CHADEMA Jifunzeni kutoka kamati ya Miss Tanzania jinsi ya kuchuja wagombea! Ni aibu kuwa Na mgombe

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
CHADEMA Jifunzeni kutoka kamati ya Miss Tanzania jinsi ya kuchuja wagombea! Ni aibu kuwa Na mgombea wa kudumu, asiyeshindanishwa.

Kamati ya Miss Tanzania chini ya Hashim Lundenga inakizidi CHADEMA katika utaratibu wa kuchuja na hadi kupata mshindi wa ulimbwende…katika kipindi cha takribani miaka 20 hushirikisha mabinti kutoka mikoa zaidi ya 20 kuanzia vitongoji, wilaya,mikoa hadi taifa ili kuwachuja na kupata bora kulingana na kanuni wakati CHADEMA wanateua mtu mmoja anayepitishwa na kura za wazi bila ushindani,ni dhahiri kuwa wanalipa suala la mgombea uraisi wepesi usio mithilika.

Sifa kubwa ya Mgombea uraisi yapaswa kuwa uadilifu na uchapakazi na sio kujulikana kama Mbowe alivyowaaminisha watu…’hatuwezi kumuacha mtu mwenye wapiga kura milioni moja’..ni dhahiri kwa Mbowe na CHADEMA siasa si huduma bora kwa wananchi bali ni vita ya kuchukua madaraka na kufanya yao. Usipokuwa na mfumo mzuri wa kuchuja ndio sasa tulishuhudia mafisadi wakiuzwa kwa kisingizio cha kujiuzulu ili kulinda chama.Hapa ndipo ninapowashauri CHADEMA kuiomba kamati ya Miss Tanzania iwafudishe jinsi ya kuchuja wagombea wa nafasi mbali mbali kuanzia mashinani hadi Taifani na sio kuokoteza. Nafasi ya uraisi ni kubwa na ni kioo cha nchi ni lazima tuweke mtu mwenye maoni na mwenye kufiukiria wananchi na sio kufikiria tumbo lake na genge lake. ‘A politician thinks of the next election; a statesman thinks of the next generation’. ~James Freeman Clarke, Sermon.

Kama mnaona aibu kujifunza kutoka CCM, umefika wakati mkawapa kandarasi hiyo kamati ya Miss Tanzania wawafunde na msione haya.
 
Hesabu ni masaa mangapi yamepita baada ya kupost huu uzi wako na wachangiaji ni wangapi? Uzi wa kipuuzi kabisa
 
unachangia upuuzi,mimi nafurahi watu wasome na kupata chakula cha ubongo....na wewe umepata hongera.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom