa pale watakapofikiri na kupendekeza jambo ambalo litagusa masilahi ya mtu binafsi.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
MBINU ZA UENEZI WA CHAMA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]
Utumiaji wa hoja nzito,tafiti maridhawa, vielelezo thabiti na ushawishi wa busara pamoja na propaganda safi.

[/TD]
[TD="width: 213"]
-Kupata uungwaji mkono kutoka kwa wasomi, watu wanaopenda siasa za kistaarabu, wenye fikra pevu pamoja na watu wa kawaida.
-kupata wafuasi wa kudumu waliojikita katika misingi imara inayoeleweka.
[/TD]
[TD="width: 213"]
Ili kutumia mbinu hii kwa ufanisi, inahitaji muda wa kutosha , watu wenye uwezo mkubwa na nia njema.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
UHUSIANO KATI YA CHAMA NA TAASISI NYINGINE
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]
Kujenga uhusiano mwema na vyama/taasisi nyingine

[/TD]
[TD="width: 213"]
Kupata ushirikiano na uungwaji mkono kutoka taasisi/vyama vingine na hata kuweza kupata ushirikiano kama chama kikishika dola na hivyo kuweza kuunda serikali.
[/TD]
[TD="width: 213"]
Uwepo wa watu wenye chuki na watu wa taasisi nyengine zote isipokuwa chama chao tu.
.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
UFUAJI WA VIJANA NDANI YA CHAMA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]
Kuandaa vijana wapembuzi,wadadisi,watundu lakini waadilifu na wenye hekima

[/TD]
[TD="width: 213"]
Kuandaa viongozi wanaoweza kumudu mikikimiki ya kiuongozi katika karne ya 21.
[/TD]
[TD="width: 213"]
-Uwepo wa vijana wanaopenda ushabiki zaidi ya kitu kingine chochote
-Uwepo wa wanasiasa wanaopenda kuwatumia vijana kwa maslahi yao binafsi
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
AINA YA AJIRA YA WATUMISHI NDANI YA CHAMA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]
Ajira za kudumu

[/TD]
[TD="width: 213"]
Watumishi watakuwa na utulivu wa nafsi na hivyo kufanya kazi kwa moyo mmoja
[/TD]
[TD="width: 213"]
-Gharama kubwa itatumika kulipa mishahara.
-Kama kuna kiongozi angependa kuwatumia na ikishindikana kuwatimua atakuwa ni kikwazo.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 638, colspan: 3"]
RASILIMALI NA UCHUMI/UTUMIAJI WA FEDHA.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 213"]
Kufanya operesheni na mikakati ya muda mtefu.Mf.Kujenga ukumbi wa mikutano badala ya kufanyia mikutano hotelini.

[/TD]
[TD="width: 213"]
Kutakuwa na utunzaji fedha,kuweka vitega uchumi na kutabiri hatma ya wakati ujao
[/TD]
[TD="width: 213"]
Inahitaji uamuzi mgumu na malengo ya mbali .
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,134
Likes
80
Points
145
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,134 80 145
Umewahi kusoma Cybernetic model of leadership?
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,915
Likes
2,483
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,915 2,483 280
Ngoja kwanza nimsikilize Mbowe hapa Mwanza nitakuja kukusoma....
Mkuu unadhani kulikuwa na haja ya kuchangia hapa kati kati hasa ukizingatia kwamba hukusoma na huna muda wa kusoma uzi?
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,915
Likes
2,483
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,915 2,483 280
Umewahi kusoma Cybernetic model of leadership?
ongea point yako unayotaka kuongea "SPECIFICALY" Na kisha ioanishe na mada.Sidhani kama kuna haja ya kupimana juu ya umahiri na ujuzi wa theory hapa.
 
T

TECH WIZ

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Messages
1,675
Likes
21
Points
0
T

TECH WIZ

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2013
1,675 21 0
I like this well-thought out analysis,It has illustrated constructive & destructive Party building plans so it's up to Chadema's higher echelon of leadership to decide which way to go with.In my opinion the Party is applying Plan A at the moment.This can be good on the side of leaders' personal interests but really bad on the Party's interest side.Plan B is the sure way to go with if we really care about the Party and a Country as a whole.I know it's hard for the devious Politicians to opt Plan B since they will have to deal with very independent & free thinking minds,critical,curious & skeptical audience & very outspoken individuals so i know for sure they will keep sticking with Plan A where there's their friendly audience.So the answer is obvious.
 
Mkuu TECH WIZ nikujibu kwa kiswahili maana kingereza kinanisumbua kidogo,
Sipendi sana kuzundumzia kwamba kwa sasa CHADEMA imechagua plan ipi kati ya hizi na nawaachia wadau wenyewe watafakari.Hata hivyo taasisi ya kisiasa itakayochagua Plan "A" Kitaalam haiwezi kutoboa katika karne hii ya 21.Kitakachotokea ni kwamba itakuwa ni taasisi isiyotabirika, taasisi inayofuata upepo, mtiririko wa matukio, hizia za watu n.k mwishowe kutakuwa hakuna "Strategist" na watakapotokea hawatapata ushirikiano wa kutosha au mipango yao haitakuwa ikiratibiwa vizuri na hatimae ni kuyumba na kusambaratika.Hii ni kwa taasisi yoyote ile itakayojikita katia plan "A" Katika zama hizi.
 
Last edited by a moderator:
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
21,528
Likes
16,349
Points
280
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
21,528 16,349 280
wewe mwenyewe umeshusha theory ndeeeeeefu, ghafla inakuwa soo kuku-check kabla ya kuku-balance, usiwe mwoga, ndo ushalianzisha ivo.
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,915
Likes
2,483
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,915 2,483 280
wewe mwenyewe umeshusha theory ndeeeeeefu, ghafla inakuwa soo kuku-check kabla ya kuku-balance, usiwe mwoga, ndo ushalianzisha ivo.
Sijui kama nimekuelewa.Kuhusu urefu, ili kitu kiweze kuwa kamili na kuleta maana wakati fulani inabidi kiwe kirefu kidogo.Tatizo ni kwamba vizazi vya siku hizi havipendi kusoma na ndio maana unaona mtu anakurupuka anacomment bila hata kusoma.
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
16,687
Likes
3,243
Points
280
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
16,687 3,243 280
betlehem
Nimekusoma ndugu yangu na kwa ulivyo viandika ni MAJI na MAFUTA haviwezi kuenda pamoja hata siku moja.

Na nionavyo mimi PLAN A ni CHADEMA ya sasa na PLAN B ni chama ambacho kwa sasa hakipo lakini kwa Jinsi nilivyo isoma na kuisikia mikakati ya CHAUMMA basi PLAN B ni CHAUMMA.

USHAHURI WANGU KWAKO NA WENZAKO:

Ni wakati sasa wa kwenda kuimarisha CHAUMA na hakika mtafanya vizuri kwenye Siasa za TZ maana kila chama kina wenyewe na watu wake kwa maana ya Mashabiki na wapenzi.

Hakuna haja ya kuangaika na CHADEMA nyinyi songeni mbelew na mkumbuke tu kuwa makini msije makaleta watu wale wale walioshindwa NCCR, CUF, TLP au CHADEMA, Hakika leteni watu wapya kabisa.
 
Last edited by a moderator:
T

TECH WIZ

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Messages
1,675
Likes
21
Points
0
T

TECH WIZ

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2013
1,675 21 0
Mkuu TECH WIZ nikujibu kwa kiswahili maana kingereza kinanisumbua kidogo,
Sipendi sana kuzundumzia kwamba kwa sasa CHADEMA imechagua plan ipi kati ya hizi na nawaachia wadau wenyewe watafakari.Hata hivyo taasisi ya kisiasa itakayochagua Plan "A" Kitaalam haiwezi kutoboa katika karne hii ya 21.Kitakachotokea ni kwamba itakuwa ni taasisi isiyotabirika, taasisi inayofuata upepo, mtiririko wa matukio, hizia za watu n.k mwishowe kutakuwa hakuna "Strategist" na watakapotokea hawatapata ushirikiano wa kutosha au mipango yao haitakuwa ikiratibiwa vizuri na hatimae ni kuyumba na kusambaratika.Hii ni kwa taasisi yoyote ile itakayojikita katia plan "A" Katika zama hizi.
Tatizo ni kwamba hiyo Plan A ulivyoi-draw up ni kama vile uli-sketch Plan inayotumiwa sasa na Uongozi wa sasa wa Chadema na hiyo Plan B ni kama advice kwa Chadema itoke huko iliko ili kipanuke na kikubalike zaidi na ile jamaa ambayo bado inasua sua kuiunga mkono Chadema.Sorry It's My Opinion.
 
