Chadema inapaswa kukarabatiwa sasa...

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,515
2,000
Ziondoshwe mbao kuukuu na mpya zitiwe... wenye fikra mgando na ung'ang'anizi wa madaraka waondolewe, wenye fikra pevu na uwezo mkubwa wa maamuzi waingie madarakani. wenye jazba na kukosa uvumilivu wa kisiasa wakae kando, wenye weledi wa siasa na mambo mbalimbali ya mahusiano na wenye itikadi tofauti. Wasiokubali kupingwa kwenye maamuzi wajitoe na wanaokubaliana na demokrasia waingie.... ili UKAMILIFU WA LILE NENO: CHAMA CHA MAENDELEO NA DEMOKRASIA yatimie. La kama si hivyo basi kitabaki kuwa chama cha Maendeleo ya wasiotaka Demokrasia!!

Hapa ndipo utakapojua kwamba Mh. Zito anawazidi mbali sana viongozi wengi wa Chadema na ndio maana sasa wanamuona kama mwiba kwao, ila kiukweli anabaki kuwa mtu stahiki wa kuiongoza CHADEMA.....
 
Vica

Member
May 27, 2008
84
0
huyu ZITO (MWANAMAGEUKO) asitake kutuchanganya tushamjua anataka kuvuruga chama..njia anayotumia sio nzuri...
 
mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,874
2,000
Watu wengine bwana, unazunguuuka wee mwisho unamalizia hakuna kiongozi kama zito! Ole wao waletae maudhi. Wachawi ni watu wasiopenda kuona wenzao wakiwa na furaha ya maisha. Wewe ni mchawi na mwanga, usitake watu waongee mambo ambayo hawakutaka kuyaongea.
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,515
2,000
Vyovyote vile msemavyo, penye uvundo hapatiwi ubani, jino bovu hung'olewa! cha ajabu ni kwamba watu fikra wanazifunika na kufuata ushabiki. na siku zote wavivu wa kufikiri huangalia jambo kwa upande wanaoupenda hata kama ni mbovu bila kutazama mazuri ya upande wasioutaka...

Chadema si mama wala baba wa yeyote... Ilikuwako TAA, TANU, ANC, ASP nk. leo havipo na maisha yanaendelea... Niliwaambia na narudia tena hapa: KIONGOZI YEYOTE ANAEHAMA-HAMA VYAMA HAFAI, nikawapa kazi ya kuchunguza ili mpate maarifa na ujuzi. Siasa ndio maisha, siasa ndio muelekeo na mustakabali wa mambo mengi. Lakini pia mnapaswa kujua SIASA NI UONGO WENYE MANUFAA kwa nani na kwa wakati gani. Ndio maana WANASIASA WAKWELI HAWAPENDWI :teeth:

Zito anaona mbali nasisitiza, alipowaambia kununua ile mitambo 'tulisema amenunuliwa na Mafisadi" leo mnalipa mamilioni mtatupia lawama upande mwingine WATANZANIA.... sijui tumirogwa au tunatumia akili za kuazima???:embarrassed:
 
watarime

Senior Member
Oct 21, 2010
105

ZITTO hasafishiki kwa kusaliti watanzania na wapenda mabadiliko

Aende tu CCM au CCM B maana dalili zote zinaonyesha hivyo!

Na ww kama co Zitto mwneyewe, utakuwa umehongwa ili kuja kupost ujinga wenu hapa JF

Zito anaona mbali nasisitiza, alipowaambia kununua ile mitambo 'tulisema amenunuliwa na Mafisadi" leo mnalipa mamilioni mtatupia lawama upande mwingine WATANZANIA.... sijui tumirogwa au tunatumia akili za kuazima???:embarrassed:

Watanzania wa leo co wale wa mwaka 47 mujue wanajua kabisa tabia ya ZITTO imebadilika co yule waliye mtumainia miaka 3 Nyuma bali ni Zitto aliye poteza muelekeo machoni na mioyoni mwa jamii na taifa kwa ujumla.
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,515
2,000
Watanzania wa leo co wale wa mwaka 47 mujue wanajua kabisa tabia ya ZITTO imebadilika co yule waliye mtumainia miaka 3 Nyuma bali ni Zitto aliye poteza muelekeo machoni na mioyoni mwa jamii na taifa kwa ujumla.
Hata ya marehemu Chacha Wangwe ilibadilika. Je kwanini wanaonekana wamebadilika? Iko hoja ya kujiuliza "je kule ndani wanapohoji jambo hupata majibu sahihi? Je ni kweli yale wanayopingana wale wengine huwa wako sawa? Ama ndio yale mkubwa hakosei?" Nilipata kujibiwa hapa kuhusu Zito na ole Sendeka :teeth:
Ni kweli katika uchokozi ule nilipata baadhi ya maoni kama nilivyokusudia na wapo wengine walinipa picha mpya kabisa ambayo sikuwa nayo lakini pia katika mjadala ule wengi walijibu kwa jazba!! hawakujua nini kilitakikana.

Lakini kwa hili nisemalo: kama wamazo mgando yataendelea basi tujiulize tutatoa kina kafulila wangapi na mwisho wa siku CHADEMA itabaki makapi ndio maana nasema huu ni muda sahihi wa kukarabati. ama si vibaya wacha wafiche moshi mlipuko ndio utakaotoa majibu :teeth:
 
Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,398
1,250
Marando at work. It happened to NCCR-Mageuzi before. You were warned.
 
