Uchaguzi 2020 CHADEMA kiliwekeza kwenye majina ya watu badala ya chama. Maeneo ambayo wabunge wao walijiunga CCM hawana wagombea wa maana

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,904
Chama imara hujenga brand name ya chama siyo majina ya watu. CHADEMA huhangaika sana kujenga majina ya watu badala ya chama. Utasikia ohh Mbowe, ohh Mdee, ohh Lissu hakuna zaidi ya hao!

Sasa kuna yale maeneo wabunge wa CHADEMA waliohamia CCM kuna ombwe kubwa. Wameweka watu wa ajabu ajabu sababu hawana replacement ya kueleweka sababu hawakuwekeza kwenye brand name ya chama zaidi waliwekeza kwenye personal name promotion. Wakihimiza zaidi watu kuchagua mtu na sio chama!

Wana CHADEMA wamejengwa zaidi kupenda mtu na sio chama zaidi hii inaenda igharimu CHADEMA uchaguzi mkuu
 
Jamani mbona mna vichwa vigumu kama mawe?

CCM ndio imewekekeza kila kitu kwa jina la Magufuli!
 
Hao waliohamia CCM pia walikuwa watu wa ajabuajabu na chama kikiwabeba. Wewe ulikuwa unamjua Mwambe kabla ya 2015,ulikuwa unamjua Lijualikali ama Mollel? Huku kwetu sijui ccm watajinadi kwa lipi maana kama ni ndege hatuna barabara ya kufika airport, kama ni flyover iko DSM haina maana kwetu, kama ni watu kutumbuliwa hela walizokuwa wanafisadi hatujapewa sisi.
Mbeleko wanayoitumia ni Magufuli lakini na yenyewe inaelekea kuchanika.
 
Hakuna kitu kinaotwa chama,chama =watu.Sasa ulitaka wawekeze kwenye chama unataka wasiwekeze kwenye watu hizi Ni akili kweli?hao viongozi wangewapata wapi?kwa mfano chief Kalumuna vs Lwakatare aliyeondoka Bukoba kawaulize wanabukoba wanamjua Kalumuna Ni Nani.
 
Umeandika umbea na udaku tu. Walioshindwa kura za maoni wameadhibiwa na ccm walionyomwa fursa na mwenye kiti wenu
 
Back
Top Bottom