kingadvisor
Senior Member
- Dec 21, 2011
- 109
- 30
Tutatoa tamko Rasmi la Chama kanda hii ya Dar es salaam kuhusiana na mgomo huwo na athari zilizojitokeza mpaka sasa.
Nilitegemea vyama vingepigana vikumbo mahospitalini kuongea na madaktari au kuwapa misaada madaktari wasigome na si kusubiri na vikamera na visimu koko vya kunasa sauti vilio vya wagonjwa wasiopata matibabu na kukaa nje ya chumba cha motuary na kuhesabu maiti ngapi zinatoka mawodini kuingia motuary na kwenda kuhutubia kueleza idadi ya waliokufa na wanaogalagala kwa maumivu mawodini .Hekima ya kisiasa inatakiwa.Nchi zingine vyama vingekuwa vinahangaika kujaribu kuepusha mgomo maana wakigoma wafao ni wa kutoka vyama vyote na msiba kwa kila chama na si serikali pekee.Nyongeza za mishahara na marupurupu kwa madaktari wabunge n.k ni kilio kwa mtu wa kawaida sababu yeye ndiye atakiwaye kukamuliwa hiyo kodi ya kugharimia hizo starehe za posho na nyumba nzuri watakazo hao madaktari.Iko siku wananchi watawavamia hawa wadai posho na marupu rupu mazuri bila kujali ni wabunge au madaktari.Kila mtu anadai aongezewe mwalimu anadai,askari anadai,daktari anadai,pesa yote inatoka kwa mlipa kodi ambaye tayari kachoka na mlundikano wa kodi mwisho wa siku kuna siku wagonjwa wataamka vitandani wawalambe makofi kuanzia serikali,vyama na hao wafanyakazi wawe madaktari au nani kwa kutumia matatizo yao kujinufaisha kisiasa na ki-kuongezeana mapato kutokana na kodi zao wagonjwa.