KERENG'ENDE

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
398
195
Mwanamageuko
Nikwelikabisa CDM inahitaji kukarabatiwa sasa kwakuondoa uchafu usio stahili katika chama na kuacha damu changa zifanye kazi hatuhitaji watu walio tawariwa na sifa na matakwa yao binafsi na hatuhitaji chama kiwe chini ya mtu fulani au mlengo wa mtufulani tunahitaji chama kama itikadi na mlengo fulani ambao unaaminiwa na jamii.CDM angalieni mtu huyu anayeitwa zitto Zuberi Kabwe atapoteza matumaini ya wananchi kwa chama,angalieni taratibu zinasemaje nazifuatwe juu ya mtu huyu isijarishe kuwa mmemwandaa toka zamani........Jaribuni kumkanya kupitia vikao halali vya chama.....aonywe kupitia njia sahihi asipo badilika basi tumwache akaungane na Masumbuko lamwai,Thomasi Ngawaia,Hiza Tambwe bilakumsahau kakayake Waridi Kaburu nawasaliti wengine wanamnahiyo....
 
kweleakwelea

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
3,058
2,000
kwani? hii nafasi ya unaibu katibu mkuu wa chama inapatikanaje? mie naomba fomu mnifanyie inavyuu! itabidi niache ajira yangu nihamie kwanza makao makuu! zito timka bana! CCM patachimbika!
 
Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,883
0
Zito ni msaliti wa wapinzani kwanza kabla ya yote atuambie amepata wapi hela ya kununua hammer.na ni kwa nini toka awekwe kwqenye ile kamati ya madini kauli zake zimekuwa za utata kila kukicha? Na kama nia yake ni nzuri kwa cdm na taifa kwa jumla.
Huyu mtu ile kauli ya kutaka kununua mitambo ya dowans ndiyo imempa hizo hela zinazomtia jeuri na kujiona yeye ndio yeye sasa sisitunaojua mwisho wa mafisadi tunamtahadharisha kuwa safari aliyiianza si salama na hao anaofikiri kunguru wenzake amekosea hao ni tai..sisi tunapigania usawa wa kipato yeye anakuja na maisha ya kimarekani je akikamata nchi atakuwaje/ na atahitaji gari ya aina gani?Nasisitiza zito atimuliwe mara moja.
 
Kishili

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
295
195
Ziondoshwe mbao kuukuu na mpya zitiwe... wenye fikra mgando na ung'ang'anizi wa madaraka waondolewe, wenye fikra pevu na uwezo mkubwa wa maamuzi waingie madarakani. wenye jazba na kukosa uvumilivu wa kisiasa wakae kando, wenye weledi wa siasa na mambo mbalimbali ya mahusiano na wenye itikadi tofauti. Wasiokubali kupingwa kwenye maamuzi wajitoe na wanaokubaliana na demokrasia waingie.... ili UKAMILIFU WA LILE NENO: CHAMA CHA MAENDELEO NA DEMOKRASIA yatimie. La kama si hivyo basi kitabaki kuwa chama cha Maendeleo ya wasiotaka Demokrasia!!

Hapa ndipo utakapojua kwamba Mh. Zito anawazidi mbali sana viongozi wengi wa Chadema na ndio maana sasa wanamuona kama mwiba kwao, ila kiukweli anabaki kuwa mtu stahiki wa kuiongoza CHADEMA.....
Ni kweli inahitaji kukarabatiwa Zitto aondoke kwani mapenzi yake kwa JK na CCM yanapitiliza hivyo angefanya kazi nzuri sana akiwa CCM. Tulimhitaji Zitto aliyekuwa akipambana na ufisadi siyo anayepamba ufisadi. Hatuhitaji Zitto aliyekaribu zaidi na akina Rostam na Karamagi kuliko viongozi wenzie wa chama. Hatumhitaji Zitto anayetoa taarifa za utendaji wa kazi za chama kwa Zoka( naibu mkurugenzi mkuu wa usalama) badala kupeleka kwa viongozi wenzie. Hajui kuwa usalama wa taifa ni usalama wa CCM kwanza? kama demokrasia maana yake ni party suiside basi hata neno hilo halina maana tena
 
Mchili

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
725
195
Kwani ni lazima Zito aongoze? Viongozi si wanachaguliwa? Kwa nini asisubiri uchaguzi? Na hao wazee unaotaka waondoke wampishe Zito ni kina nani si uwataje?

Zito mara anaomba uwaziri, mara kiongozi wa upinzani bungeni!! ana matatizo gani??
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,515
2,000
Zitto for CDM chairman! campaigns have started!
Yes Waberoya, na ndio maana wapinzani wake kwa sababu hawana hoja wanapandikiza chuki, mara yeye ni ccm, mdini n.k. lakini bado ndio anabaki kuwa alama sahihi ya uongozi wa CDM kama hawa wanaompinga hapa ni wakweli waseme: Je Mh. Mbowe amepata kumkataa JK? watuoneshe popote ushahidi wao. na nimewauliza je ilikuwaje Dr. Slaa akagombea urais sijapata majibu kwao.... watajibu simply, chama kiliamua what the secret behind? nilichokoza katika mjadala mmoja hapa "nilitaka watu waione tofauti baina ya Zito na viongozi wengi wa Chadema" kwa bahati mbaya wengi hawakutaka kuona nilimaanisha nini. Walijibu kwa jazba na narudia tena ni hao hao wanaomponda Mh. Zito hii leo... Wanadhani nyumba inajengwa kwa kubomolewa!
narudia tena: CHADEMA INAHITAJI KUKARABATIWA UPYA la sivyo haina mwendo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom