CHADEMA kitashinda uchaguzi wa mwaka 2020 kwa sera zao nzuri sio kutegemea urafiki wa kinafiki

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Kumekuwepo na Mjadala ambao unachochewa zaidi na makada wa ccm juu ya maadhimio ya Baraza kuu la Chadema la Tarehe 27 mwaka huu la kumuunga mkono Uhuru Kenyatta Katika uchaguzi uliofanyika August, 8 mwaka huu ambapo Chama cha Jubilee kiliibuka kidedea.

Hoja zao zimejikita zaidi kwanini Chadema kimeacha chama cha upinzani cha Kenya na kuamua kusapoti Chama tawala, wanafikiri kila vyama tawala ni vyama Rafiki na kila vyama vya upinzani ni vyama Rafiki.

Ninapenda kuwakumbusha kidogo mwaka 2002 baada ya muunganiko wa vyama vitano vya Kenya vikajipa jina la National Rainbow coalition (NARC) chini ya Mwai Kibaki na Raila Odinga kiliweza kukiangusha cha Dola cha KANU chini ya Uhuru Kenyatta ambacho kilikuwa chama Rafiki cha ccm.

Mwaka 2013 ulianzishwa umoja wa vyama unaitwa National Alliance (Jubilee) Chini ya Uhuru Kenyatta na William Uruto na kupambana na muunganiko mwingine wa vyama unaoitwa Coalition for Reform and Democracy (CORD). Chini ya Raila Odinga na Jubilee ikaibuka kidedea.

Chadema na Urafiki na ODM na kwa vile ODM ni Mshirika wa CORD Chadema kiliamua kuungana na Cord katika uchaguzi wa mwaka 2013 ambapo kilitoa gharama zake hili kuhakikisha ODM inashinda uchaguzi ule japo Dr John Magufuri alienda Kenya kumsaidia Raila Odinga.

Chadema iliona ni sawa maana ODM na Chadema ni taasisi na nje ya Tasisi kuna Urafiki wa MTU mmoja mmoja na sio jambo la ajabu Magufuri kuwa na Urafiki na Odinga hata Halima Mdee alikuwa na Urafiki na Esther Bulaya tangu akiwa ccm.

Ilipo fika zamu ya Chadema, mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu wa Tanzania CCM ikamsimamisha Dr John Magufuri ambae ni rafiki wa Raila Odinga cha ajabu Odinga akaacha kuuthamini Urafiki wa ODM na Chadema ambazo ni taasisi akathamini Urafiki wake na Magufuri kwa kumuunga mkono na kuyapiga teke Makubaliano waliojiwekea na Chadema.

Uhuru Kenyatta japo chama chake hakikua na Urafiki na Chadema alikuwa anaombea Magufuri ashindwe ili Odinga asiwe na Nguvu nchini Kenya waswahili wamesema adui wa adui wako ni Rafiki yako.

Uhuru Kenyatta alikuwa hapendi Magufuri kwa sababu atamsaidia Odinga kushinda mwaka 2017 na Chadema ilikuwa inapambana na Magufuri kama Mgombea wa ccm.

Katika dhana hiyo wewe ulitegemea Chadema imuunge mkono Raila Odinga na ukizingatia Jubilee sio chama Dola Bali ni chama tawala na Chadema ina vyama
Rafiki ambavyo vina Tawala kwa mfano New patriotic party (NPP) cha Ghana chini ya Nana Akufo-Ado, kwa hiyo Chadema sio dhambi kukiunga mkono chama tawala.

Katika uchaguzi wa mwaka 2017 ccm ilikuwa upande wa NASA maana Mwenyekiti wao wa chama alikuwa anamsapoti Odinga na Chadema kilikuwa upande wa jubilee Mwenyekiti chama ndio msemaji mkuu wa chama.

kila chama kipo ili kishike Dola ila iwapo kikitokea chama chochote au mtu Yoyote kukisaidia kushika Dola lazima awe Rafiki chama hicho kwa sababu umekisaidia kifikie Malengo ambayo kilikuwa kimejiwekea.

Mfano mzuri Vyama vya Kusini mwa Afrika ambavyo ni MPLA cha Angola, ANC cha Afrika Kusini, ZANU-PF cha Zimbabwe, MPLA cha Angola, FRELIMO cha Msubiji, SWAPO cha Namibia na Vyama rafiki vya CCM.

kwa sababu ya chama cha TANU cha Tanganyika kilivisaidia vyama hivyo kuingia Madarakani kama ambavyo TANU ilivyokuwa na Urafiki wa CCP ya China kwa sababu ya kupata msaada wa kushika Dola.

Mimi sioni kama Chadema inategemea msaada wowote Kutoka kwa Jubilee katika uchaguzi wa mwaka 2020 maana Chadema imejipanga kimikakati kushinda sio kwa kutegemea Urafiki wa kinafiki kama wa ODM.

wanaccm ni kama wale watu wa kipindi cha Nuhu ni wagumu sana kunielewa ninaposema Chadema itashinda mwaka 2020, mpaka waone maji yameejaa na safina linaelea.

Kauli za Magufuri pamoja na maigizo yao ya kuwatangazia watu wasimame barabarani ili ionekane watu wamezuia masafara wa Rais, Vitendo vya MaRC na MaDC pamoja na kamata kamata za polisi ni ishara ya ushindi.

vile vile Sera nzuri za Chadema ambazo watu sasa wanatamani kuzisikia, Ahadi hewa za ccm, Serikali kuwa na mawaziri wapumbavu na maisha magumu ya watu ni ishara ya ushindi.

