Chadema itoe Tamko kuhusu Tanesco, EWURA; Wizara ya Nishati/Madini na dira ya Taifa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema itoe Tamko kuhusu Tanesco, EWURA; Wizara ya Nishati/Madini na dira ya Taifa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Not_Yet_Uhuru, Dec 22, 2010.

 1. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  TANESCO ni nini? EWURA ni nini? na Nchi yetu inapelekwa wapi na Taasisi hizi??

  Ni hali ya Masikitiko makubwa, Uchumi unavurugika, Wananchi wanazidi kudidimia ktk dimbwi la kukosa huduma, ziwe za muhimu hasa zile zinazotegemea uzalishaji mdogo mdogo kwa kutumia nishati ya umeme kama ujasiriamali, huduma za mahitaji ya vyakula na vinyaji baridi mfano maziwa, maji, samaki, nyama nk. Ajira binafsi kama saloon, uchomeleaji nk; Vyote hivi vimekuwa vikitegemea sana mahitaji ya umeme ijapokuwa umekuwa ukipatikana kimkanda-mkanda, ila watanzania wamekuwa wakivumilia tu na kujiendeshea maisha yao ya kuokoteza na kujikwamua kiujasiriamali.

  Kitendo cha Tanesco kuvurunda tena ktk usimamizi wa mitambo kuwa eti baadhi kusemekana umeharibika, na kusasabisha adha kubwa kwa Taifa nzima kwa kukata umeme kila mara ni aibu na jambo ambalo limekuwa likitokea kila mwaka na kila wakati bila wahusika kuwajibika bali wao huachiwa tu kutoa 'ufafanuzi wa kisanii' ambao mara nyingi ni 'porojo tu za kujilinda nafasi zao na maslahi wa waliowaweka madarakani'. Haifai tena!

  Hii ni dhuluma, na usaliti mkubwa mno kwa taifa na wananchi wanaohangaikia maisha yao kila kukicha. Wanavutwa nyuma na utendaji uliooza, na Hakuna maendeleo yoyote kwa mtindo huu. Nchi itazidi kuangamia kwa umaskini sababu ya watu wachache wanaolindana.
  Watanzania wanahitaji dira na Mwelekeo wa hali hii. Na EWURA pasipo kujali maisha ya wa tanzania yanavyodhoofika, nao wamekubali msukumo wa TANESCO kuongeza bei ya huduma za Tanesco kuanzia mwakani. EWURA ni kwa maslahi ya nani? Tanesco ni kwa maslahi ya nani na ni ya nini Tanzania? EWURA ina maslahi gani kwa Watanzania?

  TUNAIOMBA CHADEMA itoe TAMKO na dira kwa Taifa hili. Na hata kama inafaa itangaze rasmi maaandamani ya Amani kwa nchi nzima kupinga kuangamia kwa nchi yetu! Tanesco ivunjwe na Wahusika wa EWURA na Wizara ya Nishati na Madini wawajibike. La sivyo watanzania kwa kiwango kikubwa wanazidi kukata tamaa mno na hawatasikia la yeyote kwamba wanaye watetezi wa maisha yao.

  Mungu ibariki nchi yetu. Naomba kuwasilisha.
   
 2. r

  roby m Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Kuna watu hawapendi maendeleo ya nchi hii!!!!!! hivi kama Tanesco imeshindwa kwa nini yasiruhusiwe makampuni ya watu binafsi ili kuendesha usambazaji wa umeme nchini. Hii yote ni sababu ya serikali ya kifisadi.
  Tanzania!!! we 'r crying coz of our own decision may God help us.
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
 4. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  In short ewura hunufaika na pato la asilimia moja la gharama anazotozwa mteja, kwahiyo kupanda kwa gharama za umeme kutainufaisha euwura as well.
   
 5. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  KAMPUNI MBADALA KWA TANESCO NI NDOTO...NANI ATARUHUSI HILOO??

  Hapo mjomba (VoiceOfReason) kamwe hutafanikiwa!! Labda wafe wananchi wote, 'ndio wenye Tanesco yao' watakosa consumers!

  Hapo Unaingilia Maslahi ya 'Wenyewe'....wanaojilisha kwa kilio cha Watanzania wanapojikokota kila siku kuhangaikia chakula, umeme, kujikimu na pia kodi na gharama za kulipia nishati-umeme isiyokuwepo.

  Kwa taarifa yako; Wapo waheshimiwa wanaoamka kila asubuhi, jicho lao lote lipo kwa Tanesco na wanaulizia maswali kadhaa kuizunguka Tanesco unayodhani ipo kwa ajili ya mwananchi anayelala-hoi..! mfano: Haya yaweza kuwa ndio wanayojiuliza wenye-meno, wanaomiliki 'Mradi wao huo'!

  • Mradi wangu wa Luku umeingiza ngapi leo au utaingiza ngapi mwezi huu?
  • Lile fungu la kupeleka kwa IPTL, ya kwangu imeingia ktk account?
  • Na Dowans yale masuala ambayo Tanesco wanatakiwa watugawie yamewekwa vyema?
  • Na malipo kwa Songas, mgawo 'wetu' umeendaje mwezi huu? Account zitacheka?
  • Na wale jamaa wa Makampuni makubwa yanayotumia sana umeme (kama uzalishaji wa saruji), jamaa wanajikoki..je yale mafungu yetu wameshatugawia mwezi uliopita kwa kuwapa unafuu wa bili?? n.k.
  Mjomba; Ukitafakari trend hii na nyingine ambazo zimeshaandikwa ktk media kadhaa, utagundua kuwa kubinafsisha au kuleta kampuni mbadala kwa Tanesco ni ndoto na ni jinamizi kwa makundi ya wabinafsi wanaofaidika na mirija na mianya iliyotoholewa hapo juu...

  Nchi yetu inakwisha...Tunahitaji ukombozi...Tunahitaji Taifa jipya, Watendaji wapya na dira mpya!!!

  Mungu Tuokoe...au ije kwetu Wikileaks!
   
Loading...