CHADEMA isibezwe! CCM wanatanga na nyika

Ikifikia hatua adui ama mpinzani wako anaacha kutumia ngumi na badala yake anaamua kutumia nyenzo za kumsaidia ushindi kama bisibisi, mawe, mayai viza, viwembe nk basi ujue ugomvi huo ushaumaliza ni kiasi tu cha kuwa na subira tu.
 
Hakuna nia ya dhati ya kuwasaidia wanaonunuliwa kwakuwa ccm sio malaika wasahau mara hii kuwa hao wanaowachukua ni watu ambao hapo mwanzo walikiponda sana hiki chama... Kinachafanyika sasa hivi ni MBINU YA MWISHO KUIVURUGA CHADEMA baada ya nyingine zote kushindwa
Kivurugwe tu kwani kinafaida gani ?
 
Subiri msimu wa manunuzi uishe... Ni kipindi cha mavuno ngoja kipite tutafanya tathmini hapahapa kwakuwa ndio barazani kwetu
ccm hawajaelewa bado. Chadema wanawachezea akili hahahhhhh Chadema wanajua linaloendelea watachukua pesa watasepa. Angalisho kwa Chadema kwa mtindo huu itakuwa vigumu sana wananchi kuwaamini. ccm mazozo kwelikweli mtu atachukua pesa halafu atakaaa kimyaaaaaa mtakuwa mmevuna mabua ya mahindi.
 
Machaliii wa RCHUNGA wanapotoka mererani wale wana Apolo huwa ni msimu wa mavuno kwa machangu wote wa Arusha... Pesa kitu gani bwana hasara roho... Kipindi hiki machangu huhamishia mapenzi feki yote kwa wana Apolo... Lakini wakiwa na maisha yao na wapenzi wao wa moyo.... Wanaaopolo wanapopunwa pesa zote hukimbiwa nao kuukimbia mji na kurudi chaka kutafuta tena.. Huwaachia faida tupu machangu...
Changu ni changudoa yani mwanamke aso na bwana mmoja
Kuna wimbi kubwa sana la wanaupinzani NOTABLE kuhamia CCM... Naambia wanajipangia dau... "Sema unataka bei gani, lakini nakuhitaji sana... " ofa hii inachangamkiwa sana.. Lakini je haya ni mapenzi ya kweli? Muda utasema...
Wanaohamia wote its all about cash na si vinginevyo, cheo ni urembo tu.. Mtu anaangalia anapata bei gani kwenye nini....
Wengi ni watu wazima wanaojitambua fika.. Waliopitia madhila ya ccm wana makovu, kovu halifutiki wana kumbukumbu, hawajasahau wanakubali kununuliwa sasa hivi ili kulinda mishe zao usalama wao na mustakabali wao.. Wanataka kupumua kidogo... Kupumzika kidogo

Wengi wanatambua kuwa wanachopewa kama cash kinaweza kuwa final wasipate cheo chochote... Lakini bora liende.... Muda ukifika watarudi kwa magoti na msamaha na watasamehewa...
Vyeo wanavyoahidiwa kuna maelfu ya wanaccm wanavililia wanalitambua hilo.. Hivyo tusiwachukulie poa....
Kwanini CHADEMA iko kimya? Haijapata taharuki wala kubabaika? Wanajua kucheza na wakati... Wanatambua wazi kuwa UONGO HUPANDA LIFE LAKINI UKWELI HUKWEA NGAZI...
kutangulia si kufika na ujanja ni kupata sio kuwahi... Wanaoenda ccm baadhi ni mapandikizi.... Kilio kitakachoenda ccm kitaacha simulizi za muda mrefu ujao... CHADEMA haitanunua itapokea kama walivyo... Utawala utakapofitinika....
Ukimya wa CDM una kishindo kikuu... Wasibezwe
Kuna kitu huwa napata nacho shida sana katika siasa hizi za Tanzania... kwanini Demokrasia huwa haithaminiwi hususan katika sula zima la mtu kujiamulia chama anachotaka kwenda. Tunasahau siku zote SIASA NI MASLAHI. Mwanasiasa yoyote kabla ya kuamua kwenda chama fulani ni lazima aangalie kwanza MASLAHI yake KISIASA. Lowassa asingehama CCM kama MASLAHI yake KISIASA yangezingatiwa, lakini tumeona alivyohamia CDM kufuata kile alichokikosa CCM. Bulaya asingehama CCM kama angekua ana uhakika wa kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika jimbo la Bunda Mjini Uchaguzi wa 2015 nafasi aliyokua akiitaka kwa muda mrefu, lakini alivyoona Bw. Wassira bado amemkalia kooni akaamua kuhamia CDM na tumeona jinsi MASLAHI yake ya KISIASA yalivyozingatiwa baada ya kupewa nafasi hiyo. Halikadhalika, Lembeli katika jimbo la Kahama Mjini alivyoona nafasi yake ilikua finyu sana kushindana na Kishimba CCM, akahamia CDM na kupewa nafasi hiyo, ingawa alishindwa kupata ridhaa ya Wananchi. Tujiulize hizi nafasi zote hapakua na wana CDM (MAKAMANDA) ambao wangeweza kupatiwa nafasi hizo? tena Makamanda waliokua wakikipigania chama wakati kina Bulaya na wenzao wakiwa CCM wanakula bata. Nyalandu leo amejivua ubunge na nafasi zake zote ndani ya CCM na kuhamia CDM, tujiulize angekua kwenye CABINET ya Magufuli angeweza kufanya hivyo? Mifano ni mingi sana kuhusu uhusiano uliopo kati ya SIASA NA MASLAHI.

