Chadema kaeni chonjo! Moto huu hauzimiki leo ama kesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kaeni chonjo! Moto huu hauzimiki leo ama kesho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAFILILI, Jun 10, 2012.

 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,849
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  CCM oyee! Ni furaha ilioje chama chetu kuweza kukonga mioyo ya wananchi wa DSM waliofurika viwanja wa Jangwani kwa utashi wao na mapenzi kwa chama.

  Timu ya jana imetoa salamu tosha kwa CDM kwamba CCM bado ni kipenzi cha wana darisalama kutokana na utekelezaji wa miradi yenye tija kwa wananchi wa TZ. DSM ikiwa ni kiwakilishi cha makundi ya watz toka mikoa yote, uwepo wa makundi mbalimbali ya wananchi ni uthibitisho kuwa CCM ni chombo cha wote tofauti ya CDM chombo kinachomilikiwa na watu wa Kaskazini.

  Ni faraja ilioje kuwa mkutano wa Jangwani itafuatiwa na mikutano mingine Kinondoni, Ilala na Temeke ili kuwapelekea wananchi neno la matumaini kabla ya 2015.

  Mikutano ya Ilala, Kinondoni na Temeke itafuatiwa na mlolongo wa mikutano katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Kigoma, Manyara, Mbeya, Mwanza, Ruvuma, Shinyanga na Kumalizia Iringa, hapo mwaka 2012 utakuwa umeisha. Miaka 2013 - itakuwa zamu ya mikoa mingine ikiwa na mazishi rasmi ya CDM katika mikoa ya ukanda wa Ziwa.
  TAFADHALI MWANA CCM kuwa wazi na jasiri kutetea chama chako; KWA KUVUA GAMBA NA GWANDA, VAA UZALENDO
   
 2. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 9,101
  Likes Received: 5,208
  Trophy Points: 280
  Bado kazi ipo
   
 3. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,606
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Kweli Mafilili mlikonga jana. Mitaa ya kwetu huku jet lumo walikuwa wanachukua elf tano kila mwanachama mlangoni unaposhuka kwenye coaster iliyowapeleka na kuwarudisha.
  Hiyo ndo ilani pekee mliyoweza kuitekeleza, TAKRIMA NA BAKSHISHI. POLE.
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 34,641
  Likes Received: 11,547
  Trophy Points: 280
  jana ulichukua posho nyingi wewe hadi za wenzako...e bwanae hivi t shirt zile mnazivalia wapi tena zaidi ya kwenye mikutano yenu?
   
 5. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,757
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nisinguka na kazi ningewaambia mje mnichukue nyumba, mnilipe hiyo 5000/= na mnirudishe kwangu

  huu ndio mwendo wa kula ccm kura chadema

  wajinga ndio waliwao
   
 6. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kama mkutano wa jana umetatutua kero za wana darisalam kule mabwe pande na mvua ikinyesha maji hayajai mitaani sawa na bei ya vitu kupungua kama sugar na mchele ,maharage
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 34,641
  Likes Received: 11,547
  Trophy Points: 280
  kura chadema kula ccm
   
 8. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,367
  Likes Received: 440
  Trophy Points: 180
  Huyu sio mingine bali ni Wasira from katavi game res.
   
 9. t

  tubadilike-sasa JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 677
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Sasa CCM mlikuwa mnashabikia nini? Maana mambo ya Kagoda,Deep Green,Meremeta,Uzwaji wa nyumba za serikali,Radar, nk bado yanatokota.Inahitaji mtu mwenye moyo wa mwendawazimu kushangilia CCM na Serikali yake kwa mambo inayoendelea kufanya. Dawa ya jino ni kuling'oa sio panadol
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Uongo huo, kama mlivyozowea. Kwanini hukupiga picha?
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  CHADEMA jana wameshaelezwa kinaga ubaga, tunakwenda Tanzania nzima kuwaona wananchi na kuwaeleza ana kwa nana ukweli wa mambo ulivyo, siyo hawa jamaa wanaowajaza uongo.
   
