CHADEMA kila siku mnakosea target, Siasa zenu hazivutii tena

Lakasa chika7

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
320
1,000
Wabunge zaidi ya 80% wa CCM hawakupatikana kwa njia halali. Kwanini nguvu msiiweke kuwandoa hao wana ccm waliopatikana kwa mtutu.

Hayo hamfatilii mnapambana na wabunge 19 tena waliokuwa makamanda wenu. Nani aijui kazi ya mdee, matiko na bulaya. Hivi na wewe Mwalimu (naibu Zanzibar) unataka kumtosa mzazi mchumba wako matiko.

Chadema kila siku mnamiss target. Siasa zenu hazivutii tena.
Kuna mambo ya msingi ya kufatilia now!
1. Mama samia kaunda kamati ya kufatilia BoT matumizi ya February hadi March, kazi yenu ni kumpressurize aitoe hiyo ripoti!
2. Hamna msimamo wa pamoja, lisu anaongea hivi, katibu anaongea hivi.
Chadema lazma muwe na strong institution badala ya majina

3. Achaneni na wabunge wenu hao 19 cha msingi wapeni ushirikiano.
4. Mnyika na Lisu nyie ni wanasiasa Wazuri jitahidini kukua kiungozi.
Kiongozi mzuri siyo kuwa fixed ni kuwa flexible kuendana na hali halisi.

Mfano kama Godbless Lema angetangazwa kushinda ubunge angegomea kwenda bungeni kisa wengine mmechakachuliwa.

Acheni cheap siasa kipindi cha kumkabili mama. Acheni siasa nyepesi. Tumieni nguvu kujijenga na kuinua morali ya makamanda nchi nzima.
 

ANKOJEI

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
962
1,000
Kwani wewe hu\pendi mama apite 100% mwaka 2025, mbona unataka kumharibia wakati Mbowe & co wamekubali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom