Chadema jaribuni sasa kuwaonyesha wananchi nini cha kufanya kabla ya kuingia madarakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema jaribuni sasa kuwaonyesha wananchi nini cha kufanya kabla ya kuingia madarakani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Sep 10, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tumeona kasi na ukuaji wa chama cha CHADEMA,kiukweli kasi yake ni kubwa na haishikiki.Hujuma nyingi wanafanyiwa ikiwa lengo la kukichafua chama na kukivunja nguvu ambayo imekuwa tishio kwa chama tawala.Kasi hii haiwezi kupuuzwa na kuachwa ipite hivi hivi tu bila kuwa na changamoto ambazo CDM lazima iweze kukabiliana nayo.

  Watanzania humu nchini asilimia kubwa wamegubikwa na umasikini uliokithiri,wamekata tamaa ndiyo maana wanaona kimbilio la wakati huu ni CDM.Lakini cha msingi hapa ni kuto kubweteka kwa CDM na kudhani wame concur the world bila kufanyia kazi chanagamoto hizi zinazo wakabili Watanzania maskini.

  Tumeona waziri wa serikali ya awamu ya nne ana kiri bila kutafuna maneno kuwa ule mkakati wa kuondoa umasikini hakufikia malengo yake,lakini hajatuambia nini kilichosababisha MKUKUTA 1 kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa,zidi ya umaskini kuongezeka japokuwa takwimu za makaratasi zinaonyesha umepungua kwa asilimia 2.6%.

  Nchi ina lalamika,watu wake wanalalamika,serikali ina lalamika,wqasomi wameshindwa kuonyesha na kutumia taaluma yao ili kuweza kuinusuru nchi na janga hili la kitaifa.

  Kwakuwa hata watawala hawajui tatizo la umasikini wetu ni nini kiasi cha Watanzania kupoteza imani na chama tawala na kuamua kuhamishia nguvu za zote na matumaini yao kwa CDM,basi tunaishauri CDM ionyeshe njia kwa vitendo kuliko maneno ya majukwaani kuwakomboa Watanzania kivitendo zaidi kuliko maneno.

  Programme ya kwanza ya MKUKUTA haijafikia lengo,je nini plan B ya CDM ili kuweza kufikia malengo ya MKUKUTA.Pili kwa kuwa CDM wamejenga imani kwa wananchi na wananchi kuunga mkono harakati za M4C harakati hizo kwanini zisitumike sasa kwa kutengeneza mazinigra rafiki kwa shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kujenga hospitali zenye tija na kuboresha elimu kwa watoto wetu.

  Changamoto ni nyingi ila support hii ya wananchi isiwafanye mbweteke kiasi cha kusahau matatizo ya Watanzania,kwa ushauri huu wa bure utatuweka Watanzania katika nafasi ambayo tutaamini CDM ndiyo kimbilio letu.Tunajua kweli hamna vyanzo vya mapato lakini mtaji mkubwa wa rasilimali watu mliojivunia katika operation Sangara kwa kuwavua gamba na kuwavalisha gwanda.

  Mkakati huu ikiwezekana uitwe okoa uchumi wetu tunza rasilimali zetu.Wananchi wapo tayari kutumia nguvu na rasilimali walizonazo ikiwa tu watashirikishwa katika ujenzi was taifa letu na rasilimali zao.Wakati wa malumbano uimeisha tunataka plan B kuthibitisha mkipewa nchi mnaweza.Anzaeni sasa,tafakarini na chukueni hatua.Nawasilisha
   
 2. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani elimu itolewe juu ya uwepo wa serikali, hapa namaanisha wananchi wanatakiwa kutegemea serikali ifanye nini kwa TANZANIA na sio ahadi 69 kutekeleza 3, au miradi ya kujenga nyuma za walimu 2000 kila mwaka na kujenga 3 kwa miaka mi5. Hapa Watanzania tutaamua kwa kura yenye tija sio rangi za bendera.
   
Loading...