CHADEMA:Kesi ya kupinga uchaguzi wa wabunge wa Africa mashariki kutajwa leo.

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
258
Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa bunge la Africa mashariki itatajwa leo kwa mara ya kwenza mahakama kuu kanda ya Dodoma.Kesi hiyo ilifunguliwa na Anthon Komu aliyekuwa akigombea kupitia CHADEMA.Hii imetokea kutokana na uchaguzi huo kukiuka kanuni na utaratibu.Naomba kuwasilisha.
 
kwanini hakufungua katika mahakama ya afrika ya mashariki kama walivyofanya waUganda?
 
Mgogoro kama huu ulikuwepo pia Kenya baada ya kufanyiwa mizengwe ODM. wakafungua kesi mahakama ya Afrika Mashariki ikatengua wabunge wa Kenya na kuitishwa upya uchaguzi kwa mjibu wa uwiano wa wabunge kutoka vyama vya siasa, kama chater iliyoanzisha jumuiya inavyosema. Hivi Tundu Lissu ameshindwa kumshauri Komu hadi kupeleka hii kesi kwenye mahakama za Bongo ambazo ziko mfukoni mwa Ikulu.

CDM mbona hamuonesho umakini katika masuala nyeti kama haya kama wenzenu wa Kenya! Nendani kwenye mahakama ya Afrika mashariki please achaneni na mahakama za Bongo
 
Hapa kuna walakini, vinginevyo kamanda Lissu atujuze sababu za kitaalam zilizopelekea Komu kuamua kufungua kesi hiyo Mahakama ya Dodoma badala ya Mahakama ya A. mashariki. Tujuzwe jamani tusije kuwa na mawazo yasiyozingatia taaluma....
 
Mgogoro kama huu ulikuwepo pia Kenya baada ya kufanyiwa mizengwe ODM. wakafungua kesi mahakama ya Afrika Mashariki ikatengua wabunge wa Kenya na kuitishwa upya uchaguzi kwa mjibu wa uwiano wa wabunge kutoka vyama vya siasa, kama chater iliyoanzisha jumuiya inavyosema. Hivi Tundu Lissu ameshindwa kumshauri Komu hadi kupeleka hii kesi kwenye mahakama za Bongo ambazo ziko mfukoni mwa Ikulu.

CDM mbona hamuonesho umakini katika masuala nyeti kama haya kama wenzenu wa Kenya! Nendani kwenye mahakama ya Afrika mashariki please achaneni na mahakama za Bongo

wadau JF,
nadhani kisheria inabidi kesi hii ianzie high court ya nchi husika na endapo itaamua tofauti basi rufaa itakatwa hadi mahakama ya eac.
 
Back
Top Bottom