Last edited by a moderator:
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,915
Likes
2,483
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,915 2,483 280
betlehem
Nimekusoma ndugu yangu na kwa ulivyo viandika ni MAJI na MAFUTA haviwezi kuenda pamoja hata siku moja.

Na nionavyo mimi PLAN A ni CHADEMA ya sasa na PLAN B ni chama ambacho kwa sasa hakipo lakini kwa Jinsi nilivyo isoma na kuisikia mikakati ya CHAUMMA basi PLAN B ni CHAUMMA.

USHAHURI WANGU KWAKO NA WENZAKO:

Ni wakati sasa wa kwenda kuimarisha CHAUMA na hakika mtafanya vizuri kwenye Siasa za TZ maana kila chama kina wenyewe na watu wake kwa maana ya Mashabiki na wapenzi.

Hakuna haja ya kuangaika na CHADEMA nyinyi songeni mbelew na mkumbuke tu kuwa makini msije makaleta watu wale wale walioshindwa NCCR, CUF, TLP au CHADEMA, Hakika leteni watu wapya kabisa.
Hivi wewe na wenzako mnaokazana kunifukuza CHADEMA, Hivi nimewafanya nini jamani? kosa langu nini nini hasa ndugu?
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
16,687
Likes
3,243
Points
280
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
16,687 3,243 280
Mkuu TECH WIZ nikujibu kwa kiswahili maana kingereza kinanisumbua kidogo,
Sipendi sana kuzundumzia kwamba kwa sasa CHADEMA imechagua plan ipi kati ya hizi na nawaachia wadau wenyewe watafakari.Hata hivyo taasisi ya kisiasa itakayochagua Plan "A" Kitaalam haiwezi kutoboa katika karne hii ya 21.Kitakachotokea ni kwamba itakuwa ni taasisi isiyotabirika, taasisi inayofuata upepo, mtiririko wa matukio, hizia za watu n.k mwishowe kutakuwa hakuna "Strategist" na watakapotokea hawatapata ushirikiano wa kutosha au mipango yao haitakuwa ikiratibiwa vizuri na hatimae ni kuyumba na kusambaratika.Hii ni kwa taasisi yoyote ile itakayojikita katia plan "A" Katika zama hizi.

betlehem
Nakuuliza Tena CHADEMA ikifa leo wewe inakuuma NINI? Si uanzishe cha kwako kwa PLAN B na CHADEMA ikifa basi CHAUMMA ichukue Nafasi ?

Wansema ADUI MUOMBEE NJAA au ?
 
Last edited by a moderator:
T

TECH WIZ

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Messages
1,675
Likes
21
Points
0
T

TECH WIZ

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2013
1,675 21 0
betlehem
Nimekusoma ndugu yangu na kwa ulivyo viandika ni MAJI na MAFUTA haviwezi kuenda pamoja hata siku moja.

Na nionavyo mimi PLAN A ni CHADEMA ya sasa na PLAN B ni chama ambacho kwa sasa hakipo lakini kwa Jinsi nilivyo isoma na kuisikia mikakati ya CHAUMMA basi PLAN B ni CHAUMMA.

USHAHURI WANGU KWAKO NA WENZAKO:

Ni wakati sasa wa kwenda kuimarisha CHAUMA na hakika mtafanya vizuri kwenye Siasa za TZ maana kila chama kina wenyewe na watu wake kwa maana ya Mashabiki na wapenzi.

