CHADEMA kama honeybadger kwa nyoka, na machine za catapiller kwa mlima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kama honeybadger kwa nyoka, na machine za catapiller kwa mlima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicholas, Sep 7, 2012.

 1. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Sikushangaa sana kumsikia mheshimiwa mzee 6 akionyesha jinsi gani haijui CHADEMA wala wanyama wadogo lakini hatari sana.Huku kunaweza onyesha jinsi si yeye tuu ila CCM nzima wasivyoijua CHADEMA.

  Hawajajifunza hata kwa kuona wabunge wake ni wadogo sana kimaumbile na kiumri ila hawana hofu ya ku-take on anybody in the CCM and the government. Mnyika kasimama ni kusema yote alioona wazi hayafai kuhusu rais mbele ya bunge lote, kasimama na mwanasheria mkuu bungeni na bado ana nguvu za kufanya kwa yeyote, Lema kasimama hivyo hivyo , Msigwa alisimama na kuongea kwa staili iliyonanyamazisha bunge lote la "..Ndioo na zomezomea.."kwa ujumla alinyamazisha bunge hadi akamaliza kuongea na likawa tulivu kila CHADEMA walipoongea na list inaendelea hivyo hivyo hadi kwa wabunge wasiosikika.Sidhani kama CCM walijifunza sana

  Mzee aliona safu yao ndogo kaipuuza na kuiita nyembamba..hakujua wana mziki mkubwa kama "honey badger", wanamtafuna nyoka (nikibandika CCM hapa) bila kumua tena wakianzia mkiani.Na hawamzui kujitetea kwa kung`ata au kutema mate.Mabaharia wanajua kwanini vile vi boat vidogo vitumikavyo kuvuta meli kubwa ktk maeneo ya bandari vinaitwa "Badger".


  Nadhani utajua ni kwanini ile task (CUF/NCCR) walishindwa CHADEMA wameweza kama vile caterpillar inavyokata kifusi.Katika misimamo wakishagoma wamegoma,patachimbika, na wakiamua chimbua wanachimbua kama catapillar.

  Hizo ni coinsidence tuu ambazo waswahili wanaziita bahati.Ila ni bahati zimkutazo mwajibikaji.Kwani kila kitu sahihi hulengana nacho kwa muda sahihi,kama ulikuwa katika uwajibikaji.Kwa mwajibikaji hakuna njaa.

  Its no coincidence watu wa kupenda makundi na ubaguzi hawajaweza tafsiri tabia za CHADEMA.Ila kuwashangaza zaidi napawa somo tuu...katika dialects za wachaga.Tafsrisi yake inahama kati ya "Cha/kya/sha/kya dema .cha ghema" nimegoma/amegoma na Kimelima(kuchiba kwa jembe) au tuwaite "caterpillar".

  Kuonyesha jinsi gani CHADEMA ni kama honey badger,wapo active sana. CHADEMA wapo active mwaka mzima.Honey badger si mvivu na kuamka kwake ni kufungua macho na kuondoka.Haogopi simba wala chui, wala nyoka.Ni mshapu na ana makeke ya kweli.Yupo illusive, wanyama wakubwa wakimshika ili wamue ngozi yake imepwaya na hivyo kufanya iwe ngumu kwa mnyama mkubwa kumshika sehemu hatari, na mara washikapo sehemu ya ngozi bado kinabaki na nafasi ya kupambana hadi hata ua mnyama adui na kuondoka.Yaani ngozi hujivuta kama vile defender avutavyo jezi ya forward ya polyster katika mpira.

  Nadhani sasa wengi wataelewa kwanini CCM watang`ata sana,watarusha sumu sana ila wataliwa kama nyoka aliwavyo kuanzia mkiani hadi kichwa kifikiwe.

  CCM wanaweza jitetea kuwa si dhaifu ila CHADEMA wanawafanya waonekane kuwa dhaifu.
   
