Chadema Itapendeza Zaidi Mkiteua Mgombea Urais Kutokea Upande Mwingine Wa Nchi!

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wasalaam Wana wa Jamii Forum
Nimekuja na ushauri kwa Chadema jinsi gani wanatakiwa wajipange mapema kwa ajili ya mchakato muhimu wa uteuzi wa mgombea Urais kupitia chama hicho tayari kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2020.
Itapendeza sana hii wakiteua mgombea kutoka upande mwingine wa dunia badala ya kila mara kuteua mgombea kutoka upande mmoja tu wa dunia!
Zipo faida nyingi za ushauri huu endapo utafanyiwa kazi ikiwemo kuondoa dhana ya muda mrefu kuwa chama hicho ni cha ukabila na pia itaongeza idadi ya wanaokiunga mkono.
Aidha uamuzi huo utasaidia kukijengea chama hicho 'uhalali' wa kukabidhiwa dola ikitokea wameshinda uchaguzi kihalali. Vinginevyo naona safari ya kuelekea Ikulu itabaki kuwa ndoto!
Sio vibaya mkachukua mfano wa Chama Cha Mapinduzi kwenye uteuzi wa Wagombea Urais ambao kihistoria wametokea pande zote za dunia!
Aksanteni
 
Tulianza uchagani,tukaenda mbulu then umasaini,bado upareni,umeruni na umang'atini.then tutakuja huko kwingine
 
Kaskazini tutaendelea kutoa wagombea toka kwetu tu,
Na tukichukua nji lazima kaskazini tuiangalie kwa jicho la kipekee.

Na Lowasa asipoongeza pesa tunawondoa kugombea na kuweka wachaga tu.
 
Back
Top Bottom