Sasa hali kama hiyo ndiyo inayotokea kwa sasa, upepo wa kisiasa umebadilika kila Mwanasiasa sasa anaangalia wapi MASLAHI yake KISIASA yanaweza kuzingatiwa. Wengi wetu hatujui nini kinaendelea kwenye vyama vyetu hususan vya Upinzani, wapo wanaolalamika kwamba kwenye baadhi ya Vyama hakuna fursa na hata zikijitokeza wanaofaidika ni wachache ambao wameshika mpini. Wapo pia wanaolalamika kutumika kuvijenga vyama hivyo lakini michango na mawazo yao haithaminiwi. Wapo wanaolalamika kuhusu itikadi zinazosimamiwa na vyama hivyo kutojulikana kwa sasa na hivyo kushindwa kujijenga kisiasa.

Kwahiyo ukiangalia utaona sababu ni nyingi sana zinazowapelekea wanasiasa kuhama Vyama. Sasa inashangaza watu badala ya kuangalia sababu hizi za msingi wanakimbilia kusema wananunuliwa.Mbona Mbowe, Lema, Msigwa, Mdee hawanunuliwi? Hata kama kweli wanasiasa wanaohama vyama wananunuliwa lakini tujiulize what is the motives behind? Jana Kambaya wakati anaongelea suala hili la wanasiasa kununuliwa alisema hoja ya msingi sana, kwamba hakuna biashara isiyo na mnunuzi na muuzaji. sasa tuangalie tatizo lipo kwa mnuuzi au muuzaji? Mwisho wa siku POLITICS IS ABOUT WHO GETS WHAT, WHERE AND WHEN?
 
Yani hiki ndo umeandika tangu asubuhi uko online
Machaliii wa RCHUNGA wanapotoka mererani wale wana Apolo huwa ni msimu wa mavuno kwa machangu wote wa Arusha... Pesa kitu gani bwana hasara roho... Kipindi hiki machangu huhamishia mapenzi feki yote kwa wana Apolo... Lakini wakiwa na maisha yao na wapenzi wao wa moyo.... Wanaaopolo wanapopunwa pesa zote hukimbiwa nao kuukimbia mji na kurudi chaka kutafuta tena.. Huwaachia faida tupu machangu...
Changu ni changudoa yani mwanamke aso na bwana mmoja
Kuna wimbi kubwa sana la wanaupinzani NOTABLE kuhamia CCM... Naambia wanajipangia dau... "Sema unataka bei gani, lakini nakuhitaji sana... " ofa hii inachangamkiwa sana.. Lakini je haya ni mapenzi ya kweli? Muda utasema...
Wanaohamia wote its all about cash na si vinginevyo, cheo ni urembo tu.. Mtu anaangalia anapata bei gani kwenye nini....
Wengi ni watu wazima wanaojitambua fika.. Waliopitia madhila ya ccm wana makovu, kovu halifutiki wana kumbukumbu, hawajasahau wanakubali kununuliwa sasa hivi ili kulinda mishe zao usalama wao na mustakabali wao.. Wanataka kupumua kidogo... Kupumzika kidogo

