CHADEMA itashindwa tena Kinondoni na Siha kwa sababu ya Mbowe kuendelea kuidharau Kamati Kuu

Benson Mramba

JF-Expert Member
Oct 29, 2013
644
1,482
Katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichoketi December 2017 pamoja na kujadili sababu za kupoteza kata zote 43 katika uchaguzi Mdogo pia Mbowe alishinikiza Chama kisishiriki uchaguzi Mdogo wa majimbo ya Singida Kaskazini na Songea Mjini uliofanyika January 2018. Nasema aliishinikiza Kamati Kuu kwasababu hakuruhusu mjadala juu ya pendekezo hilo na pia hakuruhusu kura. Alitumia kura ya Veto ambayo ndani ya Katiba ya Chadema Mwenyekiti hana mamlaka ya Veto isipokuwa tu kama kura za wajumbe wa Kamati Kuu zitakuwa zimegongana katika uamuzi wa jambo fulani.

Ubabe huu wa kutoshiriki Uchaguzi ulipingwa na Wanachama wengi, Viongozi wengi, wakereketwa kama sisi, baadhi ya viongozi wakuu na hata Katibu Mkuu Mashinji aliupinga kwa nguvu zote. Pamoja na sababu za uongo zilizotolewa na Mbowe kwenye kamati kuu na mbele ya vyombo vya habari kuwa ndio chanzo cha kususia uchaguzi ule, tunaojua ukweli tuliandika kuwa sababu ni ukosefu wa fedha na imethibitika hivyo.

1. Aidha Kamati Kuu hiyo hiyo ya Desemba 2017 iliazimia kuwaondoa kwenye nafasi zao Vijana wawili wa Mbowe ambao nimekuwa nikiwasema tangu mwaka jana kuwa hawana uwezo, hawana ubunifu, wafitini ndani ya Chama, Waongo na wapika Majungu ndani ya Chama. Vijana hapo ni John Mrema Mkurugenzi wa Uenezi, Itikadi na Mambo ya nje pamoja na mwenzake Reginald Munisi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi, oganaizesheni na Wanachama.

Hoja ya Wajumbe wa Kamati Kuu ilikuwa ni kuwa Vijana hawa hawatoshi katika nafasi zao, wanakula mishahara makubwa ya bure tu (Milioni 2.5 ) ndani ya chama na ndio sababu ya CHADEMA kushindwa uchaguzi katika Kata zote 43 wakati ule. Mbowe alijitahidi kuwatetea sana ila hakufanikiwa. Matokeo yake Mashinji akaahidi kutafuta mahali pa kuwafix. Tangu Desemba mpaka leo hakuna kilichofanyika na Vijana hao bado wanaendelea na majukumu yao na kuendelea kumshughulikia kila wanayehisi ni adui yao.

2. Mwezi january Kamati Kuu iliketi vikao viwili kwasababu ya mvutano wa ama kushiriki uchaguzi huu wa Kinondoni na Siha au kususia. Mbowe na vijana wake waliendelea kusisitiza chama kisusie. Kikao cha kwanza Kura zikapigwa wajumbe waliokuwa wamepangwa wakakataa kushiriki uchaguzi ila kura Tatu zikaharibika na Katibu Mkuu hakuwepo pamoja wajumbe wengine wachache waliokuwa wanataka Chama kishiriki uchaguzi.

Kikao cha pili cha Kamati Kuu cha january kiliitishwa siku chache baadae ili kuona kura zilizoharibika na kuhakikisha wajumbe wote wanakuwepo pia kuona kama chama kitapata wagombea. Katika kikao hicho kura zilipigwa tena na Mbowe na vijana wake wakashindwa kwa kura.

Mbowe akataka kutumia ubabe tena kuzuia chama kisishiriki uchuguzi ndipo baadhi ya wajumbe wakiwemo wa Meza kuu akiwemo mgombea wa Kinondoni wakamtuhumu Mbowe kupokea rushwa ili kukizuia chama kisiende kwenye uchaguzi ili kuisaidia CCM.

Kama ilivyodesturi yake akitaka kushinikiza jambo lake Mbowe baada ya kuona kamati kuu inamtuhumu akaamua kujiuzulu ili kuwatisha wajumbe. Ikabidi Lowassa, Sumaye, Ntagazwa na Baregu waombwe wambembeleze. Kishingo upande akakubali kushiriki uchaguzi.

Kwa tunaomjua Mbowe kutokana na mvurugano huo lazima atakuwa kamuwekea mtu kisasi. Na siku za karibuni tangu baada ya figisu za kupata wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki Salum Mwalimu ni miongoni mwa wapinzani wakubwa wa Mbowe. Na Mbowe anamshughulikia kupitia Vijana wake.

Dharau ya Mbowe kwa Kamati Kuu na matokeo tarajiwa.

1. John Mrema na Reginald Munisi bado wanaendelea na Kazi kwenye Kurugenzi ile ile na Kitengo kile kile. Alichofanya Mashinji ili kuidanganya kamati Kuu ameweka Ma Operation Kamanda wengine ambao wanaripoti kwa vijana hawa ili kusubiri upepo mbaya upite.

Ushauri wangu kwa Dr. Mashinji ni kuwa Vijana hawa watamuharibia Kazi na watamchonganisha na Mbowe na Chama kwa ujumla siku si nyingi au huenda wameshaanza maana majungu na fitina ndio mtaji na maisha yao.

Hivyo basi Mimi sitarajii matokeo tofauti kutoka kwa watu wale wale wenye uwezo Mdogo kama John Mrema. Kamati Kuu pamoja na udhaifu wake nayo ilishawapima na kuona hawafai.

2. Sina hakika sana kuhusu kinachoendelea Siha ila kuhusu Salum Mwalimu najua wazi kuwa wenzie wote katika Sekretarieti ya Chama makao makuu hawataki ashinde kwasababu hawampendi na yeye analijua hilo.

Hata kuteuliwa kwake ni kwasababu waliogopa kumkera baada ya walichomfanyia kwenye uteuzi wa wagombea wa ubunge wa Africa Mashariki. Naamini siku moja atakuja kusema hadharani vita aliyonayo ndani ya Chadema. Hivyo Mbowe, John Mrema na Regy hata Mashinji mwenyewe hawamtakii ushindi. Akishinda ni jitihada zake binafsi though nampa 25% kushinda.

3. Mbowe anataka Chama kishindwe ili kupata uhalali wa maamuzi yake ya kutokushiriki uchaguzi wa January na pia kujisafisha juu ya tuhuma za kuhongwa katika kamati kuu ya juzi.

Mwisho niseme Chadema itaimarika baada ya kufanya mabadiliko ya uongozi na kuienzi misingi ya demokrasia iliyoasisiwa na waasis wa Chama. Wabunge wa CHADEMA wana wajibu Mkubwa katika kulisimamia hili kwa maslahi yao binafsi 2020 na maslahi ya Chama kwa ujumla.

Aidha baada ya matokeo nitamuomba Mbowe ajipime kama bado anatosha kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Chama asisubiri Chama kimfie kabisa mikononi mwake.

Imani YANGU ni kuwa wote wanaohama ni wale ambao Mbowe na mtandao wake wanawashughulikia. Ubaya ni kwamba wana elimu ndogo, uwezo Mdogo na hofu nyingi.

CHADEMA ina tatizo kubwa ndani kuliko nje hivyo tulitatue kwanza.

Nitarudi baada ya matokeo ya uchaguzi.
 
Propaganda zimeanza
 
Huu ni upuuzi kwelikweli,inamaana na vyama vingine vya upinzani ambavyo kila kukicha vinarudi nyuma,je MWENYEKITI wao ni Mbowe?Kwahiyo akija mwenyekiti mwingine unyanyaswaji wa upinzani utakwisha?Je mikutano ya hadhara itaruhusiwa?Tume ya uchaguzi haitaleta tena figisufigisu?Acheni mawazo mgando,maana haiingii kichwani eti mwana ccm anataka chadema iwe na uongozi imara.Hii ni fikra ya kuwaeleza watoto wa chekechea na misukule.
 
Democracy ni mgongano na mpambano wa fikra, utaalamu na mitazamo. Ndg Benson jifunze kupokea mawazo yanayotokana na majadiliano ya vikao halali. Itakusaidia sana kukua kisiasa. Ukipenda kuona mitazamo yako ndio safi kila wakati wewe ndie unaepwaya. Amen.
 
Me nadhani CCM mngependa Chadema wangesusia Uchaguzi ili Mshinde bila usumbufu.Kama kweli mnajiamini,Mngeomba Kura mpaka kwa kupiga Magoti??!.Hakika kukiwa na Uwanja huru wa Kuchezea Hamtaambulia chochote kwenye Uchaguzi huu.Na Kushiriki Uchaguzi ni Muhimu ili kutambua Makosa yako na Nguvu yako pia.Kutoshiriki Uchaguzi uliopita kumefanya kilio chao na Malalaniko yao yasikike na Watu wamejua kilichofanyika.Ni hayo tu
 
Mmeshaanza majungu, watu kama nyie kinachowaumiza ni tamaa ya vyeo ndani ya chama, sasa hapo unaona Mrema na Munisi wanafaidi sana kulipwa hiyo 2.5mil, unawatolea macho, au umeambiwa akiondolewa mmoja utawekwa wewe? Nyie ndio mnaosababisha migogoro ndani ya chama.

Nenda CCM, huko Magu anagawa vyeo kiholela, Dr.Slaa ameapishwa leo, anaenda kula bata na watoto wa Ki-Swedish.
 
Back
Top Bottom