Chadema Iringa wampa mbunge wao siku 7 ajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Iringa wampa mbunge wao siku 7 ajiuzulu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  HALI ya kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo la Iringa Mjini si shwari.

  Hali hiyo inatokana na kuibuka kwa kundi la baadhi ya wanachama linalompinga mbunge wao, Mchungaji Peter Msigwa na kumtaka ajiuzulu nafasi ya uongozi wa chama ndani ya siku saba.

  Msigwa ambaye ni mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia chama hicho, pia ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa.

  Kundi hilo linaloongozwa Abuu Changawa aliyekuwa mgombea udiwani wa kata ya Kwakilosa na ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa kata hiyo, mjini hapa, lilitoa tamko linalomtaka Mchungaji Msigwa kujiuzulu wadhifa wake wa uenyekiti juzi lilipokuwa likizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Luxury Bar, mjini hapa.

  Changawa na kundi lake hilo, wanamtuhumu Mchungaji Msigwa kukihujumu chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na uchaguzi wenyewe, tuhuma ambazo Mchungaji Msigwa amekanusha kuhusika nazo pamoja na kupuuza ombi linalomtaka kujiuzulu baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi.

  Changawa alisema Mchungaji Msigwa anapoteza sifa ya kuendelea kuwa kiongozi wa chama hicho kwa madai kwamba katika uchaguzi huo, hakuwa anawafanyia kampeni wagombea wake wa udiwani, sababu iliyokifanya chama hicho kiambulie kiti kimoja tu kati ya 16 vya mjini hapa, tofauti na majimbo mengine ambako Chadema walishinda ubunge na kupata viti vingi vya udiwani.

  Hata hivyo Mchungaji Msigwa, hakuwa tayari kuyatolea ufafanuzi madai ya kundi hilo la wanachama, zaidi ya kusema kwamba hayana ukweli wowote juu yake na wanaomtuhumu wawasilishe malalamiko yao kwenye vikao halali vya chama.

  Alisisitiza kwamba, hatishiki na tamko la watu wanaomtaka ajiuzulu na kuongeza hatajiuzulu kama wanavyomtaka.
   
 2. M

  Mzalendoo Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hivi huyo diwan na vibaraka wenzake wamefadhiliwa na nan kutaka kumshushia hadh mbunge na chama? Hawajui huko ni kunzsha migogoro iso kuwa na kichwa,shame upon them.tuungane tupganie katiba mpya na fedha za dowans zirud.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  kazi ipo
   
Loading...