OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 48,757
- 102,104
CHADEMA is my loving, my amazing and my awesome Political Party, I dedicate to Tanzanians
Kwa mtu mwenye mawazo huru atakubaliana na mimi kuwa CHADEMA hii ya kabla na baada ya uchaguzi wa 2010 ndiyo inayotoa muelekeo wa vipi Tanzania inatakiwa kuwa.
Juzi kupitia ITV saa mbili usiku ikaja habari kuwa Makamanda wamekutana kwa dharura kujadili juu ya mustakabali wa nchi. Moyo wangu ukafarijika sana nikajawa na amani. Taswira ya mwenyekiti Freeman Mbowe ikanitia ujasiri sana (hii hunitokea mara zote napomuona Mbowe katika video), nikamuona pia Prof. Baregu na J.J Mnyika wakiwa deep in brainstorming. Baadaye akatokea aliyekuwa mgombea wa UKAWA Ndugu na kipenzi cha Watanzania, mwana-amani Edward Lowasa. Hapo ndipo roho ya uvumilivu na mapenzi ya dhati kwa watu wangu ikanijia. Kwamba ninaweza kudhurumiwa sana lakini ni lazima busara itumike katika kupata haki yangu. Sijawahi kuona mwanasiasa mvumilivu kama Edward Lowasa.
Nikirejesha mawazo yangu katika mkutano wa CCM kumkabidhi Rais Magufuli uenyekiti wa CCM, nikawaonea huruma sana Watanzania. Watanzania wanadanganywa sana na CCM. CCM inatumia ujinga wa baadhi yetu kujinufaisha.
Sasa nikueleze kwa nini naipenda sana CHADEMA
1. Terehe 23 July, 2016 Kikwete na wenzake walikiri kwa dhati kabisa kuwa 2015 ilikuwa chupuchupu. Na nakwambieni magumu ya kumuingiza Magufuli madarakani ni zaidi ya yanayotajwa. Kikwete, Dr.Shein, Jaji Lubuva na Jecha wa Jecha wanajua. Sina uhakika kama wameshamlilia Mungu awasamehe kwa waliyoyafanya. Huo ni muziki wa Chadema unawafanya sasa CCM wajirudi kwa Watanzania.
2. CHADEMA huwa inamuumbua sana Magufuli. Magufuli amekuwa miaka 20 madarakani . Leo anaiambia Tanzania kuwa ni kweli yale yaliyopiganiwa na yanayopiganiwa na CHADEMA ni kweli tupu. Ajabu tu anasahau kuwaambia Watanzania kwa nini hakusema kabla? Kwa nini hakusema haya kabla mambo hayajaharibika zaidi. Pengine majizi yasingekuwa mengi namna hii.
3. Kuna watu walidharau sana harakati za BAVICHA za hivi majuzi kuhusu kupigania haki ya kufanya siasa. Kuna walevi wa madaraka walidiriki mpaka kukataza mikutano ya ndani. Kiko wapi leo wamebana-wameachia, mikutano ya ndani inafanyika na hata mikutano ya wazi inayofanywa na CCM inawaumbua wale wote waliounga mkono katazo la mikutano ya kisiasa. Wanabaki kushangaa tu. Kama si BAVICHA leo ingekuwaje?
4. Wakati watanzania wakijiuliza kulikoni Tanzania ya Magufuli?Mbona hali inakuwa mbaya kila siku kwa kila mtu. Mbona ubabe unakuwa mwingi?, Makamanda wa CHADEMA wamekutana kwa siku mbili kupata majibu ya maswali hayo. Watawapa majibu hivi punde.
5. Wakati CHADEMA na BAVICHA wakipigania haki ya kufanya siasa iliyokatazwa na Rais Magufuli na kuungwa mkono na wanafiki, jana Kikwete anaiunga mkono CHADEMA kuwa viongozi wa CCM wanatakiwa kwenda kuwatembelea wanachama kwenye maeneo yao. CCM inaumbuka.
6. Kuna watu walikimbilia CHADEMA katika uchaguzi wa 2015. Watu wakapiga kelele kwamba wanakuja kukisambaratisha chama. Mbowe ni mtoto wa mjini. Hivi unawezaje kumkatalia mtu asiwe mwanachama, mwache matendo yake na njaa zake vitamuumbua. Njaa imemuumbua Mgana Msindai na Fred Mpendazoe. Walikuja kusaka vyeo wamekuta patupu. Huku CHADEMA watu tunahatarisha maisha yetu bila hata sumni. Mimi sijawahi hata kuonana na Mbowe na Mnyika au Tundu Lissu. Lakini tunakomaa mpaka CCM itoke madarakani.
7. CHADEMA inasemwa sana kwa mazuri na mabaya, hii ni kwa sababu ndiye mchezaji mwenye mpira. Mtangazaji wa mpira mara zote humtangaza mchezaji mwenye mpira.
CHADEMA is my loving, my amazing and my awesome Political Party, I dedicate to Tanzanians. Nitafia CHADEMA…………………………………….Mungu niweke hai mpaka nishuhudie CHADEMA ikiingia madarakani na kufanya kazi yako.
...............................................................................................................................

Hii ni vita ambayo tutashinda.Tutabadili silaha na position lakini target ni ileile