Bartazar
JF-Expert Member
- Oct 4, 2011
- 1,043
- 565
CCM hamjajibu hoja za msingi. Hamkutueleza habari za kuvuana magamba zimefikia wapi? Maisha bora mliyoyaahidi yapo wapi, mbona siku hizi hamyasemei? Ninyi mmeshika dola wala hamkuhitaji kufanya mkutano wa hadhara! Matendo yenu tu yangetosha kutueleza kwamba kuna vitu mmefanya. Mwenye macho huwa haambiwi tazama. Sasa mafanikio mnayosema mpaka tuyatafute kwa tochi?
Si kwamba hamjafanya kitu kabisa, la hasha, ila mlichofanya ni kiduchu ukilinganisha na umri wenu! Mkae mkielewa kuwa watz wa leo wanafahamu kutenga mchele na pumba. Zile za jangwani mbona fiksi tu, hata mioyoni mwenu mnajua kuwa mlichofanya ni fiksi na hamuwezi kujivunia! Kwanza mmewasomba watu kama kawaida yenu. Pili mmewapa elfu tano tano, t- shirt na kofia. Hata mdogo wangu alipokea hiyo hela. Hapo si mnafanya kazi ya kupaka rangi upepo? Toka hapo zamani mlipoanza kuahidi hamtekelezi, mkifanya, ni kudogo tu kwa ajili ya kuzuga, mbona ahadi zenu hazitofautiani na za kuku?