CHADEMA inasambaratika au inaimarika?

Huu mpasuko ndani ya CHADEMA je unaimarisha chama au unakisambaratisha?
Vita ya panzi ni furaha kwa kunguru.

Sijapata mantiki sawia juu ya yatokeayo CHADEMA, ukiangalia kwa umakini utagundua aidha ilikuwa ni wimbi la uchaguzi mkuu kwa watu kuibukia na kupata waliyokusudia (nafasi za ubunge/udiwani) ama ni hali ya umamluki uliokithiri. Hainiingii akilini mwangu kuona ni katika kipindi kifupi saana tangu uchaguzi umalizike tukishuhudia malumbano mazito ya kutishiana, kunyoosheana vidole, kutoaminiana na kutoshirikiana miongoni mwa wana-chadema.
Tukitarajia kupata majibu murua ya tathmini ya chadema kwa uchaguzi uliopita bila ya majibu...majibu yamegeuka na kuwa malumbano yasiyotoa dira ya tija kwa taifa letu na hivyo kuonyesha bado hatujawa na upinzani kamili wa kuleta mabadiliko.
Nionavyo: Chama kinayumba na muelekeo wa wenye uchu ni...kukisambaratisha huku KUNGURU akifurahia, tutafakari.

NI MAONI YANGU BINAFSI YASIYOEGEMEA PANDE YOYOTE, nawasilisha!!
 
Umenena vyema sana mkuu

Mkuu kuishi kwingi ni kuona mengi
Nafikiri migogoro katika chama chochote cha siasa ni kawaida kutokea, na umakini na kufaulu katika utatuzi wake ndio kukomaa kwenyewe kwa Chama. Penye wengi pana mengi
 
Huu mpasuko ndani ya CHADEMA je unaimarisha chama au unakisambaratisha?
Vita ya panzi ni furaha kwa kunguru.

CDM chuma cha pua zaidi ya mr 6-mr 6 aliyumba lakini CDM iko pale pale-msimamo ule ule!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom