Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Siku ya Jumanne Novemba 13, 2018 Diwani wa Kata ya Kindi Kati na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi Vijijini Mhe.Michael Kilawila kwa ushirikiano wa Marafiki zake kutoka Ujerumani wakiongozwa na Sebastian Schneider, walitoa misaada ya IPad 20 pamoja na Chaja 5 za nishati ya jua katika Shule ya Sekondari ya Kindi Kati.
Lengo la mradi huo ni kuwasaidia Wanafunzi na Walimu wa shule hiyo kuingia kwenye ulimwengu wa teknolojia.
IPad hizo zina programu mbalimbali za kujifunzia nje ya mtandao(offline).
Hata hivyo Mhe.Kilawila pamoja na marafiki zake hao wana mipango mingi na mikubwa na sehemu ya mipango hiyo ni kuwa na Maabara ya Kompyuta ya kisasa (Computer Lab), pia wanatarajia Waalimu wawe wanaandaa mitihani ya kila wiki hivyo kuwafanya wanafunzi kuwa na majaribio mbalimbali.
Jumatano Novemba 21, 2018 mmoja wa wafadhili ataenda kutoa mafunzo ya matumizi ya Ipads zilizokabidhiwa shuleni hapo.
Jamii ya Kata ya Kindi Kati Sekondari wameshukuru sana kwa msaada huo, Wanafunzi na Waalimu wameahidi kuzitunza na kuzitumia IPad hizo kwa uangalifu mkubwa na kwa malengo yaliyokusudiwa.