 12. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 9,101
  Likes Received: 5,208
  Trophy Points: 280
  Nyie pigeni kelele tu mnadhani wenzenu bado miaka ya 2010. Sasa hivi CCM inabadilika. Kinachotakiwa CDM wabadilishe mfumo wa sera zao maana kiukweli kelele za CDM kimewafanya CCM wanabadilika.

  USHAURI:

  Wanatakiwa CDM wabadilishe mfumo wa Sera zao la sivyo mwaka 2015 itakuwa hivi:-

  CCM 75%
  CUF 10%
  NCCR 7%
  CDM 5%
  UDP 2.5%
  Others 0.5 %


  Kuweni chonjo watanzania wanaakili sio wajinga. Vyama vyote vinatakiwa kubadilika

  TRUTH SHALL SET YOU FREE
   
 13. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 10,496
  Likes Received: 1,592
  Trophy Points: 280
  Mbona umekuwa mbogo ghafla?twende taratibu basi.
   
 14. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #14
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 10,496
  Likes Received: 1,592
  Trophy Points: 280
  We ndio yule bingwa wa kinyume nyume?
   
 15. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,208
  Likes Received: 3,188
  Trophy Points: 280
  Kama watetezi wa ccm ndio uwezo wenu wa kukinadi chama umeishia hapa nina mashaka sana na mustakabali wa chama chenu. Mafilili hawa ndio wenzako na huenda mnalipwa ujira sawa.
  Sisi tunachopenda kuskia ni treni zinatembea reli ya kati na tazara, bei ya sukari na mchele inashuka na sio porojo za kuwajibu CDM
   
 16. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,175
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280

  Ukweli ni upi Mkuu Zomba..? Kwamba mfumuko wa bei umesababishwa na mafuta na ni tatizo la dunia zima..? Kwamba JK kuwasamehe wezi wa EPA ni kutekeleza amani na stability ya nchi..? Kwamba mgao na ukosefu wa umeme na gharama za umeme kuwa juu ni kazi ya Mungu na kwamba hakuna uwezo wa binaadam unaoweza kubadilisha hilo..? Kwamba polisi na magereza yamewekwa kwa ajili ya waiba kuku na wala rushwa za shilingi mia mbili ila wale wanaoiba na kutoa rushwa ya mabilioni wanastahili kuendelea kuishi maisha ya raha katika majumba yao..? Kwamba watoto wa viongozi ndo wana haki ya kusoma na kupata huduma za afya nzuri lkn wao watoto wao waendelee kusoma katika shule za kata ambazo hazina vifaa.. maabara wala walimu na wakiugua waende kwenye private hospitals na India..? Kwamba kwa zaidi ya miaka 30 makao makuu ya chama na serikali yako Dodoma kwenye makaratasi lkn Serikali yote bado iko Dar mpaka leo..?

  Hakuna jipya ambalo CCM watalisema ambalo hawajalisema kwa miaka 50 sasa..! Umefika wakati wa kuacha ushabiki kama wa mpira na kuangalia Tanzania yenye matumaini..
   
 17. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #17
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 9,101
  Likes Received: 5,208
  Trophy Points: 280
  Hata mimi ninataka hivyo lakini si unajua dalili ya mvua ni mawingu. Mimi ninaona wingu kama mkono la mabadiliko kwenye CCM so kama dalili hizo zinaonekana; basi ni alama ya kwamba chadema wabadilishe mfumo wao. Sio kwamba napenda CCM la hasha ila naona mabadiliko yanakuja.

  TRUTH SHALL SET YOU FREE!!!!
   
 18. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #18
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 9,101
  Likes Received: 5,208
  Trophy Points: 280
  SOsoliso: Mimi napenda watu realistic kama wewe sio ushabiki usio na tija
   
 19. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 25,990
  Likes Received: 22,217
  Trophy Points: 280
  hivi wale oil chafu na vinyago ndo wanaambiwa wavae uzalendo????
  Mnarudisha oil chafu kwenye gari lenu??
   
 20. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #20
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  usijidanganye ndugu moto wa M4C hauzimiki kamwe...
   
Loading...