Chadema kama mnataka kushinda ubunge Arumeru mtumieni John Shibuda

Kweli kama wewe unaona shibuda anahoja na anaweza kuleta ushindi arumeru kwa sababu ana mipasho basi wewe una element ya uzamani uzaman wa kisiasa, ni mpenzi wa siasa za mipasho ambazo hazina nafasi kwa wakati huu tunataka wajenga hoja na watu wabadilike kwa hoja wala sio mipasho kwani watu wakibadilika kwa mipasho akija mwenye mipasho zaidi ya shibuda atachukua jimbo kwa mtazamo wako.
 
huyu chinchila mmemsahau?
huyu hawezi kuishauri chadema wa hana nia nzuri na chadema.
huo ushauri mpelekee nape utamsaidia kueneza.
 
Kunatofauti kubwa kati ya wanachadema wabunge na wabunge kupitia tiketi ya chadema ,sisi wanachadema hatuhitaji sana watu ambao wamepata ubunge kupitia chadema lakini si wanachadema.mpo hapo
 
Political prostitutes hawatakiwi kabisa huko,mwisho atadai posho ya MWIGA
 
.........umetumwa na nani kuleta ushauri huo wa kishetani ? Peleka sisiemu ushauri wako kama nguvu za giza vile...
 
Chadema wametumia busara kubwa kutokumfukuza Shibuda katika chama, maana ingeanzisha migogoro ndani ya chama. Lakini nionavyo kuwepo kwake au kutokuwepo kwake ndani ya chama hakuna tofauti.
Eti awekwe kampeni meneja? Labda awe kampeni maneja wa ccm, maana hadi sasa ndiko ulipo moyo wake.
 
Kwani Magamba Watapeleka Taarabu Arumeru? Kweli Ukisikia WATZ ni watu waliodharauliwa ni kwa Hawa Magamba wanavyo wadharau!! Badala ya Kupeleka sera wanawapelekea The Comedy!! Taarabu!! Hadi Aibu
 
Wakuu JF

Ni ushahuri ninautoa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kama kweli mna dhamira ya dhati ya kushinda ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki. Mtumueni John Shibuda, kuwa mkuu wa kampeni.

Ni mtu makini mwenye huwezo wa kujenga hoja za kuwavuta wapiga kura. Kama mtamuweka pembeni na huu uchaguzi basi mtakuwa mmefanya makosa makubwa.

Ushauri mwingine bana? Kama nguvu za Giza?!!
 
nadhan mleta uzi atakuwa na undugu na huyo shibuda,au katumwa au ndo shibuda mwenyewe,km ww ndo shibuda yan hufai ht kuwa kampen meneja wa kiranja mkuu shulen.
 
Back
Top Bottom