Chadema iwasajili wachezaji hawa dirisha dogo.

Status
Not open for further replies.

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
250
Katika kuelekea uchaguzi mkuu 2015 ambao kama ni mchezo wa soka tungesema ni UEFA Champions League. Ili kujenga timu iliyobora na ya Ushindi ni vyema CHADEMA ingewasajili wachezaji wafuatao katika dirisha dogo la usajili hata kama ni kwa mkopo.

1. Deo Filikunjombe (Timu - CCM, Ludewa). Huyu hana tofauti na kiungo wa Chelsea Eden Hazard. Kama jina lake lilivyo kweli huleta madhara anapokuwa uwanjani muda wote. Deo amekuwa hatari hata kwa timu yake Bungeni. Amekuwa jasiri kutamka wazi kuwa viongozi wa timu yake CCM wamevaa miwani ya mbao kwa kufumbia kwa makusudi maovu katika jamii.

2. Kangi Lugora (Timu - CCM, Mwibara). Mchezaji huyu hana tofauti na Vicent Kompany wa Manchester City. Huwa Hacheki uwanjani. Ni team captain, anakaba kwa nguvu, hana masihara kwa wachezaji wenzake. mara nyingi amekuwa akipanda kushambulia hasa katika mipira ya kona (bunge la bajeti). Ni mahiri pia kwa mipira ya vichwa (maswali na majibu bungeni). Kangi Lugora akiwa Bungeni utamtambua kuwa ni mbunge wa CCM tu kwa kutofautisha viti walivyokaa CCM dhidi ya wapinzani ila kwa hoja hutoelewa kama yeye ni CCM. Ni mbunge asieogopa kusema chochote na kwa yeyote. Kaonesha ujasiri mkubwa kusimamia hoja ya kumg'oa Pinda. Utampenda Lugora kwa Confidence aliyonayo.

3. Edward Lowasa (Timu - CCM, Monduli). Hili ni Jembe uwanjani. Lowasa anasakata kabumbu mithili ya Luis Suarez wa Liverpool. Ni mchezaji anaeweza kucheza timu yoyote duniani. Hajali anacheza na wachezaji gani. Akiwa peke, kwa juhudi binafsi huweza kubadili matokeo muda wowote na kupata ushindi. Yeye ni sawa na Jeshi la mtu mmoja. Licha ya utukuku wake bado mashabiki wake wanaendelea kumpenda maana mazuri anayoyafanya huwasahaulisha madhambi yake yote aliyowahi kuyafanya nyuma kwa kuwapa raha ya ushindi.

4. John Pombe Magufuli. (Timu - CCM, Chato). Huyu staili yake hana tofauti na Iniesta wa Barcelona. Ni mchezaji mzuri japo ni vigumu kujua rohoni anawaza kitu gani. Ni mchezaji anaefuata kanuni na sheria. Licha ya umri kuwa mkubwa bado anakipaji cha hali ya juu. Magufuli akisajiliwa Chadema atapewa mazoezi binafsi kwanza ili awe fiti zaidi mara baada ya kutetereka katika ujenzi wa Kilwa road ( Mbagala) na ile ya Mwenge - Tegeta ambayo imeonekana kumsumbua kuchukua maamuzi mazito.

Huu ni usajili wa dirisha dogo ambao hutoa fursa kwa timu kusajili wachezaji wachache tu. Iwapo watahitaka wengine zaidi basi nao watasajiliwa kwenye majira ya joto mwakani. Najua kuna wachezaji wachache ndani ya Chadema wanatakiwa kutolewa kwa mkopo kwenda timu ndongo kama NCCR, CUF ili kwenda kufanya mazoezi ya nguvu kurudisha vipaji vyao, kwa sasa wanaonekana kushuka viwango. Hawa ni pamoja na Kitila Mkumbo.
 

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
May 24, 2013
1,047
2,000
Ulianza vizuri ila pale kati na mwisho umeharibu kabisa. Toa lowasa weka Ester Bulaya(viti maalum),toa Magufuli weka Luhaga Mpina(kisesa). Halafu chadema iwatoe bure John shibuda na Zitto kwenda Magambani.
 

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,668
2,000
julius mtatiro - CUF
Kangi lugora - CCM
Deo filikunjombe - CCM
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom