CHADEMA kama hatutakuwa na ruzuku, ninaomba tupeane hapa mikakati ya kukinusuru chama

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,159
27,194
Habari wanaJF,

Leo kuna jambo ambalo ningependa kuona michango ya wanachadema wenzangu (hasa wale ambao hawana mihemko).

Matokeo ni kama tunavyoona kuwa ni kama hakutakuwa na ruzuku hivyo tutafute mbinu mbadala ya kukinusuru chama.

Wote tunafahamu kuwa ruzuku ilitumika kwa ajili ya kuendeshea shughuli za chama.
Hivyo ili chama kiendelee ku-survive ni lazima kuwe na vyanzo vingi vya pesa, sasa basi ninaomba wanachama kwa umoja wetu tutoe maoni ya jinsi gani tunaweza kupata pesa ili chama kiendelee kuwepo, vinginevyo hiki chama kinaenda kufa (wala sio suala la utani).

Ikumbukwe kuwa kuna kiongozi alikikopesha chama kwenye uchaguzi huu, kwa minajili ya kuja kurudishiwa pesa zake baada ya uchaguzi (hizi pesa mara nyingi hurudishwa kupitia ruzuku).

Maoni yangu mimi, vifanyike vitu vitatu hapo chini;
  • Itolewe namba, kila mwanachama achangie shillingi 1000 kila mwezi. Mfano tuna wanachama laki moja walio Active ukizidisha mara 1000( 100,000*1000) ni sawa na 100,000,000 kila mwezi. Kwa mwaka inakuwa Bil 1.2. Tuseme ukweli wanachama active laki moja watashindwa kuchanga 1000? Tena kwa mwezi?
  • Kuwe na mfumo rasmi wa kuuza bidhaa za chama, mfano Tshirt na mashati, bendera n.k. ziuzwe tshirt na shati na bidhaa nyingine za chama kama bendera, keyholders, stickers n.k hii itasaidia sana kuinua kipato cha chama.
  • Magari yapunguzwe, na baadhi yauzwe kwa minada. Mfano zile ford rangers zipo nyingi sana hadi sasa, na kwa ukata utaokikumba chama sidhani kama zitaweza tena kusurvive, hivyo ziuzwe na pesa inayopatikana iimarishe chama.
Mwisho kabisa tuseme ukweli bila kupepesa macho, mwenyekiti adhibitiwe kwenye matumizi ya pesa.

Nawasilisha.
 
Hivi ndivyo Wapemba walivuompa support Maalim baada ya kususia uchaguzi. Inawezekana na wenye uwezo watoe zaidi ya 1,000.

Kumbuka CHADEMA ni chama kikubwa, kuna nchi rafiki pia zitatoa misaada. Lakini kuhakikisha mishahara ya wanao endesha ofisi, michango ni lazima.
 
Mimi siyo Mchadema lakini niko tayari kuchangia kiasi kidogo. Tunahitaji upinzani imara na CDM naamini ndiyo chombo hicho-tunawahitaji ili waweze kutusemea inapobidi: katiba mpya, serikali ya majimbo, utawala wa haki, uhuru na maendeleo mambo amabayo CCM kamwe hawatathubutu kuyafanya.
 
Mimi nitachangia japo sio mwanachama ila kuna watu lazima tuhakikshiwe kuwa hawatahudumiwa kwa hela zetu za michango, mfano kama huyu hapa kamanda
2425918_mukya.jpg
kwanini asitafutiwe kazi nyingine ya kumupatia kipato halali?
 
We jamaa wauze tena vitendea kazi??? Kwenye siasa cha kwanza ni magari kuwafikia watu.

Wawake utaratibu mzuri wa michango,naamini watanzania wengi watawachangia.
 
Haya ndiyo mawazo ya msingi.

Mambo Kama haya yanatokea ili binadamu tupate kurudi kwenye misingi tufanikiwe zaidi.

Hapo Kati kulikuwa na mihemko na kutopokea mawazo mbadala.

Natamani nijinukuu niwakumbushe wale wabishi niliposema kuwekeza kwenye Ford Ranger ilikuwa siyo Bora maana hazizalishi faida kubwa huku zikihitaji matengenezo.

Na hazikufanya kampeni kubwa Kama ingelikuwa kuwekeza kwenye media. Media za chama siyo kiongozi binafsi.
Media zingetoa ajira kwa wanachama wengi zaidi kipindi hiki kigumu. Kwa maana zingetoa ajira Hadi kwa reporters wa mikoani.

Kwenye changamoto ndiyo Kuna fursa nzuri mpya.
 
Mimi nitachangia japo sio mwanachama ila kuna watu lazima tuhakikshiwe kuwa hawatahudumiwa kwa hela zetu za michango, mfano kama huyu hapa kamandaView attachment 1615866 kwanini asitafutiwe kazi nyingine ya kumupatia kipato halali?
Wa kuwaambia ukweli ni wale waliomzu guka mwenyekiti wale wachache ambao walimpotosha mambo mengi na kukigawa chama.

Huyu dada Hana tatizo anajiweza tuache maisha binafsi ya watu kuyafanya siasa.
 
Back
Top Bottom