CHADEMA Kama chama cha Siasa na Vuguvugu la Kisiasa: Changamoto kwa CCM na Demokrasia Tanzania


Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Katika kipindi cha hivi karibuni, vyama vya upinzani nchini Tanzania vimekuja na mbinu mpya za kisiasa ambazo zinahusisha Political Movements (vuguvugu la kisiasa); Vyama hivi ni viwili – Chadema (M4C) na CUF (F4C), lakini kwa sababu fulani fulani, mjadala mkubwa kuhusu mbinu hizi mpya za kisiasa umekuwa unakigusa zaidi Chadema na M4C, huku jamii ikigawanyika kuhusu maudhui na umuhimu wa M4C katika kipindi hiki; Kumekuwepo na mijadala mbalimbali juu ya M4C ambayo imetupatia elimu kubwa kuhusu suala hili kwa ujumla wake, lakini kwa kiasi fulani, binafsi naona kwamba bado kuna pengo kubwa ambalo mijadala hii haijaliziba, hasa kutokana na mijadala mingi juu ya M4C kuendeshwa kishabiki zaidi na pande zote mbili – yani Chadema na CCM, badala ya mjadala kutumia 'a relevant analytical framework' ; Nia ya mjadala wangu ni kuziba pengo hilo, hasa kwa kufanya mambo makuu mawili:

Kwanza, kwa kuwasilisha 'analytical framework' ambayo itatupatia mwongozo kuhusu tofauti baina ya A Political Party na A Political Movement, kwa mujibu wa gwiji wa siasa za Africa (Goran Hyden); na Pili, ni kujadili dhana ya M4C katika muktadha wa maswali makuu sita kama ifuatavyo:

 1. Je watanzania wanaelewa tofauti iliyopo baina ya 'A political Party' and 'A political Movement'?
 2. Je ni watanzania wangapi wanaelewa kwamba hata TANU (CCM) ilianza kama 'A Political Movement', kabla ya kuwa ‘A Political Party'?
 3. Je, 'Political Movements' huzaliwa katika mazingira gani?
 4. Je, kwanini imechukua zaidi ya miaka 50 kabla ya Political Movements kuzaliwa tena Tanzania? Hii ni tofauti na 'political pressure groups' kama vile DP ya Mtikila;
 5. Je vyama vya Siasa kwa mfano (Chadema na CUF), vinawezaje kuchanganya dhana hizi mbili kwa ufanisi – yani kwa upande mmoja kuwa ‘A Political Party' na kwa Upande mwingine kuwa ‘A Political Movement'?
 6. Na Mwisho, Je, ni mahitaji gani ya wananchi ambayo hayawezi kupatikana kupitia Political Parties peke yake, hivyo kuhitaji Political Movements?

Below, ni tofauti kuu baina ya Political Movements na Political Parties Per Goran Hyden, ambayo itakuwa ndio 'KEY Analytical Framework' ya kufanikisha malengo ya mjadala wetu;

VARIABLE
POLITICAL MOVEMENT
POLITICAL PARTY
OrientationCauseIssues
Level of OperationRegimeGovernment
Main Arena of OperationSocietyParliament
Method of OperationMobilizationPersuasion
Member OrientationDiffuseSpecific
Claims to ResourcesNo Formal LimitsConstrained by Rule of Law

Ni matumaini yangu kwamba mjadala wetu utatawaliwa na HOJA na sio VIROJA na ushabiki wa Kisiasa; Lakini kwa vile mjadala huu ni wa Kisiasa, ushabiki kuwepo ni jambo la kawaida lakini hata ushabiki upo wa HOJA na VIROJA; Kwa mfano, mimi ni mwana CCM na from time to time, nitakuwa na hoja za kishabiki juu ya kwanini ilikuwa ni muhimu kwa TANU kuwa a political movement katika kipindi kabla ya uhuru; Lakini pia from time to time, nitakuja na hoja zangu binafsi kama mtanzania kuelezea kwanini hata katika nyakazi hizi, kuna umuhimu wa kuwa na Political Movements, hasa kwa kuwa Tanzania as a state, is still at its formation stage, that's why it is weak, fragile, and may even fail/collapse before our eyes, kama hatutakuwa makini;

Ni imani yangu kwamba mwisho wa siku tutafanikiwa kuja na mjadala ambao utatusaidia kuelewa suala hili more SYSTEMATICALLY, hasa:

 1. Kuelewa kiini cha Political Movements katika demokrasia ya uliberali;
 2. Kuelewa umuhimu wa Political Movements katika demokrasia ya uliberali;
 3. Kuelewa mipaka ya uhalali na uhalifu (kama ipo) ya 'Political Movements' ndani ya Demokrasia ya uliberali;
 4. Kuelewa changamoto zinazotokana na Chama kuanzisha ‘A Political Movement' Badala ya Chama Kuwa ni matokeo ya ‘A Political Movement'; mfano, trajectory ya Chadema na TANU zipo tofauti katika hili;
 5. Kujifunza zaidi juu ya Demokrasia ya Uliberali kwa ujumla wake;

Last but not least, ningependa kusema kwamba - mara nyingi, political movements na mass – based parties huenda sambamba; ingawa kwa sasa, enzi za mass – based political parties imepitwa na wakati katika demokrasia zote za uliberali duniani, muitikio wa Umma kwa M4C unaashiria kwamba we have a failed state in Tanzania (nitalijadili hili kwa kina baadae), na pengine Chadema inakaribia kugeuza historia right before our eyes; Vinginevyo katika hali ya kawaida, chini ya mfumo wa sasa wa uliberali (kiuchumi, kijamii na kisiasa), jamii za leo zipo very diverse in terms of matarajio from political processes, matabaka, n.k, kiasi cha kutowezesha mazingira ya mass – based political parties kushamiri; Na hii sio kwa Tanzania tu bali karibia mataifa yote duniani yanayoendeshwa chini ya mfumo wa demokrasia ya uliberali;

Pamoja na uwepo wa mabadiliko haya – yani ya kuporomoka kwa mfumo wa mass – based political parties, bado kuna ishara kubwa kwamba, kwa upande mmoja CCM inajaribu kuendeleza mfumo wa a mass – based party kama njia ya ku justify its popular support, na kwa upande mwingine, Chadema nayo inajaribu kuiga mfumo huu ili nao wawe ni mbadala wa CCM in terms of being a substitute mass – based party with popular support; Vyama vyote viwili vinafanya juhudi hizi ndani ya mazingira ambayo in the long run, sio CCM wala Chadema itaweza fanikisha hili kwa urahisi, kwani - key determinants ya chama kuwa mass based ni pamoja na:

 • Chama kuwa na wanachama wengi sana na ambao wanalipia ada zao na pia kujishughulisha na chama husika katika muda mwingi wa maisha yao ya kila siku;
 • Popular participation nyakazi za chaguzi kuu, kwa mujibu wa itikadi ya vyama kuwa kubwa sana;
 • Na factors nyingine nyingi ambazo tutazijadili baadae;

Yote haya kwa sasa yapo in reverse, hence signaling kwamba days of mass - based political parties are not numbered by they are over and done; Na hii sio kwa Tanzania tu bali katika nchi zote zinazoendesha siasa zake chini ya mfumo wa demokrasia ya uliberali; Kwa maana nyingine, downward trend ya factors hizi maana yake ni kwamba mass - based political parties are loosing ground in liberal democracies na zinakuwa replaced na aina nyingine za vyama vya siasa, hasa 'Cartel Parties' - which is literally a consortium of elites; Tutalijadili hili kwa kina baadae;

Ni matumaini yangu kwamba mjadala huu utatufundisha mengi juu ya changamoto hizi na kwa pamoja tutaibuka kama watu tulioelimika zaidi juu ya demokrasia na umuhimu wake kwa maendeleo ya walio wengi;
 
W

WATANABE

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
1,091
Points
1,195
Age
59
W

WATANABE

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
1,091 1,195
Kama ulivyoanza kwa kichwa cha habari kuwa cha Kiwasahili ungeendelea hivyo hivyo, kwa maana baada ya kubadili lugha umewaacha wengi hivyo utakosa wachangiaji.
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,597
Points
2,000
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,597 2,000
Mchambuzi,

Katika hatua tuliyofikia political Movement haina tofauti na enzi za TANU.Sitajadili sana Cartel kwa kuwa CARTEL somehow ni irrelevant kulinganisha dynamics in our political Landscape.Cartel inafaa nchi nyingi ambazo ni adavanced katika demokrasia na sisibado tuko katika infant age ya demokrasia.Hiyo haiwezi kufanyika ingawa kuna vielement vichache.

