CHADEMA kiko tayari kushika dola,ila kinahitaji...

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
1,820
2,000
Habari wadau;
Niwasalimu wote jioni hii murua
Kama kicha kinavyosema,kwa mujibu wa utafiti uliofanywa,Chama cha Chadema kiko tayari kukamata dola kwa sasa na kwamba kuna mambo madogo madogo yakufanya ili kiweze kuwa kamili;

Baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo:
  1. Chama kibadilike kutoa chama cha harakati mpaka kuwa chama cha mkakati yaani kinacholenga matokeo.Kwa kufanya hivi mtandao wa chama uliosamba nchi nzima utaweza kuwa chachu ya mabadiliko ya kweli na kuandaa wanachama na wanachi kwa ujumla juu ya kutawaliwa na chama pinzani
  2. Uongozi wa chama uache malamiko na lawama na badala yake wajikite zaidi katika kukijenga chama internally kwa kujenga nidhamu,ubunifu,uwajibikaji na uzalendo ndani ya chama huku nje ya chama tukiepuka kabisa controversial issues ambazo kimsingi hazikijengi chama
  3. Uongozi wa chama ujipambanue kifalsafa na ikiwezekana kabisa kila kiongozi wa chama atoe personal manifesto ambayo itakuwa ni andiko linaloelezea kwa ufupi historia yake maono yake na changamoto ila kuweza kurudisha mvuto,touch na wanachama vijana
  4. Viongozi wakuu wa chama waepuka kutumika na vyama vingine kudhoofisha chama,na chama kiwe na intelijensia makini kabisa katika kuhakikisha kuwa mambo kama hayo hayajitokezi ndani ya chama
Chadema kama chama ambacho kimewiva na tayari kushika dola kinatakiwa kuwa chama cha kimkakati kwani harakati za ujenzi wa chama tayari zimezaa matunda na wote walioshirika katika harakati wanahitaji mkakati utakaowaonyesha kuwa chama kiko tayari kushika dola

Hoja yangu inaweza kukosolewa,mjadala uko wazi

PBK
 

Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,401
2,000
tangu lini akili ndogo ikaongoza akili kubwa then utegemee matokeo mazuri. DJ kazi yake ni mziki na madili Hana habari ya kuingiza CDM ikulu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom