Chadema: Kaza buti haya maandamano yana tija | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema: Kaza buti haya maandamano yana tija

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbayuwayu2008, May 16, 2011.

 1. M

  Mbayuwayu2008 Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba kutumia nafasi hii, kuwasihini wapiganaji wote wa CHADEMA kuwa wasidhani kuwa kukubalika kwa CHADEMA kwa Watanzania wote (makundi na rika zote) ni jambo rahisi. Wazidi kujitangaza kwa njia hii ya maandamano. Japo, kwa wapinga maendeleo watadhani ni kupoteza muda bali mimi naamini ktk hili.

  Watanzani wengi waliopembezoni mwa Tz hawajui kama kuna chama zaidi ya kiki chama cha magamba (ccm).
  Chadema ktk vita hii tujihakikishie kuwa umma wa Watz unakuwa na imani kubwa kuwa CHADEMA si chama cha siasa tu bali ni mkombozi ktk kujitafutia maendeleo yao.

  Watanzania ktk makundi yafuatayo wanaiamini Chadema kwa vyati kabisa:
  (1) Wasomi wengi (Vijana kwa Wazee)
  (2) Vijana wa kitanzania (Wake kwa Kiume)
  Jukumu letu sote ni kuhakikisha kuwa akina mama ambao hasa wanadanganyika na vijizawadi vya ccm wanaelimishwa kuhusu mustakabali wa maisha yao. Pia ziara/ maandamano yaelekezwe zaidi pembezoni mwa Tz, kuwafahamisha wananchi juu ya dhamira za Chadema. Watz wanapenda maendeleo ni kuwa hawana matumaini kwa kuwa ccm imewahadaa.

  Nina imani kubwa ktk chaguzi zijazo hasa za serikali za mitaa (2014), CHADEMA itaibuka kidedea kwa kupata viti vingi. Hiki ni kipimo tosha cha kushinda uchaguzi mkuu 2015. Nina mfano wa kijiji changu (Kwermusl) ambacho serikali yote ya kijiji (isipokuwa m/kiti ccm) ni Chadema. Na huyu m/kiti waliamua kumchagua kwa sababu tu ni mtu anayekubalika ktk jamii ile lkn mawazo anayotekeleza ni yale yanayoamuliwa na Wanachadema.

  Ni jambo jema pia kwa Chadema kufanyia kazi mawazo mema ya Wanajf kama kuwa na TV n.k ya Chadema na kuhakikisha kuwa inafika sehemu kubwa ya nchi hii. Hii itarahisisha Chadema kufahamika zaidi na kukubalika kwa Watz wote.

  Mungu ibariki Tanzania.
  Mungu ibariki Chadema.
  Mungu uwabariki na wapiganaji wake wa haki na maendeleo. Amen
   
 2. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na mawazo yako mkuu. Naamini kwa dhati kuwa Chadema wanayafanyia kazi mawazo yote mema ya wanajf, ambao wanatumia muda wao kuwapa mbinu nyingi. Na hasa ile yakumpendekeza Dr Slaa kugombea pia lilikuwa wazo la Wanajf. Hakika wanajf wanafikiria mbali sana.
  Cheers wanajf.
   
Loading...