CHADEMA Kinondoni: Hatuna hofu na Maulid Mtulia(CUF) kuhamia CCM, tupo imara tunasubiri kutangazwa siku ya Uchaguzi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,456
2,000
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Jimbo la Kinondoni kinatoa ufafanuzi juu hali ya kisiasa.
IMG_20171206_110951.jpg


=======

UPDATES
Mwenyekiti wa Chadema (W) Kinondon Waziri Muhunzi amesema aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni Said Mtulia ameusaliti Ukawa, Chadema pamoja na wananchi hivyo asubiri mshara wa usaliti.
=> CHADEMA yasema dhambi ya usaliti itamtafuna hapahapa duniani aliyekua Mbunge Kinondoni (CUF) Maulid Mtulia. Yasema watu waliumia na kupoteza maisha kwa ajili yake. Yaonya kuwa hata CCM watavuna dhambi hii kwa kununua wanasiasa.

=> CHADEMA yasema Prof. Ibrahimu Lipumba ametumwa kutenganisha UKAWA, na hatuko tayari kuona mfuasi wa Lipumba anasimama kugombea nafasi ya Ubunge
Katibu Mwenezi CHADEMA (W) Kinondoni George Mwingila amesema sababu alizozitoa Mtulia kujivua ubunge hazina msingi kwani UKAWA hawakuwa na ajenda ya kubomolea watu nyumba wala kununua wanachama

======

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Kinondoni kimesema hawana hofu juu ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Maulid Mtulia kuhamia CCM kwani wako imara na kusubiri taratibu za kutangazwa siku ya uchaguzi ili waweze kutetea kiti hicho.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano na mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Kinondoni, Waziri Muhunzi alipokuwa akituma salamu kwa wananchi wa eneo hilo kuwataka kuwa wavumilivu.

"Wananchi wa Jimbo la Kinondoni wako salama kwani Mtulia hakuondoka na wanachama hivyo tuko vizuri na hatujasambaratika kama ilivyodaiwa hapo awali," amesema Muhunzi.

Amesema mbunge wa jimbo hili bado ataendelea kutoka Ukawa licha ya usaliti aliyoufanya Mtulia ili hali Chadema ilipigania kila hatua kuhakikisha amepata nafasi hiyo katika uchaguzi wa 2015.

"CCM hawako salama wasifikiri kumchukua Mtulia wamemaliza Wilaya ya Kinondoni, wanachama wapo na wataendelea kuwepo ndani ya Chadema," amesema.

Kwa upande wake katibu mwenezi Wilaya ya Kinondoni, George Mwingura amesema tangu kuondoka kwa Mtulia hakuna mwanachama aliyetoka kufuatana naye.

Chanzo: Mwananchi
 

Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
13,888
2,000
Vyuma vimekaza kila upande. Naona akina Lema wamepiga ramli weee wamechoka. Wakati vyama vya wazungu vinaunganishwa na itikadi wao wote wanajua kwamba wameunganishwa na maslahi. Lipo wazi sana. Hivyo mtu anawahi penye maslahi zaidi, kwani kwachumwani?
CCM wameunganishwa na nini?
 

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
29,770
2,000
[HASHTAG]#LIVE[/HASHTAG] | Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Jimbo la Kinondoni kinatoa ufafanuzi juu hali ya kisiasa
View attachment 645192
=======UPDATES
YouTube
CHADEMA yasema dhambi ya usaliti itamtafuna hapahapa duniani aliyekua Mbunge Kinondoni (CUF) Maulid Mtulia. Yasema watu waliumia na kupoteza maisha kwa ajili yake. Yaonya kuwa hata CCM watavuna dhambi hii kwa kununua wanasiasa.
Kwa hiyo wameitisha press kuongea kuhusu mbunge wa CUF, Dah!
I feel sorry kwa hiki chama.
 

Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,597
2,000
mbona mbowe aliisaliti chadema kwa kula matapishi yake mwenyew... kuhubiri ufisadi wa lowasa nchi nzima, baadaye kampokea cdm huyo fisadi. acheni kuhadaa wananchi..
 

Mkwaruu

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
2,942
2,000
Chadema imekufa
Kina kufa vipi wakati ndo Mabingwa wa usajili bila usajili wao sisi hatuwezi kupata wachezaji. Ndo maana tunajisifia kuwasajili kutoka kwao lakini kuna wengine wanakuja kwa ajili ya kutafuna mafaili
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom