CHADEMA inaunga mkono Rasimu ya Katiba mpya - Mbowe

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema chama chake kinaunga mkono rasimu ya Katiba mpya iliyotolewa na Jaji Joseph Warioba.

Mwenyekiti huyo alikuwa akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi wa jiji la Mbeya katika mkutano wa kumnadi mgombea udiwani wa kata ya Iyela kwa tiketi ya Chadema Charles Nkelwa.

Kiongozi huyo wa upinzani bungeni amesema sababu kubwa ya kuunga mkono rasimu hiyo ni kwamba mambo mengi yaliyoorodheshwa na chama hicho yamekubaliwa.

Mbowe amesema jambo kubwa lililofanyiwa kazi ni kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika. Mbowe amesema amesikitika kuona baadhi ya wanaCCM wakiipinga serikali ya Tanganyika na kung'ang'ania serikali mbili na kudai watu hao ni wanafiki wanaopaswa kupuuzwa na wananchi.

Kauli ya Mbowe imekuja wakati ambapo mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Dr Kitila Mkumbo alinukuliwa kusema rasimu mpya ya Katiba iliyotolewa na Warioba ni bora mara mia mbili akilinganisha na katiba ya sasa.

Mara baada ya mkutano huo maelfu ya watu walitanda barabarani kumsindikiza kiongozi huyo anayependwa sana jijini Mbeya.

Source:
Mwananchi Jumatatu.
 
Mtu mwenye akili zake timamu lazima aunge mkono Serikali 3 maana ndio njia pekee ya kunusuru Muungano maana Serikali 2 iliganda kwenye tope na Serikali 1 ni ndoto
 
Mtu mwenye akili zake timamu lazima aunge mkono Serikali 3 maana ndio njia pekee ya kunusuru Muungano maana Serikali 2 iliganda kwenye tope na Serikali 1 ni ndoto

Ni kweli mkuu.Anayeipinga hana nia njema na Taifa hili.
 
kwani ni lazima kila mtu aunge mkono Serikali tatu? Inawezekana wale wanaodai serikali moja wana hoja zaidi kuliko wanaodai serikali tatu. KUtofautiana huku haina maana wenye kudai serikali tatu basi wanaitakia Tanzania mema zaidi kuliko wanaotaka serikali moja.
 
Naona wenzako wamekugeuka tena wanakuambia anayepinga serikali tatu alitakii mema taifa.
 
Issue ya serikali tatu nitaipinga bila kujali nani anaiunga mkono!
 
Inamaana mbowe anakubaliana na rais kuteuwa mwenyeketi wa tume ya uchaguzi? Anakubaliana jimbo kutoa wabunge wawili? Anapingana na mwanzilishi wa chama chake kuhusu serikali tatu?
 
tatizo kwetu watanzania tunajua kusikiliza lakini atujui kunukuu by the way ni haki kama mtanzania kutoa maoni yake
 
Inamaana mbowe anakubaliana na rais kuteuwa mwenyeketi wa tume ya uchaguzi? Anakubaliana jimbo kutoa wabunge wawili? Anapingana na mwanzilishi wa chama chake kuhusu serikali tatu?

Habari ndiyo hiyo na leo CCM nao wanaunga mkono rasimu ya katiba basi shughuli imeisha, Mbowe ndiyo kaishaamua nani atapinga.
 
MM ushabiki wa CDM umempotezea umaarufu, sasa anatapatapa.

MM hajawahi kutapatapa hata siku moja. Uwezo wako wa kukokotoa meseji zake MM tu ndo tatizo ulilo nalo wewe. Unao uweza kutofautisha meaning na implied meaning katika kila tamshi la kisiasa wewe? Au we unafikiri kila yes ni yes na kila no ni no... Mwache Mzee Mwanakijiji. apumue
 
Inamaana mbowe anakubaliana na rais kuteuwa mwenyeketi wa tume ya uchaguzi? Anakubaliana jimbo kutoa wabunge wawili? Anapingana na mwanzilishi wa chama chake kuhusu serikali tatu?

Mie nadhani anaamini hii mpya ina nafuu sana kulinganisha na ya zamani, japo pia ina matobo!
 
kwani ni lazima kila mtu aunge mkono Serikali tatu? Inawezekana wale wanaodai serikali moja wana hoja zaidi kuliko wanaodai serikali tatu. KUtofautiana huku haina maana wenye kudai serikali tatu basi wanaitakia Tanzania mema zaidi kuliko wanaotaka serikali moja.

Unapopendekeza serikali 1 au 2 inabidi utoe pia suggestion ya jinsi gani tutaadress issues za Muungano mathalani jinsi ya kushea rasilimali na kugarantee identity/autonomy ya nchi washirika bila kuuvunja muungano ambavyo vimekua ndio kero za muungano wetu kwa mda sasa na vinatishia the very existence yake. In part rasimu inatoa formula ya hizo issue 2, sasa proponents wa structure nyingine wanatakiwa kusuggest formula na sio tu kusema ni structure gani wanapenda au kuwa serikali tatu ni gharama!
 
Mkuu Molemo serikali tatu ndio mpango mzima

Mkuu ni lazima tuwe wakweli.Wakati mwingine kupinga kila kitu haifai.Kamwe wazanzibari hawawezi kuua utaifa wao eti kwa kukubali serikali moja.Pili kuendelea kuwa na serikali mbili ni unafiki wa hali ya juu.Option iliyobaki ni mfumo wa serikali tatu kama ilivyo kwenye sera ya Chadema kuhusu Muungano.
 
Last edited by a moderator:
MM hajawahi kutapatapa hata siku moja. Uwezo wako wa kukokotoa meseji zake MM tu ndo tatizo ulilo nalo wewe. Unao uweza kutofautisha meaning na implied meaning katika kila tamshi la kisiasa wewe? Au we unafikiri kila yes ni yes na kila no ni no... Mwache Mzee Mwanakijiji. apumue

Anatapatapa kuna uzi wake upo jukwaa la katiba anasema watanzania kataeni serikali tatu, hapa Mbowe anataka serikali tatu, wewe unataka serikali ngapi?
 
Mtu mwenye akili zake timamu lazima aunge mkono Serikali 3 maana ndio njia pekee ya kunusuru Muungano maana Serikali 2 iliganda kwenye tope na Serikali 1 ni ndoto
Sio Kweli kuwa watu wanaipenda tatu isipokuwa wanajua ikija itasaidia kuvunja muungano kama ilivyotokea URUSI ENZI YA AKINA YESTIN hivyo wanataka serikari angalau kuepuka kuilea Zanzibar
 
Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom