Chadema:jipeni moyo…msiogope

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chadema:jipeni moyo…msiogope

Na Mashaka Mgeta

13th February 2011

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimefanyiwa `kitu mbaya’. Kimepokonywa haki ya kuwa kambi rasmi ya upinzani bungeni kutokana na marekebisho yaliyofanywa katika kanuni za Bunge.
Marekebisho hayo yalifanywa kufuatia ombi la wabunge wa Chama Cha Wananchi (CUF) na National Convention for Construction and Reform–Mageuzi (NCCR-Mageuzi ).
Ninasema Chadema imeporwa haki hiyo kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kwa maana kabla ya hapo, kilipaswa kuunda kambi rasmi ya upinzani.
Tafsiri imebadilishwa na kuvihusisha vyama vyote vya upinzani. Ndiyo maana wabunge Augustine Mrema na John Cheyo kutoka TLP na UDP, wamechaguliwa kuziongoza kamati za Bunge.
Mrema akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa ambayo Bunge lililopita ilikuwa ikiongozwa na Dk Willibrod Slaa wa Chadema na Cheyo akaiongoza Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali.
Sina shaka na uchaguzi huo, kwa vile umefanyika kwa mujibu wa kanuni za Bunge ambalo ni chombo chenye dhamana kubwa katika kulinda maslahi ya nchi na watu wake.
Lakini ijulikane kwamba Bunge linawahusisha binadamu, wenye nia, dhamira, matarajio na utashi tofauti, ukiwemo unaolenga kustawisha maisha ya raia ama kukidhi matakwa binafsi. Inawezekana.
Sina shaka na ushiriki wa wapinzani katika kambi rasmi ya upinzani bungeni, hasa CUF ambayo bado ninaamini kwamba ina hadhi, inakubalika, ina heshima na inahitajika katika harakati za kustawisha haki, amani na maisha ya Watanzania.
CUF ni chama kikubwa chenye mipango na mikakati madhubuti. Kina viongozi makini wenye maono yenye kulitakia mema taifa hili.
Nimewahi kufanya kazi zilizowahusu viongozi wa CUF katika Tanzania Bara na Zanzibar. Nimewahi kuwa katika misafara kadhaa ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kule Unguja na Pemba. Ninamjua kwa kiasi kinachonipa mamlaka ya kimaadili kumuamini kwamba ni kiongozi makini anayekubalika.
Hata wakati Mbunge wa sasa wa jimbo la Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohammed alipoteuliwana Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuwa Mbunge, taarifa ilipotangazwa tulikuwa tumeketi jamvini na Maalim Seif na viongozi wengine wa CUF.
Tulikuwa tunakula chakula cha jioni kwenye nyumba ya moja wa viongozi wa CUF(simkumbuki kwa jina) eneo la Machomane, kandoni mwa barabara inayotoka Chakechake kwenda Gombani.
Aliposafari kutoka Pemba kwenda Dodoma kula kiapo, nilipanda meli na Hamad Rashid, nilimhoji tukiwa katika bahari ya Hindi. Makala iliyotokana na mahojiano hayo ilichapishwa kwenye gazeti hili. Yapo matukio mengi ninayoweza kuyaelezea kuhusu jinsi ninavyoijua CUF na kutokuwa na shaka kuhusu sifa nilizozielezea awali kwa chama hicho na viongozi wake.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa Chadema. Ni Watanzania wachache wanaoweza kuziruhusu akili zao ziamini kwamba Chadema si chama makini. Wakisahau na kujiaminisha hivyo, bila shaka akili na fikra zao zitakuwa zimejikita katika uhuni.Kama ni hivyo tatizo lipo wapi? Kwa nini ifikie mahali CUF na Chadema kuingia katika mgogoro ambao vyama dhaifu vya upinzani vinapata mwanya wa kujipenyeza kuwa sehemu ya kujitangaza kwa umma? Ninaamini kwamba CUF ilistahili kujiweka kando na harakati za kubadili kanuni za Bunge, ili kutimiza matakwa ya kisiasa hata kama kwa mtazamo wao, iliona umuhimu kwa wapinzani wote kuhusishwa katika kambi rasmi bungeni.
Kwa maana inasadikiwa kwamba msingi wa mabadiliko hayo, ulilenga kuipokonya Chadema haki hiyo na si vinginevyo. Hatua hiyo ina maana pana sana.
Kama wapinzani wakiongozwa na CUF walitaka hivyo, ingefanyika kwa wakati mwingine unaofaa, kwa maana muda walioutumia, ilionekana dhahiri kwamba maslahi ya kisiasa yaliwekwa mbele. Hilo ni kosa.
Ni kosa kwa sababu kama wabunge wameasisi mchakato wa kubadili kanuni ili kukidhibiti chama cha siasa chenye haki ya kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni, watashindwa vipi kushiriki katika kubadili Katiba ili kumruhusu, mathalani, Rais yeyote atakayekuwepo madarakani, aendelee kutawala, ikibidi maisha yake yote?
Waswahili wanasema, dalili ya mvua ni mawingu. Mabadiliko ya kanuni yanaweza kuwa mfano wa mawingu. Nini kitafuata?
Lakini CUF ilipaswa kurejea katika historia na washirika wake katika kufanikisha mabadiliko hayo. Ingejiuliza na bado ina haki ya kujiuliza ikiwa washirika hao wana dhamira iliyo sawa na dira na mwelekeo wao (CUF)?
Hivi CUF inajiridhisha vipi kuwa na mshirika wa kweli aliyesababisha ikose viti katika uchaguzi wa marudio kwenye majimbo kadhaa ya Pemba, ikiwa ni mara ya kwanza na pekee tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini?
CUF imejiridhisha vipi kwamba NCCR-Mageuzi iliyowawekea pingamizi wagombea wake huko Pemba huku ikijua dhahiri kwamba kwa kufanya vile ilitoa mwanya wa ushindi kwa CCM, wamebadilika na kuwa `watu wema’?
Ama baada ya uchaguzi ule ulioibua dhana ya `kura za maruhani’, Mrema aliitisha mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Chakechake na kuitaka serikali imdhibiti Maalim Seif kwa vile (eti) ni mtu hatari, leo hii `ameongoka’?
Mrema ambaye kama ilivyokuwa kwa NCCR, chama chake kilisimamisha wagombea na `kuambulia patupu’ alihoji, kama Maalim Seif aliwashawishi Watanzania wa Pemba kupigia kura maruhani, atashindwa vipi kuwashawishi waiasi serikali yao? Hivi amebadilika ama ni yule yule mwenye fikra zile zile katika chama kile kile?
Historia hiyo inakumbusha jinsi Cheyo alivyowahi kukaririwa akiitaja CUF kama chama cha kidini kilichojikita kwenye uislamu. Kumbukumbu za vyombo vya habari zipo. Je amebadilika na kuiona CUF kuwa bora?
Sitaki CUF iingizwe mkenge, sitaki iibue hasira za wanachama na wafuasi wake. Ninapenda CUF ibaki katika heshima na utumishi bora kwa nchi na watu wake. Lakini hayo yakijiri, Chadema itambue kwamba yaliyofanyika kwa mujibu wa kanuni za Bunge, yamefanyika na yatakuwa hivyo.
Bila shaka itaendelea kuwa miongoni mwa vyama madhubuti nchini. Viongozi, wanachama na wafuasi wake hawatakiwi kuogopa. Kilichotokea bungeni kiwe chachu ya kuwapa nguvu zaidi na moyo wa kutoogopa. Msikate tamaa, jipeni moyo na kuendeleza dhana yenu ya `hakuna kulala, mpaka kieleweke’.
Mashaka Mgeta ni Mwandishi wa Habari za Siasa wa NIPASHE ambaye hivi sasa yupo nchini Kenya. Anapatikana katika simu namba +255754691540, +254702115303 au barua pepe: mgeta2000@yahoo.com ama mashaka.mgeta@guardian.co.tz.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI Chadema:jipeni moyo…msiogope

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Tatizo hakuna anayeona ukweli anaousema Mashaka Mgeta.
Tamko la Naibu K/Mkuu - CUF lilionyesha tu ni kwa kiasi gani CDM waliwatenda kwenye majimbo kadhaa lakini hakusema CCM, NCCR, TLP na UDP wameshatenda madhambi mangapi kuiangamiza CUF kiasi kwamba leo hii waaminike kuliko CDM.

Wenye kutazama mbali tulitambua mchezo mchafu unasukwa na bahati mbaya sana CUF ilikubali kutumika kama dodoki.
Ni kwa kiwango gani CUF watajirudi ili kuponya uharibifu uliofanyika, nobody knows tuvute subira.
 
Back
Top Bottom