CHADEMA jitahidini muwe na "JOPO" la kumshauri mgombea wenu wa Urais ili atakachonena iwe sauti ya Chama

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,817
3,385
Nimemsikiliza Mgombea Urais kupitia Chadema. Kiujumla anapaswa kuongea zaidi kuliko wagombea wa vyama vingine.

Kwa kuwa hakuweponchini kwa muda mrefu tofauti na wale wengine, inaweza kuwa sababu ili afahamike. Lakini pia siyo mgeni kwa mambo ya nchi yetu. Watu wana shauku ya kujua "SERA MBADALA" na siyo " SERA FITINA".

Hapa nina maana kwa mfano JPM kanunua ndege kadhaa, je, yeye ana maoni gani mbadala? Mfano mwngine JPM kakopa korosho za wakulima na malipo yakasuasua, je yeye kwenye hili ana maoni gani?

Haya ndiyo watu wengi kama siyo wote wangependa kuyasikia na ndiyo yatawapa credibility Chadema ya kura nyingi.

Siyo wakati wa kupoteza muda kuponda hata vile ambavyo mwananchi wa kawaida anaona vimemsaidia.

Mfano, ukisimama hadharani ukasema JPM anatoa au kupokea rushwa wananchi watakudharau kwa vile wamejionea alivyopambana na ulaji rushwa, alivyotumbua wengi nk.

Hapo utapoteza credibility haraka na wananchi watawachoka mapema tuu. Nchi imebadilika sana.

Hivyo, kwa vile Mgombea wenu ni jina kubwa hapa nchini, awe makini na anachokiongea, na kuwe na jopo la kumfunga breki mapema. Bado hamjachelewa.

Hayo ni maoni yangu binafsi.
 
Natamani sana Lissu awe anaongelea tu Masuala (Issues) tena zile zenye Tija kwa Maendeleo, ila kwa Hasira zake nahisi ataliongelea Shambulizi.
Kuna mambo mengi yatakayochangia kumpa Lissu kura, na mojawapo ni hilo shambulio, na sijui kwanini hupendi kusikia kuhusu lile shambulio dhidi yake.
 
Mkuu kwanza kampeni bado hazijaanza kwa hiyo hayo mambo yataongelewa huko.

Pia kuna issues ambazo hazina sura ya kutaifa hivyo si muhimu ziongelewe popote pale mfano ukimuongelea korosho mtu wa kanda ya ziwa ataona ni jambo la maana kwake? Vitu kama hivyo vitaongelewa huko sehemu husika.

Kwa hiyo Jpm anapambana na rushwa? Kutumbua watu hovyo hovyo kwa tuhuma za ubadhirifu na kisha baadae kuwarejesha bila hatua yoyote kuchukuliwa kwako ndio mapambano ya rushwa?

Kama anapambana na rushwa kwa nini hataki miradi aliyoifanya bila idhini ya bunge isikaguliwe, anaficha nini? Kwa nini amuondoe CAG (Assad) baada ya ripoti yake kuonesha deficit ya 1.5trl badala ya kushughulikia huo upotevu?

Nini ambacho mwananchi wa kawaida amesaidiwa na kikapondwa? Mfano katumbua watu wenye vyeti feki kisha kamuacha Makonda anayetuhumiwa kwa kosa hilo hilo tena anasema mradi anachapa kazi hata kama hana vyeti, huyo ndio mtu anaye wasaidia wananchi?

Mwisho huu ni uchaguzi, anayeona ana sababu za kumchagua huyo magufuli na akamchague na watakao shawishiwa na Lissu nao watampigia kura pia.
 
Lissu kajiwekea uhalali wa kuongea chochote huku akitegemea International Mercy kwamba ana watetezi wengi. Katika political arena ni sawa ila kwa nchi Kama Tanzania ambayo imekua inanyonywa miaka mingi tungependa mtu anayekuja na "SERA TATUZI" za mikwamo yetu ya kimaendeleo.

Anachuku cheap ideas ndo anabeba kama major ideas. Tuna macho na tunaona kinachoendelea. Ukimuuliza alipokuwa Mbunge kule Ikungi alifanya nn, hana cha kusema sanasana atasingizia kwamba alikua anazuiwa kufanya maendeleo na hatakuambia kwamba naye alikua sehemu ya tatizo la kuwarudisha nyuma wana Ikungi, alikua anawaambia eti kazi ya kujenga Shule, kuchimba visima vya maji sio kazi yao ni kazi ya Serikali mawazo mgando kama hayo halafu leo hii anajinasibu kama mtetezi wa wanyonge.

Yeye atukane, kejeli, kukosa ukomavu, kukosa uzalendo alafu mwisho wa siku atavuna anachopanda.
Chadema kumbukeni haya "Kikwete mtembezi sana, ni Rais dhaifu" kwa sasa "Magufuli hatembei ni dictator" kwa miaka 8 "Lowassa fisadi, mwizi" alipowapiga hela "Lowassa mtu mzuri sana" hatujasahau nyie endeleeni.....
 
Kuna mambo mengi yatakayochangia kumpa Lissu kura, na mojawapo ni hilo shambulio, na sijui kwanini hupendi kusikia kuhusu lile shambulio dhidi yake.

Kwakuwa linasemwa Kinyume na ambavyo Ukweli wenyewe ulivyo. Najua na Wewe ni Mmoja wa wale ambao wanauamini huo 'Uwongo' mkubwa!!
 
Muda utasema... Uongo una mwisho, CHADEMA wanauhadaa ulimwengu kuhusu issue ya Lissu. Lakini kilichotokea kinajulikana na hao Viongozi wao wanaujua ukweli lakini baada ya mambo kuwa kinyume tukio hilo limegeuzwa kuwa mtaji. Naamini hata Lissu mwenyewe anajua lakini hana ujanja kwake imekua political gain
 
Mkuu kwanza kampeni bado hazijaanza kwa hiyo hayo mambo yataongelewa huko.

Pia kuna issues ambazo hazina sura ya kutaifa hivyo si muhimu ziongelewe popote pale mfano ukimuongelea korosho mtu wa kanda ya ziwa ataona ni jambo la maana kwake? Vitu kama hivyo vitaongelewa huko sehemu husika.

Kwa hiyo Jpm anapambana na rushwa? Kutumbua watu hovyo hovyo kwa tuhuma za ubadhirifu na kisha baadae kuwarejesha bila hatua yoyote kuchukuliwa kwako ndio mapambano ya rushwa?

Kama anapambana na rushwa kwa nini hataki miradi aliyoifanya bila idhini ya bunge isikaguliwe, anaficha nini? Kwa nini amuondoe CAG (Assad) baada ya ripoti yake kuonesha deficit ya 1.5trl badala ya kushughulikia huo upotevu?

Nini ambacho mwananchi wa kawaida amesaidiwa na kikapondwa? Mfano katumbua watu wenye vyeti feki kisha kamuacha Makonda anayetuhumiwa kwa kosa hilo hilo tena anasema mradi anachapa kazi hata kama hana vyeti, huyo ndio mtu anaye wasaidia wananchi?

Mwisho huu ni uchaguzi, anayeona ana sababu za kumchagua huyo magufuli na akamchague na watakao shawishiwa na Lissu nao watampigia kura pia.
Noted.
 
Nimemsikiliza Mgombea Urais kupitia Chadema. Kiujumla anapaswa kuongea zaidi kuliko wagombea wa vyama vingine.

Kwa kuwa hakuweponchini kwa muda mrefu tofauti na wale wengine, inaweza kuwa sababu ili afahamike. Lakini pia siyo mgeni kwa mambo ya nchi yetu. Watu wana shauku ya kujua "SERA MBADALA" na siyo " SERA FITINA".

Hapa nina maana kwa mfano JPM kanunua ndege kadhaa, je, yeye ana maoni gani mbadala? Mfano mwngine JPM kakopa korosho za wakulima na malipo yakasuasua, je yeye kwenye hili ana maoni gani?

Haya ndiyo watu wengi kama siyo wote wangependa kuyasikia na ndiyo yatawapa credibility Chadema ya kura nyingi.

Siyo wakati wa kupoteza muda kuponda hata vile ambavyo mwananchi wa kawaida anaona vimemsaidia.

Mfano, ukisimama hadharani ukasema JPM anatoa au kupokea rushwa wananchi watakudharau kwa vile wamejionea alivyopambana na ulaji rushwa, alivyotumbua wengi nk.

Hapo utapoteza credibility haraka na wananchi watawachoka mapema tuu. Nchi imebadilika sana.

Hivyo, kwa vile Mgombea wenu ni jina kubwa hapa nchini, awe makini na anachokiongea, na kuwe na jopo la kumfunga breki mapema. Bado hamjachelewa.

Hayo ni maoni yangu binafsi.
Good thinking
 
Sera za Lissu
-Safari hii uhuni basi
-Nikishindwa uchaguzi naingia barabarani
-CCM hawana marafiki
-Magufuli alinunua jogoo kwa tsh 100,000/=

Eee Mwenyezi niweke hai hadi tarehe 28/10/2020 nifanye yangu .
 
Back
Top Bottom