CHADEMA, kama kweli mnapokea misaada kutoka UK, Mtatunusuru vipi na hoja ya USHOGA tukiwapa kura?

Hoja za namna hii hutumiwa na wachovu wasiokuwa na majibu kwa hoja za msingi kama vile ukosefu wa huduma za jamii, kudidimia kiwango cha maisha, mikataba mibovu inayowezesha rasilimali zetu ziwanufaishe wanasiasa na washirika wao huku wengi wakiendelea kutota kwa umasikini
 
Pamoja na shida zote za mwanadamu. Raha pamoja na starehe mbalimbali. Ushoga na ndoa za jinsia moja ni kitu kibaya kinachomchukiza Mungu pia. Inasemekana kuwa chama chetu hiki kikuu cha upinza yaani CHADEMA kinapata misaada mingi kutoka Uingereza. Nchi ambayo kupitia waziri wake mkuu wameweka mashariti kwa nchi za kiafrika zilizo katika jumuiya ya madola iwapo kama zinataka kuendelea kupewa misaada basi zikubali ndoa ya jinsia moja. Sisi watu ambao hatuna itikadi ya vyama huwa tunaangalia maslahi ya nchi zaidi bila ya kujali ni chama gani kitatawala. Kwa hili mmejiandaa vipi kukabiliana nalo iwapo kama tutawapa dhamana ya kushika hatamu za uongozi wa nchi.
ina maana Tz,hakuna ushoga?na kama wapo wamesababishwa na Chadema!kama kweli huna chama,unaongea kwa issue ya kitaifa,kwa nini husemi misaada inayopata Nch toka Uk.umeishupalia Cdm.UNALO LAKO MOYONI!ila c vizuri kukua kichwa pekee!ni ushauri tu.
 
Serikali ya CDM itakuwa sio ya kutembeza bakuli kama hii,yenyewe itatumia rasilimali za nchi kuinua watu wake sio kuwa ombaomba mpaka kulazimishwa misaada ya kejeli.Maneno ya Cameroon yaliistahili CCM pekee maana hata rais wao alijisifu kuwa anatembea sana ili kupata misaada
 
ina maana Tz,hakuna ushoga?na kama wapo wamesababishwa na Chadema!kama kweli huna chama,unaongea kwa issue ya kitaifa,kwa nini husemi misaada inayopata Nch toka Uk.umeishupalia Cdm.UNALO LAKO MOYONI!ila c vizuri kukua kichwa pekee!ni ushauri tu.

Nikiitaja chadema napata faida kubwa sana kutoka maneno ya wachangia mada, we hujui tu!
 
We kweli nduza uliyekurupukia mada, swali limeulizwa kwa chadema huko unaenda wapi. Tayari vyupa vinasumbua si ulale. Haya ndo matatizo ya kulewa bila kula.
Mleta mada huwa anamtindio wa ubongo, akijitahidi kuwaza sana basi huja na majibu kama haya, halafu hujisifu ati na yeye ni Great Thinker! kweli dunia haiishiwi maajabu.
 
Back
Top Bottom