CHADEMA inatumiaje upande wa pili wa shilingia wa amri "batili" ya Magufuli?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
Moja ya maagizo au niseme amri ambazo Raisi Magufuli analaumiwa na kulaaniwa nazo ni kitendo cha kubinya demokrasia nchini kwa kupiga vita shughuli za siasa haswa zenye sura za kitaifa pamoja na ziara za viongozi wakuu wa vyama wa taifa mikoani na majimboni.

Amri ni amri, na amri ya kiongozi ni sheria, hata kama ni ya "kidikteta".

Ninachokiona hata hivyo ni uelekeo wa vyama vya upinzani, CHADEMA for that matter, kulemaa kisa kikiwa kulalamikia amri hii ya Rais, however unlawful it remains.
Wapinzani wajue uimara wa nyumba ni msingi, uimara wa miti ni mashina na mizizi yake! Leo kwa mfano hakuna harakati zozote zinazofanyika kueneza, kujenga kuimarisha vyama hivi katika ngazi za chini. Ikiwa huko ndiko kwenye Wanachama na wapiga kura.
Hivi tuamini viongozi walioko huko, wa majimboni, mikoani, walayani na kwenye kata, vijijini, matawini na kupitia wabunge (kwenye majimbo yenye wabunge) hawana wanaloweza kufanya kujenga vyama vyao, kuongeza wanachama na kutoa elimu ya uraia huko mpaka waende kina MBOWE, SEIF, LISSU, MNYIKA na Wengineo.

Viongozi amkeni, toeni semina kwa wale wa chini, watumeni kazi na walete taarifa ya utekelezaji. Kwa staili hiyo naamini watawaandalia njia na kazi ya viongozi wakuu itakuwa nyepesi na madhubuti kuliko ilivyo sasa, kwamba vyama vinaenezwa, kujengwa na elimu ya uraia hutolewa kwa maana hiyo kipindi cha uchaguzi!

CHADEMA/UKAWA kumbukeni Education is power and is the mother of knowledge!
 
Back
Top Bottom