Political movement mara nyingi imezoeleka ni kwa ajili ya a specific goal kama ilivyokua kwa ODM ya Kenya katika mchakato wa BOMAS na tumeshuhudia kitu kilichoanza kama movement ndani ya serikali kilizaa chama strong cha kisiasa na almost kingetwaa Dola

Sasa ni lazima uwe na raslimali za kutosha kuongoza movement kama pressure ya kusukuma agenda.Kwa mfano kwa CHADEMA ingawa mambo mengi sitaki kuyaandika hapa(reserved) ni lazima tufanye cocktail ya strateggy za chama na Movement(M4C).Wakati wabunge wakisimamia kuibana serikali Bungeni huku nje wale viongozi na wanachama na raslimali zote zinaendelea kutekeleza mkakati wa ku-push mass kila angle ya nchi hii kwa malengo ya kuunganisha na ku-sentize public.we need to put more efforts and consolidating of what we have already achieved.

Sasa kwenye hoja ya movement za CUF na CHADEMA haziwezi kuwa kitu kimoja au kuunganishwa.Sababu ni zile zile za CARTEL ambayo vyama vya siasa hufanya Collussion na kupunguza competition baina yao.Kufanya hivyo ni lazima Demokrasia yetu iwe elevated kuliko hapa ilipo sasa ili tutumie professionals,Technocrats na pia kiwango cha Elimu ya Uraia kipande ,watu wajue umuhimu wa wanachoelezwa katika ilani na policies badala ya kuwa fanatics n.k

So CUF na CHADEMA tunaweza kufanya movement collussion kwenye hoja ya ume huru za uchaguzi ingawa kwenye katiba mpya ndiyo ingwekuwa working groung nzuri
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Kama ulivyoanza kwa kichwa cha habari kuwa cha Kiwasahili ungeendelea hivyo hivyo, kwa maana baada ya kubadili lugha umewaacha wengi hivyo utakosa wachangiaji.
najitahidi ku - master lugha ya kiswahili, huku pia nikijaribu kutumia lugha ya kiingereza ili nisipoteze maana ya maneno au ujumbe fulani; Tatizo lingine pia ni kwamba katika lugha yetu hatuna literature ya kutosha inayozungumzia nadharia mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kijamii; Tuna kazi kubwa katika kufanikisha hilo; Vinginevyo iwapo inatokea kwamba kuna hoja inakuvutia kwa kiasi fulani lakini hauelewi kutokana na matatizo ya lugha, sidhani kama kuna ubaya kuulizia ufafanuzi;
 
measkron

measkron

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
3,786
Points
1,500
measkron

measkron

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
3,786 1,500
mi nadhani bado nchi nyingi za kiafrika bado tupo kwenye transtion stage katika political,economy na nk..
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Ben Saanane;

Nashukuru kwa mchango wako katika bandiko namba tatu; Nakubaliana na wewe katika maeneo kadhaa;

Kwanza ni hoja kwamba mazingira ya sasa yanaruhusu kushamiri kwa Political Movements nchini; Hii ni kwa sababu kazi iliyoanzishwa na TANU haikukamilika, iliishia njiani kutokana na sababu mbalimbali; Mbaya zaidi, CCM kwa kiasi fulani inasaliti historia yake yenyewe, na ni usaliti huu ndio unaipa Chadema nguvu kubwa mbele ya UMMA;

Pili ni hoja kwamba Jamii yetu haijafikia hatua ya kuwa na Vyama aina ya Cartel, ingawa sikubaliana na wewe katika hili mia kwa mia; Kabla sijachangia sana juu ya hili, nikuulize, je kuna chama gani Tanzania ambacho hakikuanzishwa na elite or a consortium of elites? Kuna chama chochote Tanzania kilianzishwa na wakulima au wafanyakazi per se? Haijawahi kutokea na sidhani kama itakuja kutokea;

Tatu ni hoja yako kwamba collusion ya opposition kuhusu katiba mpya ingefanikisha sana Political Movement towards katiba mpya; Lakini ni muhimu tukumbuke kwamba kazi ya CUF haikuwa nyingine zaidi ya kukomboa Zanzibar, na kazi hiyo inakaribia kukamilika; Tofauti na wenzetu ambao hatimaye wamefanikiwa kupata Katiba Mpya, pia wapo mbioni kupata Taifa jipya; Hivyo Chadema haiwezi kuwa compatible na malengo ya CUF, hata kama sehemu kubwa ya constitutional crisis remains to be the Union Question; kwa kifupi, Geopolitics haziruhusu collusion baina ya Chadema na CUF, na ukweli huu utabakia kwa muda mrefu sana;

