CHADEMA Kisipoangalia Kitarudi Kuwa "Chama cha Msimu!"

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,192
1,971
Hali ya mambo inavyoenda CDM kimekuwa kimya sana ukilinganisha na kilivyokuwa enzi za "Maisha Bora kwa kila Mtz!" Wamebaki tu kusema kuwa" Dr Magu anatumia sera zetu!"
Sijui hiyo gia waliyobadilishia angani imesababisha haya yote?
Kama mambo yataendelea kama yalivyo basi ni dhahiri kuwa Chama hiki kitarudi tena kuwa cha msimu kikisubiri tu wakati wa kuomba kura!
Otherwise, warudi kama walivyokuwa au wafanye zaidi ya hapo. Pia wanatakiwa watembelee wananchi ili kutimiza ahadi walizotoa. Kama watakula jiwe kama ilivyo wakati huu wa "Hapa Kazi tu" mwaka 2020 watabaki na Wabunge 2 tu Bungeni!
Ni ushauri tu kwa CDM, kama hawataki wanaweza kuacha tu!
 
Watetezi wa UKAWA/CHADEMA wako kuandaa "matamko mazito?"
 
Kwa akili hii usingeweza kuendelea kuwa moderator jf.
yaonyesha akina maxence walikustukia unaharibu jamvi.
 
Washabiki wa Chadema ndio wanaoua chama wala si Mbowe ...maana hawashauri, hawaonyi, hawawajibishi viongozi wao ....mpaka sasa hawaamini Chadema iko kwenye hali mbaya kisiasa na kifalsafa ....ila itafika dakika watalaumiana wao kwa wao na hapa hapa JF mtashuhudia .....
 
Kama Mshauri wa chama ni mzee Kingunge au Lowassa unategemea nini?
 
Washabiki wa Chadema ndio wanaoua chama wala si Mbowe ...maana hawashauri, hawaonyi, hawawajibishi viongozi wao ....mpaka sasa hawaamini Chadema iko kwenye hali mbaya kisiasa na kifalsafa ....ila itafika dakika watalaumiana wao kwa wao na hapa hapa JF mtashuhudia .....
Mkuu hili la Mwapachu ni mwendelezo wa "project"..ya kujenga taswira hasi kwa chadema bila wao kujuwa na hili litasababisha wengi waliounga mkono chadema kabla kukata tamaa na kuamua kupigia CCM kwa "trend" hii,angalau CCM kuruhusu fikra mbadala inaiboresha lakini hili la chadema kutengeneza mazingira kwamba wanachama wote "wana akili moja,hawapingi wazo"...ni bomu hatari kusababisha msambaratiko.
 
Siasa zinabadilika. Ila muda ni mfupi mno kwa mtu kuhama chama tangu uchaguzi upite. Ni wenye tamaa tu wanahama baada ya uchaguzi. Baada ya miaka 2 wataona kama walikuwa sahihi au la. Kwa sasa ni usanii...
 
Dua za kuku hizi miaka nenda miaka rudi hazikomi
Tatizo lako unafikiri kuwa Chama kitajengwa kwa kutoa matamko kwenye vyombo vya Habari kama afanyavyo Mbowe na Lissu badala ya kufungua matawi!
 
Tatizo lako unafikiri kuwa Chama kitajengwa kwa kutoa matamko kwenye vyombo vya Habari kama afanyavyo Mbowe na Lissu badala ya kufungua matawi!
Naona tumepishana mahali tukubaliane kutokubaliana hatuwezi kuwa na mitazamo inayofanana
 
Washabiki wa Chadema ndio wanaoua chama wala si Mbowe ...maana hawashauri, hawaonyi, hawawajibishi viongozi wao ....mpaka sasa hawaamini Chadema iko kwenye hali mbaya kisiasa na kifalsafa ....ila itafika dakika watalaumiana wao kwa wao na hapa hapa JF mtashuhudia .....
Eti kwa mawazo yenye ueledi wanamtegemea Mmawia humu JF......
 
Back
Top Bottom