CHADEMA ku-survive bila ruzuku: CCM oneni aibu na iwe mwanzo wa kufuta ruzuku kwa vyama vyote vya siasa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,887
143,983
Kama CHADEMA wameweza ku-survive bila ruzuku mpaka leo hii, na zaidi wameweza kubuni utratibu mpya wa kuwaingizia mapato kupitia michango ya wanachama,basi CCM kama chama kikongwe kinapaswa kuona aibu na kuacha kuendelea kupokea ruzuku kutoka serikalini.

Wakati umefika vyama vya siasa vianze kujitegemea na kama ni ruzuku, basi itolewe kwa vyama vichanga na kuwe na muda maalumu wa kisheria wa kuvilea baada ya kupewa usajili wa Kudumu na baada ya hapo na vyenyewe vijigemee.

Haiwezekani kinda la ndege linzaliwa leo na baada ya muda linaanza kujitegemea lakini CCM yenye umri wa zaidi ya nusu karne, bado inaishi kwa kulelewa na kodi za masikini wa nchi hii na wakati huo huo viongozi wa hiki chama wanaimba vijana wajiajiri ili hali wao wenyewe wameshindwa kuiendesha CCM bila ruzuku. Aibu!

Badala ya kuimba vijana wajiajiri, achieni hiyo ruzuku irudi serikalini ili itumike katika kuajiri vijana wanaomaliza masomo na kubaki kurandaranda mitaani wakikabiliwa na ukosefu wa mitaji na mazingira magumu ya kufanya biashara.

Binafsi napendeleza chama ambacho kinashindwa kujitegemea kimapato iwe ni kigezo kimojawapo cha kukataliwa Katika sanduku la kura.

Hapa chini na ungana na kauli hii ya Mbowe ya kukataa ruzuku baada ya Waziri wa fedha kumpigia simu akimtaka wakachukue hiyo ruzuku ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni moja.

Hii ndio kauli ya Mbowe kwa mujibu wa hii tweet ya John Pambalu:

"tumekataa hata senti 5 ya serikali ya ruzuku. Tunaijenga Chadema yenye kujitegemea. Waziri wa fedha ananipigia simu 'Mbowe unajua tangu uchaguzi mnazo zaidi ya bilioni moja zenu, njoo mchukue fedha zenu'.. Nikamuuliza 'urafiki wetu na CCM umeanza lini?'"- @freemanmbowetz.
 
Waziri wa fedha ananipigia simu 'Mbowe unajua tangu uchaguzi mnazo zaidi ya bilioni moja zenu, njoo mchukue fedha zenu'.. Nikamuuliza 'urafiki wetu na CCM umeanza lini?'"
Huyo ndo Mbowe bana
trumpsmirk.png
 
Nafikiri hili ni hitaji la kila mwananchi.

Ila wanasiasa ni wanafiki tu.

Kwanza suala la Mbowe kuitaja taja hiyo 1B tafsiri yake ni kuitamani. Sitaki nataka.

Wakishakutana na Samia, wale COVID-19 wataendelea na ruzuku itachukuliwa na wafuasi watademka, ila wananchi hatutashangaa.

Hao ndio wanasiasa.
 
Kama CHADEMA wameweza ku-survive bila ruzuku mpaka leo hii, na zaidi wameweza kubuni utratibu mpya wa kuwaingizia mapato kupitia michango ya wanachama,basi CCM kama chama kikongwe kinapaswa kuona aibu na kuacha kuendelea kupokea ruzuku kutoka serikalini...
Usipologwa leo ushukuru sana Mungu
 
Wakati umefika vyama vya siasa vianze kujitegemea na kama ruzuku, basi itolewe kwa vyama vichanga na kuwe na muda maalumu wa kisheria wa kuvilea baada ya kupewa usajili wa Kudumu na baada ya hapo na vyenyewe vijigemee.
Naunga mkono hoja.
P
 
Naunga mkono hoja.
P
Siku ukikutana na Mama kupitia kikao cha wazee wa Dar-es-Salaam, wanahabari au vinginevyo, toa hii hoja kwa Mama.
 
Aisee..

Kama kila mwezi mna 140,000,000 ni kweli zitakuwa zimeshafika Billion moja na ushee...

Tatizo ni kuwa, hizo ni pesa haramu zinazotokana na wabunge haramu kutoka uchaguzi haramu...!

Huu ni msimamo wa watu wakweli na kamwe siyo waongo...
 
Walijichanganya walipomuona mama mwenzao leo wameshituka and it's too late.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom