Chadema itengeneze vipeperushi ya hotuba ya tundu lissu vigawiwe kwa umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema itengeneze vipeperushi ya hotuba ya tundu lissu vigawiwe kwa umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lu-ma-ga, Nov 15, 2011.

 1. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Nimesoma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyowasilishwa bungeni jana na mh.Tundu Antiphas MughwaiLissu (MB)
  kwa hakika nimesoma between the lines, imenisisimua sana na kunielimisha mambo mengi ambayo sikuyajua na leo nimeelewa ni kwa nini mchakato huu uliowasilishwa bungeni kuwa ni mauzauza ya kifisadi.

  Nimejifunza kuwa CCM hawana nia ya kuandika katiba mpya bali wanatafuta sababu za kuchelewa process kwani hiyo si SERA YAO.Katiba mpya ilikuwa SERA ya CDM na ni bora ikaendelea kuwa CDM hadi hapo katiba itakapopatikana na leo nimehamasika kiasi kwamba niko tayari kuandamana kupinga huu mswada, kama waandamanaji watafikia idadi ya 1,000,000 basi mimi nitakuwa wa 1,000,001.

  Ombi langu kwa CDM ni kwamba inabidi muingie gharama kutengeneza VIPEPERUSHI vya kutosha kwa nchi nzima ili WATANGANYIKA waelewe.

  Mh.Lissu amesema vizuri sana juu ya Tanganyika; bado tunakubaliana na kwamba "ni ujinga kudhani kwambaVisiwa vya Zanzibar vitaendelea kuwa na maamuzi na ushawishi mkubwa katika masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika kwa sababu utaratibu wa asili haujawahi kufanya maslahi ya Visiwa hivyo kuwa bora zaidi ya maslahi yaTanganyika!"

  Nawasilisha

   
Loading...