CHADEMA isimezwe na kesi za uchaguzi...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
CHADEMA ni chama makini. CCM ni chama tawala.Sifa hizo mbili zinavitofautisha vyama hivi na kuonyesha nguvu zao.CHADEMA ina safari ndefu ya kuikomboa nchi hii.Ijikite kwenye kutekeleza ahadi zao kwa wananchi kwa yale Majimbo inayoyaongoza.Isipelekeshwe na kesi za uchaguzi.Wananchi hawatapima,mwaka 2015,nani alishinda kesi wapi bali nani katekeleza nini.Mwenye masikio na asikie...
 
Tambua kuwa kutetea haki za wanyonge mahakamani na popote pale ni ahadi za CHADEMA. CHADEMA inaongozwa na watu ambao wana upeo, wanatambua mbinu zinazochezwa na serikali ya CCM. Hawako tayari kutekwa akili na mpumbavu yeyote!
 
Tambua kuwa kutetea haki za wanyonge mahakamani na popote pale ni ahadi za CHADEMA. CHADEMA inaongozwa na watu ambao wana upeo, wanatambua mbinu zinazochezwa na serikali ya CCM. Hawako tayari kutekwa akili na mpumbavu yeyote!
Nakubaliana na wewe Mkuu.Lakini,nikiwa kama mpenda mabadiliko,nimejaribu kutoa angalizo tu..
 
Amini usiamini. Hizi kesi nazo, zilizofunguliwa na CDM na zile zilizofunguliwa na CCM, zote zina mchango wake katika kuipaisha CDM.
 
Ushauri wangu

Hizi kesi za uchaguzi (kupinga matokeo ya ubunge) zina nafasi ya kutetea waliopokwa ushindi kusudi haki itendeke. Upande wa pili ni gharama kuendesha chaguzi za marudio kwa maana ya muda na resources kama fedha, manhours etc.

Ni kweli kwamba HAKI ina GHARAMA lakini ni busara pia kupima matokeo kwa kuweka balance. Mambo mengi ya serikali yanakwama kwasababu ya ukosefu wa fedha (zimekwenda wapi wao ndio wanajua) na tukubali tukatae uchaguzi ukirudiwa bado fedha kidogo iliyopo hazina itaishia huko na maisha ya watanzania yataendelea kuwa duni kwa miradi kutokukamilika au kufanyika kabisa, madawa kuendelea kukosekana n.k.

Kwa kuwa idadi ya wapinzani mjengoni haizidi asilimia 20 hata upinzani ukapata viti kumi vya ubunge impact yake mjengoni inaweza isiwe kubwa.

Kwa hali hiyo basi ni vyema wale waliofungua kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa withdraw malalamiko yao (kama yule wa mbozi alivyofanya) na badala yake nguvu na resources zielekezwe kwenye kutoa elimu ya uraia na kujenga chama (call it M4C or anything similar). Miaka takriban mitatu iliyobaki kabla ya uchaguzi mkuu sio muda mrefu.

Ni mtazamo tu..... without prejudice!
 
Kweli mkuu, hivi kuna chama kingine tofauti na chadema ambacho viongozi wake na wabunge wengi wana kesi mahakamani?.
.
"Ama kweli CHADEMA NI SAWA NA NG'OMBE ASIYE NA BEI SOKONI".
 
Back
Top Bottom