 2. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Operation ya Chadema kusini iliamsha hofu kubwa si tuu kwa wabunge bali hata mawaziri wa CCM.Wabunge wa ccm walilia kwa uchungu bungeni kama vile walichungulia jehanam ya kisiasa na kurudi.Ingawa karibu CCM wote wanaamini kuwa CDM ina safu nyembamba na ina Nguvu Kaskazini tuu.Inaonyesha bado hawajaona nguvu za hawa jamaa,ni kama timu ikicheza na Agentina halafu ikaja na fikra kuwa Messi si hatari akiwa timu ya Taifa, na kwa wachezaji wenye miili mikubwa wakisimama naye humuona km katoto na habari wazisikiazo huona kuwa ni uongo tuu.Ila mahali fulani ktk mechi akipata mpira wapinzani hujisikia wanyonge mbele ya Messi huanza kupaniki na kuzidi kuwa wanyonge.Hawajaona kuwa CDM kwa Mbeya ina Nguvu kuliko hata Kilimanjaro.Hata rais naye hakuogopa kuiweka CDM katika list ya vyama vya msimu.CDM hawakuogopa mwambia rais nchi haitotawalika, sasa tunaona jinsi ccm wanavyohangaika.Rais aliwahi sema pengine bila kutambua sana,kuwa CDM wanajaribu mpotezea stim za kazi kwa kumletea mambo kibao,ila hawataweza ng`o,wao mwendo mdundo.Kwa wana ccm waliomsikia Lema kwa mbali kupitia CCM hulia kilio kikuu akifika majimboni mwao.Hao ndio CDM.

  Haya ndio mambo ambayo hunifanya nisvunje ahadi yangu kwa watoto.Yaani kama nimewaahidi watoto wangu kuwa wakikosea tena nitawachapa, na wakifanya hilo kosa tena ,wasipokiri na kuomba msahama,lazima niwachape.Ninajua nisipofanya hivyo watoto hawataniamini tena si kwenye hilo tuu bali hata ahadi nyingi kama siku nikiwaahidi kitu kizuri iwapo watafikia au kuzidi malengo .Watoto smart watajua mwongo ni mwongo tuu,wengine watajiuliza kama mzazi kashindwa timiza hadi ya adhabu ilisyomgharimu chochote,itakuweje kutoa zawadi inayohitai hela kiasi alichosema?CCM wanajidanganya sana kuwa CDM si tishio linalozidi polisi kwa hiyo wao watakuwa salama sana, sasa imefikia mahali wenyewe kwa wenyewe hawaaminiani.Magufuli pekee ndie alionekana jifunza kwa kutoa hotuba ya wizara yake bungeni huku akijiweka pembeni pasipo kumchokoza "honeybadger", kajitahidi paint picture kuwa hana madhara kwa badger ili badger aendelee na shughuli zake.

  Mheshimiwa 6 alisema kuwa alikuwa akishawishika na CDM kuingia ili kunenepesha safu ya uongozi, na aliwasikiliza sana tuu ila hakuipenda ilani yao(oh no..hakufikia makubaliano-yaani hakukubaliwa naye hakukubali).Mimi sikuitafsiri literally hivyo, mimi nililiangalia CDM kuwa wapo tenacious enough kuwa offensive kwa CCM, wakatumia office za bunge kumrubuni speaker toka chama Tawala, ni ishara tosha wana uwezo wa kuipasua CCM anytime, ni ishara kuwa wanaweza ilima yote na kuondoa udongo na kuipoteza ktk ramani ya siasa.Kwa jeuri kama ya Honeybadger amlavyo nyoka hawaogopi meno,sumu, pembe za CCM (dola), wao wakijisikia kumtafuna CCM wanaanzia popote, mkiani, mgongoni bila hofu.Wanatafuna bunge(kwa hoja na kuwafanya wabunge wa CCM na wengine Useless, wanashambulia hadi speaker (mh Sitta)),wanashambulia katika nguvu za umma, wanakwenda pale CCM wamemwaga sumu kama tarime(CDM kuhusishwa na kifo cha wangwe), arumeru(kauli ya wazee Lema asifike meru), wame face tishio la kufutwa na msajili kama honey badger anavyoumfuata cobra aliyejitunisha huku akipiga kelele, na kurusha sumu, na kuamua kumla cobra kuanzaia mkiani kama vile hajaona kichwa kipo.
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii imesimama lakini haikuonekana Jana watu walikuwa busy na ile thread yenye mtizamo wa kidini
   
 4. m

  mnduoeye Senior Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nicholaus ,umekuwa na maono kama nabii nakusifu sana .CCM kwa sasa wakonjia panda hawaamini chama cha msimu kitawatoa jasho namna hiyo. Imani yao ilikuwa CDM wataonekana tu kipindi cha uchaguzi kumbe wamalamba garasha kwa imani yao hiyo.Wakawahutubia wakiwaaminisha wananchi kuwa hawa wataonekana wakati wa kampeni tu ,na imani hiyo imewatoka waaminishwa na hata hawaogopi tena mabomu ya machozi kwa sababu waliaminishwa uongo.SASA WANATUMIA NGUVU kwani kwa imani hawasogei tena wamebanwa.Monitor wote wamefurukuta wamezidiwa (Nape,Mukama.Mwigulu, 6)sasa wanamtumainia Kiranja mkuu Tendwa,naye jana katendwa kaambiwa ukweli kuwa sasa sio 1947.Sijui kama jana alilala.CCM WAJITAFAKARI NA WACHUKUE HATUA NGUVU ITAWAGHARIMU SANA HONOYBARGE YU KARIBU YAO
   
 5. Man 4 M4C

  Man 4 M4C JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 737
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kamanda mitaani kwenu wanasema "CCM WANALO HILO" imekula kwao. Wao wanaingalia cdm kumbe na wananchi wenyewe wamebadilika wanataka mageuzi.
   
 6. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  thank u kwa msg nzuri but just out of curiosity.....what's a honeybarger dudes?

  Just wanna know
   
 7. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Mojawapo ya jamii yake alitokea katik movie "THE GODS MUST BE CRAZY"

  Labda kwa haraka unaweza check hapa, ila ni vyema ukaangalia Video zake.
  Honey badger - Wikipedia, the free encyclopedia

  Hizi ni quote kutoka kurasa ya wikipedia kama quick reference.:

  Quote "The honey badger has a fairly long body, but is distinctly thick-set and broad across the back. Its skin is remarkably loose, and allows it to turn and twist freely within it.[SUP][11][/SUP] The skin around the neck is 6 millimetres (0.24 in) thick, an adaptation to fighting conspecifics.[SUP][12][/SUP] The head is small and flat, with a short muzzle. The eyes are small, and the ears are little more than ridges on the skin,[SUP][11][/SUP] another possible adaptation to avoiding damage while fighting.[SUP][12][/SUP]"
  [​IMG]

  ".........Honey badgers have even been known to chase away young lions and take their kills. They will eat fruit and vegetables such as berries, roots and bulbs.[SUP][20][/SUP]......."

  "They may hunt frogs and rodents such as gerbils and ground squirrels by digging them out of their burrows. Honey badgers are able to feed on tortoises without difficulty, due to their powerful jaws. They kill and eat snakes, even highly venomous or large ones such as cobras. They have been known to dig up human corpses in India.[SUP][27][/SUP] They devour all parts of their prey, including skin, hair, feathers, flesh and bones, holding their food down with their forepaws.[SUP][28][/SUP] When seeking vegetable food, they lift stones or tear bark from trees.[SUP][20][/SUP]"

  ".......Because of the toughness and looseness of their skin, honey badgers are very difficult to kill with dogs. Their skin is hard to penetrate, and its looseness allows them to twist and turn on their attackers when held. The only safe grip on a honey badger is on the back of the neck. The skin is also tough enough to resist several machete blows. The only sure way of killing them quickly is through a blow to the skull with a club or a shot to the head with a gun, as their skin is almost impervious to arrows and spears.[SUP][29][/SUP]........."  na hii


