Uchaguzi 2020 CHADEMA kinavyozidi kupoteza kura, kimekuwa kikiwaponda wasanii wanaoburudisha kampeni za CCM wakati ni wapiga kura

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,903
Kushinda uchaguzi ni moja na kuwavuta kwako watu wengi wezekanavyo ili wawe upande wako wao na familia zao wakupe kura.

CHADEMA tumeiona ikiponda kuanzia Askari, wafanyakazi wa tume, viongozi wa dini, wenye magari wanaobeba wana CCM kwenda mikutanoni nk hao wote ni wapiga kura ambao CHADEMA inawaponda.

Lakini siku za karibuni wamekuja na gia ingine ya kuwaponda wasanii maarufu ambao wana ushawishi mkubwa mno kwa wapenzi wa kazi zao ambao wanazunguka na kufanya kampeni mikutano ya CCM.

CHADEMA wamekuwa wakiwaponda wakati hao ni wapiga kura. Badala ya ku win their hearts wawapigie kura wao wanaponda.

CHADEMA ukweli hawakujiandaa kugombea uraisi ikitakiwa mapema kabisa waanze ku-win hearts za makundi mbalimbali kwenye jamii yenye mvuto kwa jamii na yenye makundi makubwa na ushawishi yakiwemo wasanii, viongozi wa dini kubwa kubwa no lakini wapi.

Political strategy yao ya ku-win viongozi wa makundi ilistawi wakati wa Slaa na Lowassa tu hawa waliobaki hamna kitu yaani wanategemea tu kuokota kura za wapita njia mabarabarani.

Swala la ku win hearts of groups kwao halipo halafu wanategemea kushinda uraisi na ubunge na udiwani!

Kuponda wasanii ni kupoteza kura zao ndio maana CCM hata kwenye Ilani ya CCM tuna ilani ya kuwawezesha wasanii na kukuza usanii ipo kwenye ilani kabisa tofauti na vyama vingine ikiwemo CHADEMA ndio maana wasanii wanaipenda CCM inawajali kuwaheshimu na kwenye ilani na sera wasanii wamepewa nafasi.
 
Tunawaelimisha wanachama wa Chadema waelewe chama chao kikishindwa uchaguzi waanze kujua sababu mapema jua linawaka
Yaani wewe!! Kwahiyo kwenye kampeni za CCM badala mtoe sera za namna ya kuinua kipato cha mtu hasa vijana, nyie mnatoa burudani. Basi iteni free fiesta.
 
Tunawaelimisha wanachama wa Chadema waelewe chama chao kikishindwa uchaguzi waanze kujua sababu mapema jua linawaka

Badala utete hoja na sera za chama chako. Wewe unaangalia CHADEMA wamefanya nini na wanasemaje.

CCM propaganda zimewashinda. Polepole jukumu la uenezi limemshinda na vijana wake mmeshapoteana hamjui nini cha kufanya.
 
Yaani wewe!! Kwahiyo kwenye kampeni za CCM badala mtoe sera za namna ya kuinua kipato cha mtu hasa vijana, nyie mnatoa burudani. Basi iteni free fiesta.
Vyote vinafanywa huoni kwenye mikutano burudani kibao na sera zinamwagwa.Tunaanza na burudani Halafu tunamwaga sera Halafu tukimaliza sera tunamwaga burudani watu waburudike na sera.

Burudani na sera bega kwa bega
 
Tunawaelimisha wanachama wa Chadema waelewe chama chao kikishindwa uchaguzi waanze kujua sababu mapema jua linawaka
Hao wanaoonesha ngono jukwaani endeleeni nao tu matokeo yake mtauaona. Mtanzania gani anayejitambua atashawishiwa kupiga kura kwa kuoneshwa Chupi ya Msanii?
 
Hao wanaoonesha ngono jukwaani endeleeni nao tu matokeo yake mtauaona. Mtanzania gani anayejitambua atashawishiwa kupiga kura kwa kuoneshwa Chupi ya Msanii?
Pambaneni na hali zenu tukutane sanduku la kura October 28.
 
Vyote vinafanywa huoni kwenye mikutano burudani kibao na sera zinamwagwa.Tunaanza na burudani Halafu tunamwaga sera Halafu tukimaliza sera tunamwaga burudani watu waburudike na sera.

Burudani na sera bega kwa bega
Kwa hiyo sera zenu ni kwa ajili ya burudani tu kwa wananchi.
 
Pambaneni na hali zenu tukutane sanduku la kura October 28
Bora usubiri tarehe 28 kuliko kusifia NGONO kwenye majukwaa mbele ya watoto. Mmekosa haya chama Kikongwe kuvunja maadili hadharani?

Hayo wanayofanya Wasanii mchana huwa wanayafanya kwenye kumbi usiku tena mbele ya watu wazima, Leo wanaonesha ishara za ngono hadharani mchana kweupe na wapambe mnashangilia? Kwa hiyo unadhani thread yako hii inaiharibia CHADEMA?

Inaonesha hujui kinachoongelewa na watu wenye maadili kuhusu NGONO MAJUKWAANI.
 
Yaani wewe!! Kwahiyo kwenye kampeni za CCM badala mtoe sera za namna ya kuinua kipato cha mtu hasa vijana, nyie mnatoa burudani. Basi iteni free fiesta.
CCM haijaanza jana wala juzi kutumia wasanii.
 
Sijasoma maelezo yako yote kwani naona yamejaa utopolo, kwa kifupi hao wasanii wahuni hatutegemei wakaipigia kura Chadema kwa sababu akili zao tu ni sawa na janga hili CCM na hivyo tunaamini ni wapiga kura wa CCM, wapo wachache kama Roma ambao hawawezi kwenda kuruka ruka ovyo kwenye majukwaa ya CCM, hawa ni wale wachache walioelimika na wanajitambua.
 
Bora usubiri tarehe 28 kuliko kusifia NGONO kwenye majukwaa mbele ya watoto. Mmekosa haya chama Kikongwe kuvunja maadili hadharani? Hayo wanayofanya Wasanii mchana huwa wanayafanya kwenye kumbi usiku tena mbele ya watu wazima, Leo wanaonesha ishara za ngono hadharani mchana kweupe na wapambe mnashangilia? Kwa hiyo unadhani thread yako hii inaiharibia CHADEMA? Inaonesha hujui kinachoongelewa na watu wenye maadili kuhusu NGONO MAJUKWAANI.
Mkuu ccm na wapambe wao hawajawahi kuwa na akili, wanayofanya hao wasanii wahuni ndio ccm inashabikia tena mbele ya watoto kama ulivyosema
 
Kwani hao wasanii wanaburudisha bure? Si wanalipwa? Hao wakilipwa kiwango cha fedha wanazozitaka wanakwenda chama chochote wapo kazini kwa nza huwa hawapigi kura.
 
Back
Top Bottom