Chadema: Kazi bado ni kubwa acheni hoja ya mgombea urais! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema: Kazi bado ni kubwa acheni hoja ya mgombea urais!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyami2010, Oct 21, 2012.

 1. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  WanaJF

  Kwa namna upepo wa siasa unavyovuma ndani ya CCM, haina shaka tena EL ndiye atakuwa mgombea Urais kupitia CCM. Kwenye chaguzi za CCM zinazoendelea, EL amefanikiwa kwa 95% kuweka timu sawasawa. Karibia nchi nzima, wajumbe wote wa NEC ni watu wa mtandao wa EL na ndivyo itakavyokuwa kwa CC. Mkutano Mkuu wa Taifa - CCM ni Rubber Stamp tu!


  CHADEMA, EL kuwa mgombea wa CCM ni opportunity ya pekee toka kwa Mungu ya kuichukua nchi 2015, msikosee! Kaeni chini muwe na mkakati wa kujipanga kuanzia ngazi ya chini kabisa hususani kwenye vitongoji na muanze kutoa elimu kwa wapiga kura na namna ya kulinda kura.

  Wapendwa, kwa hakika CCM ni imara sana ngazi za vitongoji hususani mikoani. Watu wa kawaida wanahitaji hamasa na elimu ya kutosha juu ya uchafu wa CCM na kwa nani CHADEMA. Kuanzia sasa elekezeni nguvu yenu kwa wapiga kura ngazi za chini. Kwa Mijini, mashuleni, vyuoni na makazini watu walishaelimika wanasubiri ifike 2015.

  Ombi langu, CHADEMA kwa sasa acheni kulumbana juu ya nani awe mgombea wa Urais maana kazi bado ndo inaanza. Huu ni ushauri tu, naomba kutoa hoja!
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,018
  Likes Received: 3,612
  Trophy Points: 280
  Tulio na mapenzi mema na nchi yetu na DCM tumelikemea sana hili hasa huyu mtoto mtukutu Zito. Ona EL hajatamka wazi kuwa ana nia ya kugombea urais, bali anajipanga kwanza, Mtoto mtukut Zito linaleta mgawanyiko!
   
Loading...