CHADEMA kubalini kuna tatizo na kuchukua hatua, vinginevyo mtaendelea kukanusha

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Dalili za Uongozi wa Chama chochote, Umoja wowote, Kikundi chochote kuchokwa na wanachama wake ni pamoja na taarifa zake kuanza kuvuja hovyo hovyo.

Viongozi hawa huanza kutengeneza Makundi Makundi hasa pale inapotokea Wale wa juu kiuegemea/kupendelea upande mmoja. Makundi haya hayaishii kwa viongozi tu bali huenea mpaka kwa walaji ambao ni wanachama wa kawaida.

Siku za hivi karibuni limejitokeza ombwe la kinachoonekana wazi ni kuvuja kwa mambo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) zikiwemo barua za taarifa kwa wanachama wake na watanzania kwa ujumla kuhusu mamnbo mbalimbali, taarifa ambazo hata hivyo zimekuwa zikikanushwa ndani ya kipindi kifupi sana tangu zianze kusambazwa, jambo ambalo kwa mjuzi wa mambo anaweza pasi na shaka kufikia hitimisho kwamba aliyesambaza ujumbe huo ndiye aliyejitokeza kukanusha. Sitaki niwafumbue macho watu wengine waamini hivyo. Miongoni mwa siri zilizovuja siku za hivi karibu ni pamoja na:
1.Kikao cha siri cha Wabunge Vijana wa chama hicho mjini Dodoma. Wabunge siyo tu ni kundi muhimu sana ndani ya chama bali wana nguvu katika maamuzi.

2. Barua iliyosambaa katika Mitandao ya Kijamii ikionekana kuandikwa na kundi lingine Muhimu sana, kundi la Wasomi wa vyuo vikuu kupitia umoja wao wa Chadema. students' Organisation (CHASO). Historia inaonesha wasomi wamekuwa ni chanzo cha mabadiliko katika nchi nyingi sana duniani.

3. Barua ya Mkuu. Wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama ikiwataarifu Wanachama na Watanzania wote juu kuteuliwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). Mama Hellen Kijo Bisimba kuwa mjumbe wa Baraza la Wazee wa Chadema. Mama Bisimba anamaliza muda wake kuitumikia LHRC 30 may, 2018, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa na kituo hicho katika Mitandao ya Kijamii jana wakati wakikanusha Madai ya uteuzi wa Mtumishi wao huyo kuwa Kiongozi ndani ya chama cha siasa. Siku chache kabla ya kusambaa kwa barua ya Mama Bisimba kuteuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la wazee wa Chadema alionekana katika picha tofauti tofauti akiwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa Upande mmoja wa CUF, maalim Seif Sharif Hamad. Picha hizi oia zilisaambaa katika Mitandao ya Kijamii.

Chama au taasisi yoyote inapofikia hatua hii, mambo mawii tu ya msingi ya kujiuliza ni:
1. Tatizo ni nini?
2. Nini kifanyike?

Niende moja kwa moja kwenye tatizo. Kabla ya kujua tatizo nini, kwanza mnapaswa kukubali kuna tatizo, vinginevyo hakutakuwa na suluhu. Naandika haya kwa mapenzi mema kabisa. Ndani ya Chadema kuna uwezekano wa haya yakawa ni tatizo
1. Kuna watu hawaridhishwi na wanavyotendewa ukilinganisha na wengine (kuna upendeleo). Hapana siri hapa hili limekuwa likipigiwa kelele sana.
2. Basi tu watu wamechoka wanataka kuona mabadiliko hata kama mabadiliko hayo hayatakuwa na athari chana, ilimradi tu waone sura mpya,. Hiyo ni hulka ya binadamu.

Ni kifanyike baada ya kukubali kuna tatizo?
1. Ni kutafuta suluhu kati ya pande mbili ambazo hazikubaliani baadhi ya mambo
2. Kukubali mabadiliko, na hili ni la msingi sana.

3. Kudhibiti mfumo wa utoaji habari.
 
Unafikiri CCM wanapenda Chadema iwepo? ni lazima watengeneze kila aina ya propaganda ili ionekane Chadema haifai na ina migogoro.

CCM haiwezi kufurahi Chadema ikiwa wamoja.
Hili ndilo kosa mnalofanya, mnawapa nafasi wasaliti ndani ya chama kukiua chama kwa vile wanajua mtasema ni CCM, hoja dhaifu kabisa.
 
Unafikiri CCM wanapenda Chadema iwepo? ni lazima watengeneze kila aina ya propaganda ili ionekane Chadema haifai na ina migogoro.

CCM haiwezi kufurahi Chadema ikiwa wamoja.
Hakika CCM hawezi kupenda CHADEMA iwepo kuwatisha kama vile CHADEMA wasivyopenda CCM na SERIKALI yake ikafanya mazuri kwa wananchi wake. Utaona uzushi mwingi na kubeza na wachambuzi kibao.
 
Hakika CCM hawezi kupenda CHADEMA iwepo kuwatisha kama vile CHADEMA wasivyopenda CCM na SERIKALI yake ikafanya mazuri kwa wananchi wake. Utaona uzushi mwingi na kubeza na wachambuzi kibao.
Mkuu , hiki chama cha Chadema kimefikia mwisho wake, ni kama Kocha3 wa mpira ambaye wachezaji wake wamemchoka, atabaki kuilaumu timu pinzani kuwa inacheza rafu
 
Wewe mtoa mada unawaona hawa ccm ni watu bora kwa vile wameweza kususia mazishi ya mbunge mwenzao au? Kati ya siri kuvuja nani anavujiwa zaidi? Ni Chadema ambao siri zao zimevuja kama ulizosema wewe au ni CCM ambao siri zao zinavujishwa na Mange kila siku?
 
Mbowe kawaroga watu wake, hawapendi kabisa kusikia ushauri mzuri kama.huu unapotolewa. Waacheni tu wafie mbali.
 
Mkuu , hiki chama cha Chadema kimefikia mwisho wake, ni kama Kocha3 wa mpira ambaye wachezaji wake wamemchoka, atabaki kuilaumu timu pinzani kuwa inacheza rafu
Ukitaka uone kama Chadema imefika mwisho au la basi ruhusu Mikutano ya vyama vya Kisiasa.
 
Wewe mtoa mada unawaona hawa ccm ni watu bora kwa vile wameweza kususia mazishi ya mbunge mwenzao au? Kati ya siri kuvuja nani anavujiwa zaidi? Ni Chadema ambao siri zao zimevuja kama ulizosema wewe au ni CCM ambao siri zao zinavujishwa na Mange kila siku?
Mkuu mambo ya msiba yanaingiaje hapa?
Sijaona popote ambapo Mleta mada ameongelea msiba. Hata hivyo kwani kwenda msibani ni lazima? Chadema mbona mnavurugwa hivi?
 
Hatuhitaji ushauri toka kwa wachawi, watekaji,watesaji,wauaji, kama tukiharibikiwa si ndiyo furaha kwenu?
 
Wewe mtoa mada unawaona hawa ccm ni watu bora kwa vile wameweza kususia mazishi ya mbunge mwenzao au? Kati ya siri kuvuja nani anavujiwa zaidi? Ni Chadema ambao siri zao zimevuja kama ulizosema wewe au ni CCM ambao siri zao zinavujishwa na Mange kila siku?
Ni wapi mleta mada amesema ccm ni watu bora?
 
CDM Sio chama cha watu wanakubali kukoselewa na kujikosoa, kwao kila kitu ni perfect.
 
Back
Top Bottom