CHADEMA: Kuanzia Jumatatu, Sept 22 ni wiki ya Maandamano Nchi nzima bila kikomo

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
10628330_1534208343480978_2953897830793713955_n.jpg


KESHO NDIO KESHO JINO KWA JINO. DOLE KWA DOLE, MPAKA WAVUNJE BUNGE

.CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kimetangaza rasmi kuanza maandamano pamoja na Migomo nchi nzima kwaanzia kesho mpaka Jumamosi kushinikiza Bunge la Katiba lisitishwe kwa madai Bunge hilo limekuwa likitekezea pesa za Watanzania huku Katiba haipatikani.

Maandamano hayo yametangazwa muda huu jijini Dar Es Salaam na Mkurugenzi wa Mafunzo na oganizesheni wa Chama hicho,Benson Sengo Kagaila wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo alisema licha ya Jeshi la Polisi kuwanyima Kibali cha kufanya Maandamano pamoja na Migomo ambayo ni haki ya kikatiba kwa kila mtanzania,basi chama hicho kitaanza maandamano rasmi kuanzia kesho Jumatatu mpaka Jumamosi.

“Jeshi la Polisi nchini limetunyima haki ya kufanya Maandamo ambayo kimsingi ni haki ya kila Mtanzani kudai haki yake ambayo katiba imetamka wazi,basi Kuanzia kesho mpaka Jumamosi Tunatangaza Maandamano nchi nzima kupinga wizi huu unaofanyika Bungeni Dodoma na hatutamuogopa mtu yeyote,tena nawataka watanzania wajitokeze kila walipo wajumuike katika kufanya Maandamano nchi nzima”alisema Kagaila

Kagaila alizidi kusema Maandamano haya yatafanyika nchi nzima na kila mkoa maandamano hayo yataanzia kwenye ofisi za Chadema kwenye Mikoa hadi kwenye Ofisi za Mkuu wa mkoa,

“Maandamano haya yatafanyika kwa awamu katika wiki zima,kwa upande wa Mkoa wa Dar Es Salaam tutafanya Jumatano wiki hii na tutaelekea Ofisi za Waziri Mkuu na kwa upande wa Dodoma wataelekea Ofisi za Bunge na mikoa mingine watachagua lini hasa katika wiki hii wataanza maandamamo ila nimetoa maagizo kwa Viongozi wa Chadema wa Mikoa kuhakikisha wanachagua siku yoyote ndani ya wiki hii kuanza maandamano,tena wasiogope polisi wala nani kwa sababu Polisi wamekuwa upande wa Chama cha Mapinduzi na Kuacha kazi yao kikatiba”alizidi kusema Kagaila.

Vilevile Kagaila aliwataka watanzania popote walipo kujiweka tayari kwa maandamano kwani maandamano hayo ni ya amani na kusema Chadema haitaweza kukubali kuyumbishwa na Jeshi la polisi ambalo limekuwa likifanya mambo kibabaishaji.

Kwa Upande wake Wakili wa Chama hicho John Mallya alisema wamejipanga kisheria katika kuhakikisha haki ya msingi ya maandamano inapatikana na kuwataka wanachama pamoja na wapenzi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye maandamo hayo’.

“Tumeomba kibali cha maandamano Jeshi la polisi linatukatalia na kusema Bunge la katiba liko kisheria kama ndio hivyo mbona bunge lenyewe linakiuka sheria ya mabadiliko ya katiba kwa kitendo chake cha kujigeuza na kuanza kuchukua maoni kutoka kwa wananchi ambayo sio kazi yake,kwa hiyo nawaomba watanzania wote kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano”alisema Mallya.

 
Kila la kheri makamanda wa jiji la mbeya katika maandamano yav kesho tarehe 22/09/2014 jiji la mbeya chini ya rais wa mbeya kamanda joseph mbilinyi a.k.a sugu akishirikiana na waziri mkuu mwenye mvuto kuliko pinda kamanda john mwambigija a.k.a mzee wa upako wataongoza maandamano ya amani kupinga bunge maalum la katiba kuendelea kutumia mabilioni ya fedha za wavuja jasho wa tanzania masikini ambao ni ufisadi.

Kama ilivyo kawaida ya umma wa mbeya,wabibi,wababu,vijana na makamo wakiingia barabarani huwa ni mpaka jeshi la wananchi na jeshi la kujenga taifa liingilie kati(rejea maandamano ya tarehe 11.11.2011) ambapo jeshi la polisi lilisalimu amri na nguvu ya umma. Maandamano ya kesho ni ya amani na kama polisi watayaingilia iwe kwa maagizo ya ccm ama kwa utashi wao waandamanaji wawe tayari kujilinda na watashinda.

Chama cha wananchi(cuf) nacho kupitia kwa mwenyekiti wake wa chama taifa prof lipumba kimetangaza kuanza maandamano nchi nzima.Binafsi Nawashukuru wanacuf kwa kuanzisha maandamano pia.
 
Hakuna mwenye uwezo wa kuzuia nguvu ya umma ..nawatakieni kila heri makamanda msiogope risasi wala mabomu kwani uonevu na hujuma za polisi juu yenu zina mwisho wake makamanda msikate tamaa songeni mbele daima






View attachment 187050
 
Hakuna cha maandamano wala nini. Jana mmetudanganya huku Arusha kumbe mnaogopa polisi.
Kweli kabisa Mkuu. Wameshindwa Dodoma, Dar es Salaam, Arusha, Hai, Mwanga, Mwanza nk. Huko ambeya hawawezi kufanikiwa. Style ile ile iliyotumika sehemu nyingine ndiyo itakayotumika hiyo kesho kusambaratisha hao wahuni tena bila ya madhara yoyote
 
Back
Top Bottom