CHADEMA kuasisi mgomo wa madereva ni kwa manufaa ya nani?

Kama kweli chadema imefikia hatua hii ya ku control hata secta ya usafiri wakati serikali ipo,basi ina haki yakupewa nchi ituongoze ina mipango makini.Hongera Chadema kwa uwezo mkubwa kimipango
 
Ni kweli mkuu,CHADEMA ni hatari sana ndo imeifanya Tanzania kuwa maskini ya kutupwa,ni hawa hawa CHADEMA ndo walisababisha rais wetu kuugua tezi dume,ni CHADEMA ndo walisababisha vurugu za panya road,ni hawa CHADEMA ndo wanasababisha wagonjwa wanakufa hosp kwa kukosa huduma bora na madawa,ni CHADEMA ndo imefanya vijana wengi hawana ajira,yaani hawa hawa CHADEMA ndo walimtesa Dr Ulimboka na kulifungua gazeti la mwana.halisi,ni CHADEMA ndo walimuua Mwangosi na kusingizia eti ni police,CHADEMA ndo wanapeleka meno ya tembo ughaibuni na wanalinda majangili, ni Dr slaa,mbowe na kina Tundu Lissu ndo walikwiba mapesa ya ESCROW na EPA,CHADEMA ndo wameua viwanda nchini,ni hawa hawa Ndo wameangusha thamani ya sh,ni CHADEMA ndo walimuua Baba wa taifa ili waweze kuuza mali za umma kama Benk ya NBC na migodi,ni CHADEMA ndo wanasinzia bungeni na kudai mishahara mikubwa,Watanzania tuwaogopeni CHADEMA,ndo hao hao wamefanya maisha kuwa magumu hapa Tanzania huku wenyewe wakila mboga saba kila siku,jamani CHADEMA haifai kabisa.
 

[/................... Wazalendo walio ndani ya Chadema wakiwemo wanaomuunga mkono Zitto tayari wameanza kulipinga suala hili na muda si mrefu mtasikia mvurugano ukitokea........ ..........................

Blah blah nyingi lakini hicho hapo juu ndiyo ulichopanga toka moyoni! Pepo mchafu akuachie huru!
 
Duuuh sikuwahi kufikiria kua kuna watu wenue akil za kushikiwa ila leo nimemuona mtu.......kwaher
 
Hoja ya kuisingizia CDM kila jambo, ni kukosa Busara ya Mawazo tu na umakini pia. Walau ungekuja na hoja kwa njia ya kuuliza kuliko kuhukumu moja kwa moja tena kwa kutaja majina ya watu. Ipo siku atakuja mwengine kama wewe na kusema Mf; JF CDM ndio wanaipa Promo ama Kiki.
NAWAZA TU
 
Huu siyo mgomo unalazimishwa kuitwa mgomo. Ukimtisha mtu akiweka basi lake barabarani mtalipiga mawe huo ndio mgomo? Kuna wahujumu nchi wachache wanaokodi wahuni kufanya haya ili mgomo uonekane umefanikiwa kumbe hamna kitu. Twendeni tu tutafika
 
Na hili lifoleni linalonitesa hivi sasa for more than two hrs sijatoka posta ni CDM wanahisika 😄😄 kweli mtu akiishiwa mawazo anaweza kuandika chochote... No vyema ukaisaidia serekali mawazo wakutatua changamoto kuliko kuhangaika Na CDM, CDM wanahusikaje Na mambo haya??
 
Ukisikia vilaza na huyu mtoa mada n mmoja wapo, chadema inahusikaje ktk masual ya madereva
 
Back
Top Bottom