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Mukama ndio wa kulaumu hapa zaidi ya akina Nape.Yeye ndiye alikuwepo katika kundi liliowalea akina Nape kwa kuwaambia kwa kuwadanganya vitu.Vijana hawakujifunza jinis ya kujua wanyama hatari na kutowapelekea pua.Hata watoto wa simba huifunza mapema kuwa nyoka ni hatari na hawaendi wanusa.This time akina nape na uzoefu wao unaoishia katika report zenye matokeo ambayo CCM imesambaratisha vyama vingine vilivyokuwa vikionekana tishio kuliko CDM.Hawajawahi ona honeybadger...ndio nawatambulisha hapa.
   
 9. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimetoka Arusha>>DAR, Then DAR>>ARUSHA , Namimi nimesikia jinsi watu kwenye bus wasivyo chelewa kuonyesha 'live' kwamba wao ni CDM. Yani mwendo mdundo wa kuiponda serikali mpaka baas; kuhusu kifo cha Mwandishi. Mbaba anaonge hadi mishipa ya kichwa inasimama!
   
 10. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Sikuwa nimefahamu kwanini wabunge na wanachama wa CCM wapo shallow hivyo, na pia wana uelewa tofauti sana, hadi linipo analyse propaganda zao.Nimeangalia pattern yao ya kuamini kitu au hta kua analyse.Nimegundua haya.

  -Kwanza zidumu fikra zamwenyekiti .watu wanaamini mwenyeketi wao na viongozi wengine wanajua kila kitu+ wanaongea ukweli tupu+ na wao ndio wanaruhusiwa panga kila kitu.(kwa hiyo hata kusikiliza habari njeama katika TV kuhusu vyama vingine wao huon akuwa ni uongo, kwa vile ukweli unatoka kwa mwenyekiti.

  -Propaganda za CCM ktk dunia huru hazina pa kuaminika zaidi ya ndani ya CCM kwani ndipo watu wamefungwa kiakili na kujikuta wakimaini kila kitokacho katik chama.Ilimradi waambie ni ilani ya chama.Ndio maana hakuna mwanacc anaifahamu CDM.Na hilo halibadiliki labda mwenyekiti awaambie cdm wamejirekebisha na kutii amri ndipo watakuwa huru kuikubali CDM.Watu huru wanasoma, na kusikiliza habari kwa makini na kuitafakari kwa fikra huru hivyo hujua wapi CCM wamechemsha.

  -CCM wanarudia sana propaganda za voda fasta kiasi ch akufanya hata walioziasha baadaya kuwarudia na kuaminishwa.Yaani waanzilishi wa hizo propaganda, wanapowapa wafuasi wao zikazunguka sana ndani km ilivyo kwa umbea mwingine,halafu zikarudi tena kwa kupiti akwa kada wao ambaye nalisema kama vile kaliona, aliyeanzisha huwa affected naye kuamini kuwa alichofiri ni sahihi.

  -CCM hawana tena source ya right information ,kwani tayari ufisadi unawakorogasana ndani na hivyo kuwaacha wasomi na wanachama wengine kuwa vulnerable kwa habari zisizo sahihi.

  Mwisho wa siku ndio hii CCm iliyojaa watu wenye vichwa corrupted...honeybadger naye anawakoroga na kuwatisha mfululizo
   
 11. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hii thread tamu mpaka imenikosesha ucngizi.
   