Hakuna haja ya kuangaika na CHADEMA nyinyi songeni mbelew na mkumbuke tu kuwa makini msije makaleta watu wale wale walioshindwa NCCR, CUF, TLP au CHADEMA, Hakika leteni watu wapya kabisa.
Nionavyo ni kwamba baadhi yenu ndani ya Chadema hata hamjui misingi ya hiki Chama.Hiki ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo kutofautiana kimtazamo & kukosoana ni moja wapo ya values za hiki Chama.You could be on the wrong Party for sure!Sorry!!??
 
Last edited by a moderator:
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
16,687
Likes
3,243
Points
280
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
16,687 3,243 280
Hivi wewe na wenzako mnaokazana kunifukuza CHADEMA, Hivi nimewafanya nini jamani? kosa langu nini nini hasa ndugu?

betlehem

Hivi nimekufukuza nimekushahuri?
Hivi kama wewe ni msomi mwerrevu na bora zaidi ya wengine, sasa kwanini unangangania kukaa na wajinga? Hivi ujuhi Samaki mmoja akioza basi wanaoza wote ?

Huoni sasa na wewe pamoja na ubora wote unaojidai kuwa unao, Unavyoendelea kubaki CHADEMA na wewe unaonekana ni walewale ?
 
Last edited by a moderator:
T

TECH WIZ

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Messages
1,675
Likes
21
Points
0
T

TECH WIZ

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2013
1,675 21 0
betlehem
Nakuuliza Tena CHADEMA ikifa leo wewe inakuuma NINI? Si uanzishe cha kwako kwa PLAN B na CHADEMA ikifa basi CHAUMMA ichukue Nafasi ?

Wansema ADUI MUOMBEE NJAA au ?
You are flipping wrong dude!Bethlem have as much right as you to speak his mind & no one not even you who could deprive him of that constitutional right.The Party's Constitution provide him with that freedom of expression right,Philosophical dogma is not allowed in Chadema only is allowed in the Communist Party of CCM where its leaders are chosen but not elected through the ballot box.We don't wanna see Chadema following the suit.
 
Last edited by a moderator:
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,595
Likes
534
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,595 534 280
Betlehem,

Habari za weekend?

Ndugu yangu, nimekusoma vizuri. Plan A na B umeziweka bayana. Hata hivyo kuna upungufu mkubwa katika hizi plan ulizoweka.

Umefanya assumption kwamba lengo kuu la Chadema kama chama cha siasa ni kupata fursa ya kuunda serikali.

Hata hivyo kwa Chadema hilo sio lengo kuu. Chadema ikifika 2015 hata ukiwaonyesha marking scheme ya jinsi ya kushinda uchaguzi, hawako tayari kuifuata marking scheme hiyo iwapo vitu fulani havijatimia.

Fursa ya kuunda serikali Chadema wanaitaka but with conditions.

Cc Pasco
 
Last edited by a moderator:
L

Lilambo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Messages
2,524
Likes
6
Points
135
L

Lilambo

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2013
2,524 6 135
Asante mkuu kwa uchambuzi wako.. Lakini kwa Tz ya sasa kupata chama kitakachoenda na plan B ni ngumu sana. Sbb viongozi wakuu wa vyama vya siasa nchini Tz wanaaply plan A ambayo inabeba maslahi ya wakubwa. Vijana na watu wenye mitazamo ya plan B wanapaswa kuunganisha nguvu na kuunda strong political party. Kwani tuliowategemea cdm wana madhaifu mengi sana.
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,595
Likes
534
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,595 534 280
Hivi wewe na wenzako mnaokazana kunifukuza CHADEMA, Hivi nimewafanya nini jamani? kosa langu nini nini hasa ndugu?
Kuwa Chadema na kuizungimzia Chadema au Chama chochote ni haki yako ya kikatiba. Vyama vinaendeshwa kwa kodi unayolipa.

Utaratibu huu wa kutoleana kauli za dharau uko Chadema kwa sababu kuna watu wanaoona chama ni mali yao binafsi.
 
Forum statistics

Threads 1,275,220
Members 490,932
Posts 30,536,052