CHADEMA Kidedea, Diwani wa Kijitonyanya Ulole Ashinda Kesi, Arudishiwa Udiwani

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
550
Hatimaye CHADEMA imeendelea kuitesa CCM mahakamani baada ya Diwani Ulole wa kijitonyama aliyekuwa amevuliwa udiwani kushinda kesi mahakama kuu na kurudishiwa udiwani wake. Jaji Wambura alisema hakuona sababu za msingi za kumvua udiwani maana defects zilizokuwepo hazikuathiri matokeo. Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Imetulia ahsante kwa taarifa; tunasubiri uamuzi wa mahakama naye Matata arudishiwe uanachama CDM.
 
Safi sana, magamba ni kuendelea kuwatesa hadi kieleweke! Chadema ina vichwa hatari sana vya sheria, chezea chadema weye!
 
Hatimaye Chadema imeendelea kuitesa CCM mahakamani baada ya Diwani Ulole wa kijitonyama aliyekuwa amevuliwa udiwani kushinda kesi mahakama kuu na kurudishiwa udiwani wake. Jaji Wambura alisema hakuona sababu za msingi za kumvua udiwani maana defects zilizokuwepo hazikuathiri matokeo. Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Mkuu hebu eleza vizuri, alikuwa amevuliwa udiwani! Na nani na kwa sababu gani? Maana kwetu wengine hatujawahi hata kusikia kwamba Mh. Ulole Athuman alikuwa amevuliwa udiwani. Na huyu kamanda Ulole ndiye alimbwaga Abdallah Bulembo ambaye sasa ndo Mwenyekiti wa Wazazi huko Magamba.
 
Nia yao imetimia, kwani ilikua ni kumsimamisha kwa muda, ili asitekeleze ahadi, mwisho wa siku hakuna maendeleo yeyote, na kata kurudi CCM.
 
Wakuu.Siku ya leo ilikuwa siku ya Hukumu katika mahakama ya Rufaa juu ya Diwani wa Kata ya kijitonyama na mgombea udiwani wa ccm 2010 mahakama imemrudishia Udiwani bwana Athuma juma Ulole ulole, Mahakama imesema Ulole ulole Alishinda kihalali kwa maana hiyo inamtangza kuwa Diwani wa kata ya kijitonyama mpaka 2015. Tutashinda mengi
 
Mtu anaporudishiwa haki yake aliyoporwa kwa dhuluma huko tunakuita kushinda au tutafute msamiati mwingine,manake watu wanaporwa haki zao mchana kweupe wakirudishiwa tunaita kushinda sielewi mimi
 
Wakuu.Siku ya leo ilikuwa siku ya Hukumu katika mahakama ya Rufaa juu ya Diwani wa Kata ya kijitonyama na mgombea udiwani wa ccm 2010 mahakama imemrudishia Udiwani bwana Athuma juma Ulole ulole, Mahakama imesema Ulole ulole Alishinda kihalali kwa maana hiyo inamtangza kuwa Diwani wa kata ya kijitonyama mpaka 2015. Tutashinda mengi
Mbona kwenye habari kama hizi huwa siwaoni Ritz, Chama, Mafilili na wapuuzi wengine wa Magamba?
 
ccm walienda kumpinga mahakani eti majina yake yanatofautiana. kwenye fomu ya uchaguzi iliandikwa uloleulole juma athuman na kwenye tamko la sheria aliandika juma athumani uloleulole. kwa kosa hilo ccm wakaiomba mahakama itengue udiwani wake. kumbuka huyu diwani japo kesi yake ilikua mahakamani lakini aliweza kuzuia kujengwa na kubomoa ukuta wa nyumba ya spika wa bunge anna makinda uliokua ukiziba mtaa unao unganisha kinyama na sinza. sasa hivi twapita kwa raha zetu. thenkyu diwani. mia
 
Magamba chaliiiiii, safi sana
 
Mkuu hebu eleza vizuri, alikuwa amevuliwa udiwani! Na nani na kwa sababu gani? Maana kwetu wengine hatujawahi hata kusikia kwamba Mh. Ulole Athuman alikuwa amevuliwa udiwani. Na huyu kamanda Ulole ndiye alimbwaga Abdallah Bulembo ambaye sasa ndo Mwenyekiti wa Wazazi huko Magamba.
Na hapa ndio pa kuanzia, mimi ni mkazi wa Kijitonyama, Ali Maua so story yote naijua.
Bwana Bulembo alikwishakubali kua ameshindwa na Juma Ulole hata kabla matokeo ya Uchaguzi mkuu hayajatoka. Hata akili ya kukata rufaa haikuwepo kabisa kichwani mwake.

Tabu ilianza pale alipopata wazo la Kugombea Wazazi-Taifa kwa CCM. Wapambe wake walimfuata na kumshauri aachane wazo la kugombea Wazazi-Taifa maana kama hakubaliki kwenye kata, basi Taifa itakua ni ndoto kupata.

Ndipo jamaa alipoamua kuiweka kata ya Kijitonyama "pending" bila diwani ili apate cha kujitetea kua hakushindwa kihalali. Hata kesi yenyewe hakujishughulisha nayo sana kwani alijua hawezi kushinda.

Mara kwa mara wana-Kijitonyama wamejaribu kumbana na kumsema kwa kitendo chake cha kuwaweka bila diwani kwa maslahi yake binafsi na amekua akiona haya na aibu. Anafahamu kua janja yake imejulikana, hivyo kwa aibu hata safari za huku Kijitonyama zimekua adimu.

Kuna tetesi kua hata jina Bulembo Abdallah kaliomba kwa aliekua Mtangazaji wa BBC Bw. Abdallah Majura Bulembo ili aweze kulitumia kwani yeye alifeli masomo yake.
 
Ahsante kwa Maelezo SAHIHI.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom