Chadema kuandamana nchi nzima tarehe 16, kuupinga muswada......! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kuandamana nchi nzima tarehe 16, kuupinga muswada......!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by King junior, Apr 9, 2011.

 1. King junior

  King junior Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chanzo cha kuaminika, "kutoka kwa 'jembe' LEMA GODBLESS" akihutubia katika ufunguzi wa tawi la Udom, amesema kuwa "wapo katika mchakato wa kuandaa maandamano tarehe 16 mwezi huu kuupinga vikali muswada wa katiba mpya" mbali na hilo, alitangaza rasmi kongamano la vyuo vikuu litakalofanyika Area D, mjini DODOMA siku ya kesho tarehe 10/04 kuanzia saa nne asubuhi, kongamano hilo linatarajia kuhusika na kujadili mambo mbalimbali yanayoikumba nchi hii, likiwemo la katiba mpya, Dr. W. Slaa ni miongoni mwa watakaokuwepo katika kongamano hilo........!
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hawa chadema tumeshawachoka na maandamano yao ambayo hayana faida yoyote kwa mwananchi wa kawaida zaidi ya kuumiza wasio na hatia!
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri sasa wataijua nchi nzima maana yake nini?
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  watu wenye fikra za rejao ndo waliopo madarakani ndo maana nchi haipigi hatua. mawazo mgando ni hatari saana kwa maendeleo ya nchi.
   
 5. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Umewahi Kuandamana?? Basi kama ndivyo then usiandamane ili wakose watu!!!!!!!!!!!!
   
 6. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hayo maneno akisikia JK atarudiwa na kale ka-ugonjwa wake uleee, akitaka kupotezea anaanguka. Alafu mnasahau mnaanza kujadili kuanguka
   
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Safi saana mpaka kieleweke, Zitto vp? CCM B wanamtangaza lini, good lema na wapganaj wote wa ukweli
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Siasa za Tanzania ni vichekesho, kidogo maandamano, kidogo kususa, kidogo kuzomeana.

  Hivi ule si mswada? Kwa nini Chadema wasiandike mswada wao wanaouona unafaa waupeleke bungeni? Simpo. Mswada si sheria, ni mapendekezo tu. Na waoi wanahaki ya kupeleka mswada wao. Wakikataliwa hapo hata mimi ntaunga mkono maandamano yao. Lakini kwa sasa, mnhhhhh, kudanganyana tu.
   
 9. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ulikuwa wapi? hadi nimekumisi.
  Sisi tutaanzia sakina-sanawari-kwa mrefu-usa river hadi Semunge kwa babu. Tunagonga ki-cup alaf tunaretreat kwa nguvu mpya tukipita majengo-mbauda hadi olasiti
  Karibu nduka.
   
 10. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tunasubiri tuone nini kitafuata baada ya maneno na intelijensia za mwema
   
 11. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />  Acha Ubwege wewe ****,Hayo machache tu ambayo Ccm wanayafanya ni kwa sababu ya Hekaheka wanazopata kutoka Chadema,wangekuwa wameshachapa Usingizi zaidi!!
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu, nilikuwa kifungoni bana, nadhani wengine watakuwa maeneo ya Tanga, Igunga, Mikindani, na Mchinga wakianadamana.
   
 13. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sawa, endeleeni wanaharakati wetu na maandamano yasiyo na tija.
   
 14. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />


  Kwa hiyo wewe Una Hekima na Akili Kuliko Slaa? Ungekuwa na Akili ungekuwa kada wa Ccm? Kwani hao wajomba zako kuleta Mswada uliyosheni hila ni kitu cha bahati mbaya? We are taking it to the streets,come what may,this is a defining moment!! No turning back!
   
 15. m

  mwanawakondoo New Member

  #15
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaleyale ya CUF ya miaka ileee... Watu wakafa, wakalema na kwa mara ya kwanza Tz ikazalisha wakimbizi kibao. Sasa yakowapi?
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Sana tena, hapati hata robo ya hekima akili zangu. Sijawahi kufukuzwa au kukataliwa uongozi popote pale. Na pia sijawahi kuwa na kashfa ya kung'ang'ania zinaa na kuvunja amri ya sita! Aliyoisomea! Sasa akili na hekima za slaa ziko wapi hapo?
   
 17. s

  seniorita JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  MaandamanO ndiyo njia sahiihi ya kuweka wazi disappointments za wananchi, it is a non-violence way to demand what its rightly ours....
   
 18. King junior

  King junior Member

  #18
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi umeshauona huo muswada majimshindo? Unafikiri walichokiandika mle ni mazuri? Wamempa nguvu kubwa Baba Ridhiwan, kila kifungu ni rais atafanya hivi, au vile, kuna kipengele kinakataza haki ya wananchi kuhoji chochote kuhusu rais, hata bunge, hiyo haitoshi wameandika kwa lugha ya kingereza wakati inatuhusu wa-Tz ambao kimombo kwetu ni issue, hvi kwa akili yako bila CDM, CCM wangekuwa na mpango hata wa kuleta fake muswaada wao huu.? Uwe unafikiri kabla hujaongea, kama unaona utaongea pumba utulie, unafikiri kwenye muswada wamekubali wanasiasa wahusike kwenye muswada huo? Wanawaogopa, we unaropoka tu "CDM wakiandaa muswada wao, unadhani ninyi CCM mtaukubali??? Utakuwa umelalia haki kitu ambacho ccm wamezoea wizi hvyo watapinga tu, nawaunga mkono CDM na Z.bar walivyofanya....!
   
 19. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wanafunzi wa UDOM kumbuke na lengo lilowapeleka Dodoma. Msikalie siasa tu mkasahau madarasa, mutakwenda na maji. Ukidisco hapo Chuoni, utakuwa form six leaver tu ambaye hivyo vyama vya siasa unvyovishabikia vinaiona ni elimu ya chini. Kwa hiyo waweza kuambulia umwenyekiti wa shina au tawi la CDM, CCM, TLP n.k huku wasomi wakichukua nafasi za juu. Shikeni sana lililo wapeleka vyuoni ili mkimaliza muweze kugombea vyeo vya juu katika vyama vyenu.
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Nimesema, kama chadema hawakuupenda huo mswada, si waandike wao? Kuna aliewakataza. Jee ambayo hawajayapenda hayajadiliki? Na nani aliosema haujadiliki? Kwa nini chadema wakae wanatisha watu kwa maandamano? Na kudanganya watu? Kutaka kuvunja amani kwa kutumwa na nchi za nje?

  Na mimi kama ni serikali nayapiga marufuku maandamanoi na halafu waingie mitaani. Kale kamkong'oto ka arusha na pale udsm kama hakijawakolea sasa ndio mtalijuwa jiji.
   
Loading...