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  CCM sasa ndio wanaanza pata pata kafahamu ka uwezo wa "badger". Sasa wanaanza hisi kuwa CDM wanaingia katika roho yao.Kuwa CDM wanabomoa lile bawa la kupiga makada wao, lile bawa linye uwezo wa kuchagua Wagombea urais kupitia CCM.Lile bawa linaloibeba CCM katika nchi.Yaan UVCCM

  Sihitaji kuangalia kama ni kweli ni kweli ama ni hofu tuu..ila nia uhakika halipiti bure, CCM wakiguswa na jani tuu wanajua wanajua ni ndevu za "Badger". Sishangai hili kwani CDM kama waliweza tumia office za Bunge linaloongozwa na Spika wa Chama Tawala na kuweza mchezea kiongozi huyo wa Bunge, ni wazi hao vijana wasio hata na hakika ya kufika popote katika CCM kama makundi wayapigiayo debe yatashindwa, hawatapona. Sasa kama CCM hawaka hakika tena na vijana wao, wala viongozi wao wa juu,mara waisikiapo CDM ikinguruma ni wazi kuwa CCM ni "Nyoka Mjinga".

  Movie inaendelea...Honeybadger doesnt care....who is blocking the way ...the most fearless terrestrial creature in the world.
   
 13. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  sidhani kama ni sahihi kwa CUF kuingia katik vita na CDM kwani tayari hawawezi tena kuwa kambi rasmi ya upinzania bungeni au hata kuwa sehemu ya hilo.sasa hivi walipaswa kusoma upepo wapate faida ya kusimamisha mtu kwa usalama sehemu CDM haina mtu au ina mtu si imara sana.Ila huku kuingia katik vita na hawa jamaa inaweza warusidha katk useless state very quickly.
   
 14. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Baada ya msururu mrefu wa wanaopita anga za CDM vibaya.Sasa njia panda TBC nao wameamua pima maji.Sijui kama TBC wame calculate vizuri risk hapa.TBC ni mojawapo ya TV zilziopoteza mvuto sana mchini.Ni kituo kinacholaumiwa sana na watanzania kwa kukosa mvuto na kuwa na vipindi vya hovyo, na vinavyorudia sana.Watoto wadongo siku hizi wanajua jinsi gani kipindi cha chereko kinavyorudia matukio,wameshika matukio kama watoto wa enzi zile za movie za Rambo.

  Cha kusikitisha ni kwamba hata CDM nao wanahitaji media,na wanahitajia sana ili kuwafikia watu,kujibu hoja, kufuta tuhuma na kupeleka mashambulizi.Ila hapa TBC nao wanahitaji Chadema sana ili wawe valid katik masikio ya wananchi.Na bila masikio ya wananchi TBC itaishia kupoteza umeme tuu kam ailivyo TBC radio.Sikumbuki kama nilishawahi tune hii radio,kwanza kuijua ilitoke abahati mbaya sana ktik gari na ndipo nilipojua kuwa ipo radio inayoitwa TBC.

  TBC inaingia katik vita ikiwa dhaifu sana kama chombo cha propaganda.Tangu kuondoka kwa Tido kwa staili ambayo,hata kama ilikuwa ni mpango mzuri hakukua na matokeo mazuri sana kwa jina la TB.Kuwepo kwa TV nyingine zinazovuta washabiki hata wale wa mpira kama ATN,TBC haijabaki na Kitu,labda wachache wanaoikubuka "ze original comedy'.

  Hapa tayari CDM wanaonekana wazi kuwa watapunguza audience kwa TBC vibaya.Na hii itakuja wanyima CCM platform kabisa,kwani hawawezi tena hata kuanzisha TV nyingine na kuiibua kwa haraka hivyo.Hapa "The Honey badger" ataendelea kula nyoka bila hofu kubwa.Na wanazo silaha nyingi za kuilipua TBC katik uendeshaji, mikataba etc.Hii ni ishara sasa CCM (The Snake) anazidi jiachia akatwe nguvu yake moja.Kwa CCM TBC ni muhimu kuliko vyomvo vyao vya habari vyote.
   
 15. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #15
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,779
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Asubuhi njema! Watalaam wa siasa za vyombo vya habari watatuambia vizuri kama TBC1 ni mali ya Umma kama tulivyodanganywa au ni mali ya CCM. Nijuavyo kama ilivyotokea kwa Sadam Hussein, Muamal Gaddaf, hata Mobutu Sesseko au Idd Amin Dada wote hawa walikuwa na vituo vyao eidha Redio, Magazeti au TV kwa lengo la kuhadaa umma na hivyo kubadilisha UONGO kuwa UKWELI na UKWELI kuwa UONGO, lakini wote hao baada ya tawala zao kuanguka na vyombo vyao vya propaganda wajanja wakagawana kilichopo kuna aliyepata Mixer, Mic, Sender, Booster na kuna aliyeambua Zuria la studio. Ndivyo itakavyokuwa kwa TBC media house siku ambapo wanafamilia watakapo gawana mali za marehemu CCM baada ya mazishi kabla hata ya hitma.....
   
 16. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Kweli mwaka huu CDM watakuwa na muda mzuri sana.najribu fikiria M4C inapata bahati ya kuingia ktk campains nyingine sumbawanga.Sipati picture CCM hoi Kifedha,hoi kimkakati.CDM ndio wanaamka kwa energy.

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/322692-wananchi-wa-sumbawanga-mjini-wanataka-uchaguzi-urudiwe.html

  Najaribu pata picture kama ndio showdown inakuja .CDM watafaidika haswa,kwani m4c inaendelea kwingine halafu wakashushe zahma pale,by the time wanatoka Sumbawanga inakuwa imesimikwa rasmi kuwa territory yao
   
 17. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Uwepo wa topic kama hizi na nyingine nyingi inaonyesha jinsi gani CCM wana hofu juu ya CDM kuliko CDM wanaihofia CCM.CCM si kuwa tuu hawajui matatizo ya Tanzania yameletwa na nini bali hata ya kwao wenyewe hawajui yanafika vipi wala majibu yake ni yapi.

  Kama kweli habari ni kweli ina maana the badger is going for "jugular".Ingawa pia mwandishi kaonekana kuwa so naive katika footer yake.
   
 18. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  CCM kulia kuwa CDM inawachonganisha na wananchi na mambo mengine dhaifu kama hayo. Hiyo habari inanifanya niwaone CCM km mzinzi anayemlilia daktari CDM kuwa Kamchonganisha na Ngono kwa vile kamwambia ana virus visababishavyo ukimwi.:yawn::yawn::yawn::yawn:
   
 19. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Tmko la CDM juu ya kutomheshimu Tendwa huku wakisisistiza kuwa wataheshimu sheria kunamfanya Tendwa kuwa useless na mara nyingi kila atakachojaribu kifanya ni lazima atumie nguvu kuwashawishi watu kuwa anafanya kitu sahihi.Kesha jiingiza kwa honey badger.

  Sasa vurugu za mwandishi mwingine wa Channel 10,ni uzito mwingine kwa Tendwa, kwani sasa waliofanya ni vijana wa CCM na si polisi,Polisi nao hawajapona kwani nao habari za kuuwa mtoto ni mbaya kwao.
  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/324646-mwandishi-mwingine-wa-channel-ten-ashambuliwa-na-vijana-wa-uvccm-huko-bububu-zanzibar.html

  Hii habari pia inaondoa mashaka kwa Channel10 kwani mwanzo kulikuwa na dhana kuwa mwanagozi si mwajiriwa kabisa ila ni agent.Sijui hili la Bububu,ila ni uhsahidi pia kuwa tatizo si chadema.Na hatari ya waandishi ipo mbali zaidi.
   
 20. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  baada ya wabunge wa Arusha,mwenyekiti mBeya sasa mwanza napo wanataka "pima maji" sijui "sumu yao kama imeshakuwa kali".Chagulani kaanza mapema kutema cheche.Sijui kama ana ufahamu mkubwa kuhusu huyu kiumbe CDM.Sijui kama anafahamu fate ya wenzake kisisasa na maamuzi makini na yasiyopinda ya CDM.

  We are here to witness how honey badger doesn't care who is blocking the way.Chagulani?Mala? TBC?Polisi? Tendwa? Wassira? CUF? +++?
   
Loading...