Kuna tofauti moja kubwa baina ya Chadema na CUF ambayo watu wengi hawaitazami; CUF kama chama cha Siasa kinafikia maturity stage na muda sio mrefu kitaingia kwenye declining phase; Nitafafanua kwa njia nyepesi; Kama ilivyokuwa kwa TANU, CUF ilikuw na kazi kubwa moja – kuletea wananchi husika ukombozi; Kazi hii ikikamilika (i.e. ukombozi wa Kisiasa), kazi inahamia kwenye ukombozi wa kiuchumi; Kama vile TANU (baadae CCM) ilivyokwama katika hatua ya pili ya ukombozi (ukombozi wa kiuchumi), CUF nayo itagota katika hilo kwani viongozi wake wengi hawapo kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar kwa jumla wake bali sehemu ndogo ya wananchi hao; Kwa utabiri wangu, kule Zanzibar, ndani ya miaka kumi kitaibuka chama kipya cha mfano wa Chadema ambacho kita phase out CUF, kama CCM inavyoelekea kuwa phased out na Chadema bara, hasa iwapo political market forces zitaachwa to play out, bila dola kuingilia; unless CCM ibadilike na ibadilike sasahivi, sio baadae; Tofauti na CUF ambayo imefikia maturity stage, Chadema bado ina experience growth, na ikifanikiwa kuingia madarakani 2015 au 2020, bila umakini, nacho kinafikia mwisho wa growth na kufuata mkondo wa CUF; Ndio maana sustainability is very important for Chadema – hatujui wamejipanga vipi in the medium to long term iwapo wataingia ikulu;

Wananchi wana too much expectations na Chadema, na wataichoka mapema sana ikiingia ikulu kwani Chadema does little kuwaeleza wananchi maneno – 'tunataka kuingia to reconstruct what CCM has destructed for 50 years, so don't expect much in the first 10 years ya utawala wetu; Lakini mtarajie serikali sikivu, isiyovumilia rushwa, na itakayo wapunguzia gharama za maisha, not abruptly but incrementaly'; Kauli hii ikipangwa vizuri, Chadema ikiingia Ikulu, itakaa kwa muda mrefu sana, hasa iwapo itajaribu ku balance suala la udini, ukabila...kwa kifupi, kuchukua mazuri ya Mwalimu Nyerere; Kwa kifupi Chadema needs kuuza kwa umma mpango wao wa muda mfupi, kati na mrefu wa maisha ya ikulu, vinginevyo CCM tutakuwa tunawasubiria kwa hamu waboronge, halafu ifikapo 2020 tuwaambie wananchi maneno kama - mnaona sasa, kutawala nchi sio mchezo, hawana kitu hawa, ni rahisi sana kupiga kelele ukiwa upande wa upinzani, ukiingia jikoni ni suala tofauti, si bora CCM? Turudisheni ikulu tuka fanye kazi...; Na wananchi wakija kuitikia wito huu, huo ndio utakuwa ni mwisho wa Chadema;

Nikiingia kwenye upande wa hoja zako ambazo Napata shida kidogo kukubaliana na wewe, kwanza ni hoja yako kwamba ili ufanikiwe with a political movement, ni lazima uwe na rasilimali za kutosha; Kwa mtazamo wangu, hakuna rasilimali muhimu katika hili zaidi ya WATU walioshiba the cause, na wenye imani na the cause, na waliokuwa tayari kutoa absolute confidence and unconditional support kwa leadership husika; Pia political movements do not need professionals, technocrats and the like but it's the other way round – technocrats and professionals wenye Uzalendo na nchi yao need political movements kufanikisha their cause;

Pia kwenye suala la elimu ya uraia, naelewa kimsingi unalenga nini lakini ni muhimu ukumbuke kwamba TANU haikutoa elimu yoyote ya uraia, elimu hii ilitolewa na Civic Institutions za the Colonial State kwamba TANU inafanya mambo yasio kuwa na maslahi kwa nchi; Ilichofanya TANU ilikuwa ni ku mobilize watu weusi and persuade them kwamba Civic Institutions of the state zilikuwa harmful na kwamba what needed was a defeat to these institutions ili community based institutions alizozikuta mkoloni zirudi katika nafasi yake ndani ya jamii; Haikuhitaji elimu ya uraia kuwa shawishi weusi wa Tanganyika kwani madhara yaliyotokana na interruption juu ya maisha yao by an alien entity yalikuwa wazi; Kilichohotajika ni a charismatic and organized person no mobilize wengi kuunga mkono the relevant cause at hand;

Pia sidhani kama mafanikio ya M4C leo hii yanatokana na mchango mkubwa wa Elimu ya Uraia, unless we have a different notion juu ya elimu ya Uraia;
 

Forum statistics

Threads 1,294,754
Members 498,027
Posts 31,187,127
Top