Wengi wanatambua kuwa wanachopewa kama cash kinaweza kuwa final wasipate cheo chochote... Lakini bora liende.... Muda ukifika watarudi kwa magoti na msamaha na watasamehewa...
Vyeo wanavyoahidiwa kuna maelfu ya wanaccm wanavililia wanalitambua hilo.. Hivyo tusiwachukulie poa....
Kwanini CHADEMA iko kimya? Haijapata taharuki wala kubabaika? Wanajua kucheza na wakati... Wanatambua wazi kuwa UONGO HUPANDA LIFE LAKINI UKWELI HUKWEA NGAZI...
kutangulia si kufika na ujanja ni kupata sio kuwahi... Wanaoenda ccm baadhi ni mapandikizi.... Kilio kitakachoenda ccm kitaacha simulizi za muda mrefu ujao... CHADEMA haitanunua itapokea kama walivyo... Utawala utakapofitinika....
Ukimya wa CDM una kishindo kikuu... Wasibezwe
 
Yanarakiwa mawazo mpya ndani ya CHADEMA. Mbowe akaye pembeni Na kuchagua mwenyekiti mpya Na karibu mpya.
1, kuna madini mengi sana chama ni.
2, Wazabuni eti ni mbowe mwenyewe. 3, Marahemu anadai pesa zake za choppar. Tangu zamani Na familia wazihitaji. Kulipia kodi ya chappor Na Svs.
 
Haya!!wakati tunaisubir chadema na ccm kujua mbivu na mbichi,ndio tunaendelea kumsubir YESU maana anakuja
 
Ndg. Mshana Jr. Unaweza kwa nafsi yako ukasema walipohamia Chadema waziri wakuu wastaafu wawili nao walinunuliwa na chadema?
 
Siasa &mtazamo wako finyu wa kikaskazini ndo unaokupotosha!usidhani wote ni nyumbu!
Unamuita wa kaskazin kwakuwa amejiita mshana ? Kwani kuwa wa kaskazin ni dhambi ckiz? Hivi ww na mtoa uzi nani anastahil kuitwa nyumbu? Mwenzio amechambua wewe unatoa vijimaneno vya kebehi ili uonekane mzalendo wa kuchonga!? Ndo maana nyufa kwenye maghorofa mnasema ni jamnbo la kawaida huku mkijidai wajuzu wa mambo msioambilika? Jiulize kama kweli mnajenga Tanzania mpya kwanini mnatumia nguvu nyingi kuwafanya watu waone na kukubali mnayoyafanya ? Mmekataza mikutano ya vyama vya siasa, magazeti mmefugia na sasa mnaingiza nchi hasara kwa kufanya siasa chafu za kununua wabunge na madiwani ili tu kina polepole wafurahi. Huu ni unafiki na dio unyumbu wenyewe kama hujui
 
Hivi kati ya wote waliochukuliwa toka upinzani nani wa maana hapo? Mwigamba? Msando? Katambi? Mtulia? mimi sioni bidhaa safi hapo. Yaani credit waliyokuwa nayo ni ule wasifu wao wa kuwa upande wa upinzani. Leo Katambi hata akiitisha press conference hatavuta attention hata ya wananchi na waandishi wa habari kama alivyokuwa Chadema. Believe me.
 
Yanarakiwa mawazo mpya ndani ya CHADEMA. Mbowe akaye pembeni Na kuchagua mwenyekiti mpya Na karibu mpya.
1, kuna madini mengi sana chama ni.
2, Wazabuni eti ni mbowe mwenyewe. 3, Marahemu anadai pesa zake za choppar. Tangu zamani Na familia wazihitaji. Kulipia kodi ya chappor Na Svs.
Mkuu mbowe hawezi kutoka kirahisi ivo coz tunaangalia maslahi mapana ya chama,unaweza ukawa na mwenyekiti kama la professeri akatumia chama kama mtaji wake wa kupata rupia,mbowe hana iyo hulka ya kuhongwa na sizonje ili atusaliti,he is there to stay
 
Back
Top Bottom