Wanasiasa hodari wa Chadema kama vile Tundu Lisu, Halima Mdee, Salimu Mwalimu,John Heche na wengine wengi ambao hoja zao haziwezi jipiwa na kiongozi yoyote wa ccm.

Bali ccm wanaenda kuomba msaada kwa polisi wawanyamazishe kwa kesi za Uchochezi, ccm kuwadhoofisha watu ambao walikuwa wanakisaidia chama kama Nape hi nayo fimbo.

Kuwa na watu ambao hawana mvuto kama Pole pole, Mpogolo, Bashite ambao hawawezi kuongea kwenye mikutano ya Hadhara nayo ni sababu Pole Pole Hawezi hata Robo heka heka za Nape.

Bunge Kutokuwa Live watu kutokujua Bajeti ya Serikali na Mipango ya Serikali Bungeni watu kutokuona Michango ya wabunge wao Bungeni nayo ni sababu tosha.

Wabunge Wa Upinzani wanaweza sema niliongea sema kwa vile Bunge halionyeshwi ndio maana hamkuniona lakini wa ccm akisema hivyo ni kuichonganisha Serikali yake na wananchi.

Ni Mimi Mhere Mwita.
 
Uchambuzi mfu.
 
Hivi kukiwa na mkutano wa vyama vya upinzani Afrika ya Mashariki na ukafanyika nchini Kenya, je CHADEMA watashiriki?
 
Chadema itaungana na yeyote bila kujali kama ni chama tawala au chama cha upinzani ilimradi tu tufanane misimamo na misingi ya kile tunachokipigania
 
Wengi mmejifunza kuandika na si kuelewa!!

Moja CHADEMA haijaunga Jubilee kama unavyoandika hapa. CHADEMA kwa kukosa sera bora kinafuata kauli ya wanachama wake wenye mrengo wa kujiinua wenyewe binafsi kama akina Lowassa, TL, Wema, nk. Maranyingi wanatoa kauli ambazo mwisho zinabebwa na chama.

Kinachofanyika ndani yake ni ukosefu wa kusoma alama za nyakati na kufanya Timings. Lowassa ndo ameibua haya na Chama kikaunga bila kufikiri. Hii inaonyesha kukosa sera na upeo wa kiuongozi ndani ya chama.

Tunahitaji watu wenye uelewa wa siasa na mfumo toauti wa uendeshaji siasa na si huu wa mbowe uliokosa mashiko.

Hatuwezi kuandika kwa kupamba wakubwa huku tunatengeneza taswira hasi kwa jamii.

Unaandika yale waliyoandika wenzako 2011-2015 kwa kutopenda kufikiri, leo wamepotea mtandaoni.

CHADEMA tunaipenda, ila imekosa mfumo na falsafa ya kimaendeleo. Hatuwezi kuendelea kwa kutetea uovu unaoendelea ndani ya chadema hata kife. Tutasema.
 
  • Thanks
Reactions: kpm

Great mind!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema itaungana na yeyote bila kujali kama ni chama tawala au chama cha upinzani ilimradi tu tufanane misimamo na misingi ya kile tunachokipigania
kwa hiyo unataka kulinganisha ukawa na jubilee? we jamaa bhana!
Hivi mmekosa kabisa pa kushika!
 
ccm sio kua hawaelewi,niwaelewa wazuri tu,na wanajua kabisa kua hawapendeki wala kuungwa mkono,hivyo turufu yao sasa ni ubabe unyanyasaji,nauonevu kwa yeyote anaye wakosoa au anayewaeleza ukweli.ndo maana tunaona kuleta maendeleo kwa raia ni kugumu,hivyo hela ya maendeleo,wanaelekeza kununua wapinzani kama madiwani na yeyote atakeyefika bei baada ya kuelemewa na umaskini unaoliua taifa sasa hivi.na walijua tu wakitia nchi umaskini,watawanunua wapinzani legelege na wasaliti watakaoshindwa kuvumilia wakiwa katika umoja kutafuta ukombozi.njia ya ccm ni kurudia chaguzi ili waendelee kuwepo kama Zanzibar na madiwani wa upinzani sasa hivi,lipumba na mkewe sakaya, slaa na wajinga wa aina hiyo.tudumu tu katika kuomba na kuamini,muda sio mrefu watakwama tu.bagbo yuko wapi ? Kaburu aliyejimilikisha Afrika kusini yuko wapi ? Hata ccm nayo itapita siku moja.mpaka kumuita TB Joshua,sio dalili nzuri ! maji hapo pomwani.Mungu tunaoumia na kuteseka ni wengi kuliko walao makombo mezani mwa bwana wao.tunakuomba usikie kilio cha wengi,na utuponye na dhuluma ya ccm mtesi wetu.huna likushindalo Baba yetu.tunaanguka miguuni pako,tukiitia ukombozi,toka mikononi mwa ccm watuachie huru.tujibu Mungu Mara hii tu,tumefika mwisho kwa maonevu tunayopitia.onekana Mungu wetu tunayekuamini na kukutegemea,Amen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ungejaribu kupinga chadema kumuunga mkono Kenyatta uone nn kingefata, hako kacheo ulichonacho kangenyofolewa fasta! bado cjaona ndan ya chama mwenye kupinga maamuzi ya mbowe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kukiwa na mkutano wa vyama vya upinzani Afrika ya Mashariki na ukafanyika nchini Kenya, je CHADEMA watashiriki?
Chadema iko tayari kushirikiana na mtu yeyote wa ndani na nje atakayesaidia kuing'oa ccm madarakani na kuwakomboa watanzania kutoka kwenye utumwa wa milele .
 
Back
Top Bottom